Kumbe hata CCM huwa inachacha?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Ndiyo sababu wakaona bora wakupue mabilioni ya EPA ili kugharamia uchaguzi mkuu wa 2005. Wanachama hawatoi tena ada, wameshashtuka!

Date::8/25/2008
Ukata wakwamisha mchakato wa uchaguzi Vijana CCM
Na Kizitto Noya
Mwananchi

UHABA wa fedha umevuruga mchakato wa uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kusababisha baadhi ya vikao vya ndani vinavyochuja majina ya wagombea, kusogezwa mbele.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa UVCCM Francis Isack, zinasema kuwa kikao cha Baraza Kuu la UVCCM kilichotakiwa kufanyika Agosti mwaka huu, kimesogezwa hadi Oktoba kutokana na ukosefu wa fedha.

Kikao hicho kilitakiwa kufanyika mwezi Agosti ili kutoa fursa kwa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kukutana Septemba mbili na tatu mwaka huu kwa ajili ya kupitia majina ya wagombea hao na kutangaza washindi.

Kitendo cha Baraza Kuu kufanyika Oktoba, kimeathiri ratiba ya vikao vyote vinavyofuata baada ya Kikao cha Kamati ya Ukelezaji ya UVCCM kilichofanyika Agosti 16 na 17 mwaka huu mjini Dodoma.

Hata hivyo Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM Mtinga alisema mabadiliko hayo hayatabadili Desemba, kuwa mwezi wa kufanyika uchaguzi huo.

''Kikao cha Baraza Kuu kitakaa Oktoba katika tarehe ambayo hatujapanga. Kikao hicho kigumu kufanyika haraka kwa kuwa kina mambo mengi ya kuzingatia moja ikiwa fedha za kukiendeshea,'' alisema Mtinga.

Alisema kikao cha Baraza Kuu kinahitaji fedha kwa ajili ya kuwasafirisha wajumbe kutoka mikoa yote nchini na kuwalipa posho jambo ambalo kwa hali ilivyo, haliwezekani kwa sasa.

Kukwama kwa kikao hicho, kumevuruga pia ratiba ya vikao vya Kamati ya Maadili ya CCM na Kamati Kuu (CC) ambavyo taarifa za awali zimedai kuwa vilipangwa kufanyika Agosti 20 na 21, mwaka huu chini mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa kanuni za CCM katika uchaguzi huo, Kikao cha Baraza Kuu la UVCCM ni cha tatu kuchambua majina ya wagombea. Kikao cha kwanza katika mchakato huo ni Sekretarieti ya UVCCM na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo.

Kikao cha Baraza Kuu kinafuatiwa na Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu wake , Yusuf Makamba, Kamati ya Maadili ya CCM, Kamati Kuu (CC) na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Katika hatua nyingine Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Isack amebeza kuripotiwa kwa habari za matokeo ya vikao vya mchakato wa kuwachuja wagombea wa UVCCM akisema kuwa vikao hivyo havina maamuzi ya mwisho ya mchakato huo.

Akizungumza na gazeti hili jana Isack alisema yanayofikiwa na vikao hivyo sio maamuzi ya mwisho ya mchakato wa kuwapata wagombea hivyo habari zake zinaweza kupotosha jamii.

Isack alitoa kauli hiyo kufuatia habari zilizoripotiwa wiki iliyopita kuhusu maamuzi ya Kikao ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM kumuengua Nape Nnauye katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM kwa kumpa alama ya chini y E .

Alisema kikao hicho ni sehemu ya mchakato ya uchaguz huu na maamuzi yake ni mapendekezo ambayo yanaweza kubadilika wakati wowote hivyo habari zake zinaweza kupotosha jamii na kuvuruga mchakato mzima wa uchaguzi.

''Maamuzi ya ndani ya kikao sio kitu cha kuamini kwani uchaguzi ni mchakato na kwa kuwa ni maamuzi ya ndani yanaweza kubadilika wawati wowote kwa sababu muhimu,'' alisema.

Kwa mujibu wa Isack habari zinazopaswa kuripotiwa ni mwisho katika mchakato huo ambazo hutangaza washindi na ili habari hizo ziwe za kweli lazima yeye (Mtinga) azitoe kwa mujibu wa wadhifa wake.

