Kumbe elimu bure inawezekana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe elimu bure inawezekana!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magobe T, Dec 21, 2010.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF, nilikuwa Algeria kwa wiki moja hivi na huko nimeonana na baadhi ya Watanzania, ambao wameamua kufanya kazi huko kuliko kurudi Tanzania kwa kile walichodai "viongozi wetu ndio wanaorudisha maendeleo nyuma".

  Nilipokuwa naongea nao, walinithibitishia kuwa huko Algeria elimu ni bure hadi chuo kikuu, kinachotakiwa ni juhudi za mwanafunzi tu. Hata allowance ya wanafunzi ni hela nzuri tu. Pili, walisema hata huduma za afya zinapatikana vizuri zaidi kuliko Tanzania ila wana utaratibu kwamba wanalipia 20% ya gharama, kwa namna ambayo inawafanya wapate huduma hiyo bila shida na bila ubaguzi wala ruhwa.

  Walisema kila wakikutana na viongozi wa Tanzania huwa wanawauliza kwa nini wasijifunze baadhi ya mambo yanayoenda vizuri Algeria na kuyafanya Tanzania - mfano uchimbaji wa madini unaoinufaisha nchi yetu.

  Nimeona niliseme hili kwani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu baadhi ya viongozi wa CCM walidai hakuna nchi duniani inayotoa elimu bure (badala ya kusema hawajui kama kuna nchi duniani inayotoa elimu bure).
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza nikupongeze sana ndugu yangu MAGOBE kwa thread hii nzuri hivi! japo mimi ndio mdau wa kwanza kuchangia...Lakini ningependa wadau wengi wa JF waione na wachangie maana kuna watu wakati wa kampeni pale DR Slaa Mgombea wa CDM aliposema elimu bure mpaka form six itatolewa na CDM watu walibenyua midomo sana,watu walichonga sana,watu walinyoosha midomo sana,Wakasema Dr Slaa mzushi hakuna kitu kama hicho!!! Hata mheshimiwa mkubwa wa KAYA naye akagonelea msumari eti! Elimu bure haiwezekani wengine wana SISI M wakubwa wakasema hakuna nchi inayotoa elimu bure!!!!!!!!! '' UNAFIKI HUU'' Sasa Ndugu yangu MAGOBE nazani Mungu alipanga utuletee hii habari. Najiuliza Watanzania tutadanganywa mpaka lini?
   
 3. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mwambie jk,atembelee na huko kwa kina maalimu ajifunze sio kwenda usa,,kusikana mkono na obama,
   
 4. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Unajua nn wakuu hawa jamaa wa SISI M wanavyosema hakuna nchi inayotoa elim bure sio kwamba hawajui,wanajua kuwa watanzania ni wajinga na wapumbavu tunalosema watakubali,hii kitu ndo huwa inanipa hasira natamani hata nikawalipue wote.Yaani huwa wanafanya vitu wakiona watu wote ni mazoba.Thread nzuri ikiwezekana isambaze kwenye majukwaa mengine wengine huwa hawafiki huku.
   
Loading...