Kumbe Chama cha Mapinduzi kinapendwa kiasi hiki?

Airmanula

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
3,760
5,264
Ukiingia kwenye mitandao ni CCM, CCM, CCM, hata wale wabunge wa upinzani wanaifuatilia Chama cha Mapinduzi, hakika chama hiki kinapendwa sana na watu.

Embu jaribu kuona ya kua, katika kura za maoni, wabunge wa upinzani wanashangilia watia nia waliondolewa katika kinyang'anyiro, na kuwafurahia wale walioshinda, hii inaonesha ya kua wanaamini CCM ni chama kizuri na kinafanya mambo kwa uwazi na kwa demokrasia ya hali ya juu, na wao wanasapoti kwa asilimia kubwa sana ndio mana unaona wako macho kufuatilia kila hatua katika kura za maoni sehemu mbalimbali nchini.

Hakika CCM ni chama tawala na chama pendwa kabisa, na tunaomba muendelee hivyo hivyo kukisapoti. Pia hata wale mnaowacheka waliohama vyama vya upinzania bado wataendelea kua wanachama wa CCM na zaidi nafasi katika serikali ziko nyingi na bado nchi inahitaji wachapa kazi, kwahio kufurahia kwenu kisihitimishe kua sasa ndio hawana lolote.

CCM ni chama kikubwa, pia serikali yetu ni serikali sikivu, na naamino hao waliobwagwa sio mwisho wa maisha. Teuzi bado ziko nyingi.

Kidumu chama tawala.
 
utapeli upi mkuu acha mihemko bwana mambo yanaendeshwa kisayansi kabisa, chama pendwa ndio mana mnafuatilia kwa ukaribu kila hatua, hii inaonesha mapenzi ya dhati mliyonayo kwa CCM mnahakikisha wanapita wagombea wazuri.
Sayansi ya jamii

Social science (sanaa)
 
Back
Top Bottom