Alisema Nape na wengine ambao walielezwa kuenguliwa katika mchakato huo, wanaweza kurudishwa na kikao hicho hicho au kingine na kuwa miongoni mwa washindi hivyo sio sahihi kuueleza umma kuwa baadhi ya wagombea wameenguwa katika moja ya vikao vinavyopitia majina hayo.

Siku tatu baada ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM kukutana Dodoma na kuwahoji wagombea wa nafasi ya mwenyekit wa UVCCM, kulipatikana taarifa kwamba kikao hicho chini ya mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk Emmanuel Nchimbi, kimemuengua mjumbe wa Halmashauri kuu CCM na Baraza Kuu la UVCCM Nnauye kuwania nafasi hiyo kwa kigezo cha umri.

Kauli ya Mtinga imeonekana kuunga mkono msimamo wa Nape kwamba Kamati ya Utekelezaji ya UVCMM haina mamlaka kisheria kukata jina la mgombea na kufanunua kuwa mamlaka ya maamuzi hayo yako katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

''Vikao vya chini havina mamlaka kukata jina la mgombea wanachofanya ni kujadili na kuweka alama na mimi waliniwekea alama mbaya ya E ikimaanisha kwamba sifai.

Hata hivyo kikao chenye mamlaka ya kukata jina na Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake RAis Jakaya Kikwete,'' alisema Nape.
 
Prof. Ndullu kawa mnoko, hawana kwa kuchota tena mapesa ya wananchi. Waende kwa RA, atawasaidia.

Hivi kweli chama chako unachokipenda, unataka ukienda kwenye mikutano mpaka ulipwe posho? Nitaelewa kama ni malazi na chakula lakini posho ya ziada? Kweli kuna umuhimu kwenye mikutano ya vyama?
 
Ndugu zangu,msifikiri hivi vitu vinakuja kimakosa ila vimepangwa.Vikao hivi vinashindwa kumuondoa Nape kwakuwa bado hajavuka umri unaotakiwa,lakini baada ya september nadhani atakuwa amepita umri unao takiwa kuwa mgombea uenyekiti Vijana.

Sasa basi inawezekana vinamlenga Nape na Bashe au ni kweli kuna ukata hatuwezi kujua haya mambo yanweza yakaonekana hivi kwa sura ya nje lakini kwa undani kuna agenda mbadala.

Nawasilisha.
 
Ndugu zangu,msifikiri hivi vitu vinakuja kimakosa ila vimepangwa.Vikao hivi vinashindwa kumuondoa Nape kwakuwa bado hajavuka umri unaotakiwa,lakini baada ya september nadhani atakuwa amepita umri unao takiwa kuwa mgombea uenyekiti Vijana.

Sasa basi inawezekana vinamlenga Nape na Bashe au ni kweli kuna ukata hatuwezi kujua haya mambo yanweza yakaonekana hivi kwa sura ya nje lakini kwa undani kuna agenda mbadala.

Nawasilisha.

HOJA YAKO NI NZITO NA INAHITAJI UFUATILIAJI WA KINA, inawezekana kuwa kuna jambo linahifadhiwa hapo...
 
Ndugu zangu,msifikiri hivi vitu vinakuja kimakosa ila vimepangwa.Vikao hivi vinashindwa kumuondoa Nape kwakuwa bado hajavuka umri unaotakiwa,lakini baada ya september nadhani atakuwa amepita umri unao takiwa kuwa mgombea uenyekiti Vijana.

Sasa basi inawezekana vinamlenga Nape na Bashe au ni kweli kuna ukata hatuwezi kujua haya mambo yanweza yakaonekana hivi kwa sura ya nje lakini kwa undani kuna agenda mbadala.

Nawasilisha.

Huu ndio uhakika, ni kweli huu ndio mkakati wa mwisho ku make sure that Nnape hapiti kwa kigezo cha umri. Ingekuwa Nnape kayatetea mafisadi Basi kina RA wangefadhili vikao vyote
 
Back
Top Bottom