Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Wakuu,
Yule Manju kama sio mbobezi wa masuala ya Fizikia na hesabu bwana Albert Einstein alipoandika papers zake ili atunukiwe shahada ya Udaktari(PhD) katika chuo kikuu cha Bern, alikataliwa na kuambiwa kwamba alichokiandika ni 'usanii tu' wala hakina uhalisia wa Fizikia wala mashiko hivyo hawezi kutunukiwa shahada hio ya juu kabisa.
Lakini tukumbuke huyo ndiye alichangia theory nyingi katika Fizikia ikiwemo ile formula maarufu ya E=mc².
Albert Einstein alizaliwa mwaka 1879 huko Ujermani na kufariki mwaka 1955 huko Marekani akiwa na miaka 76.
Hii,inatufundisha kwamba hata uwe haukubaliki vipi, hutakiwi kukata tamaa,songa mbele baadae wataona thamani yako.
Jionee kiambatanisho.
Asante.