Albert Einstein: Kutoka kuwa kilaza darasani hadi kuwa nguli wa fizikia

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
ALBERT Einstein ni mwanasayansi maarufu aliyeleta mapinduzi katika ulimwengu wa sayansi ambapo enzi za utoto wake walimu walimwita kilaza darasani.

Maisha ya awali ya Eistern hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu cha Intelligence Quotients- IQ (160-190).

Msomi huyu ambaye alianza kama mjinga, aligeuza ujinga wake kuwa mwanasayansi mashuhuri na katika historia ya duniani hatoweza kusahaulika.

Mwanafizikia huyu raia wa Marekani mwenye asili ya Ujerumani, alifanya mapinduzi ya sayansi ya fizikia, anajulikana zaidi kwa kugundua sayansi ya mabomu ya nyuklia.

Einstein alizaliwa mwaka 1879, huko Ulm, Ujerumani, alipata elimu ya awali katika mji wa Munich. Alikuwa mwanafunzi mwenye kiwango cha akili kidogo baadhi ya walimu wake walidhani kuwa ni walemavu wa akili (mentally handicapped); kutokana na kushindwa kuzungumza vizuri alipokuwa na umri wa miaka tisa.

Hata hivyo, alivutiwa na masuala ya asili ya ulimwengu. Alikuwa na hisia za ajabu ya kushangaza na aligundua kuwapo kwa nguvu isiyoonekana (Invisible forces) inayoongoza sindano ya dira (campass).

Alipokuwa na umri wa miaka 16 aliweza kufanya mahesabu ya kutatua na kufumbua masuala ya fizikia na uhandisi.

Einstein alimaliza elimu ya sekondari akiwa na miaka 16 na hakupenda kuendelea na masomo, akaamua kuachana nayo na kusoma mwenyewe huku akitafuta njia ya kuingia chuo kikuu.

Mwalimu wake akamfukuza kwa sababu ya mtazamo wake ambao ungeweza kuwaathiri wanafunzi wa darasa lake.

Einstein alijaribu kutuma maombi ya kujisajili na chuo cha Federal Institute of Technology (FIT) huko Zurich nchini Uswisi, lakini ujuzi wake wa masomo yasiyo ya hisabati hakuwa na uwezo nayo hivyo kusababisha kufeli mtihani wa kujiunga na chuo hicho.

Kwa ushauri wa mkuu wa chuo, alienda kujiunga na chuo cha Cantonal huko Aarau, Uswisi na kufanikiwa kupata diploma ambayo ilimwezesha kukubaliwa na chuo cha FIT mwaka 1896 ambapo alishindwa awali.

Akiwa hapo, alitambua uwezo wake mkubwa katika masuala ya fizikia kuliko hisabati.
Einstein alifaulu na kuhitimu katika chuo cha FIT mwaka 1900, lakini kwa sababu ya kutoelewana na mmoja wa profesa wake hakuweza kuendelea masomo kutokana na kukosa msaada wa fedha.
Mwaka 1902, aliajiriwa katika chuo cha Bern akiwa mkaguzi, nchini Uswisi, lakini baada kufikisha umri wa miaka 26 alitimiza vigezo vyote vya kumwezesha kufundisha chuo kikuu. Aliandika utafiti wake wa kwanza kuhusu mapinduzi ya sayansi.

Utafiti huo ulimpa umaarufu Einstein, na vyuo vikuu vikaanza kumgombania kwa huduma zake, mwaka 1909, baada ya kutumika kama mwalimu wa chuo cha Bern aliitwa kufanya kazi akiwa profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Zurich huko Uswiss. Miaka miwili baadaye alichaguliwa kuwa profesa kamili katika Chuo Kikuu cha Ujerumani huko Prague, nchini Czechoslovakia. Ndani ya mwaka mmoja na nusu akarudi katika chuo cha FIT akiwa profesa kamili.
Hatimaye, mwaka 1913, wanasayansi maarufu wa Max Planck na Walther Nernst walisafiri kwenda Zurich kumshawishi Einstein kukubali kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Berlin huko Ujerumani, pamoja kuwa mwanachama kamili wa Chuo cha Sayansi cha Prussia ambapo alikubali hiyo ofa.

Maisha ya awali ya Eistein hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu yaani IQ (Intelligence Quotients-160-190).

Einstein alianza kujulikana katika masuala ya Fizikia na umaarufu wake ulizidi kuongezeka kutokana na tafiti zake kukubalika, hatua ambayo ilizifanya kazi zake kupata sifa kem kem katika ulimwengu wa Fizikia.

Akiwa nchini Ujerumani, kipindi hicho chuki dhidi ya Wayahudi iliongezeka, Einstein alianza kupata mashambulizi kutoka kwa wanasayansi wenzake Philipp Lenard na Johannes Stark ambao walikuwa washindi wa tuzo za Nobel katika masuala ya Fikizia.

Wanafizikia hao walianza kuhusisha nadharia ya Einstein kuwa ‘fizikia ni Kiyahudi.’ (Theory of Relativity) hivyo, mwanasayansi huyu alijiuzulu kutoka Chuo cha Prussia cha Sayansi mwaka wa 1933.

Kwa mara kadhaa, Einstein alikuwa akitembelea Chuo cha California Institute of Technology nchini Marekani, ambapo safari yake ya mwisho mwaka 1933 alipewa nafasi katika Institute for Advanced Studies huku Princeton, huko Massachusetts.

Akiwa nchini Marekani, mwaka 1939 Einstein alikuwa mstari wa mbele katika utengenezaji wa bomu la atomiki, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo, Franklin D. Roosevelt kuelezea kuwa Wajerumani wamepiga hatua katika maendeleo ya sayansi, kwamba Adolf Hitler anaweza kuwa wa kwanza kutengeneza silaha za atomiki.

Hii ilichochea jitihada za Marekani kutengeneza bomu la nyuklia. Einstein alishtuka na kusikitishwa kutokana fumbo maarufu la Fikizia E = mc 2 ambalo lilionyesha njia ya kutumia katika kutengeza bomu la nyuklia ambalo lililolitumika kulipua mji wa Hiroshima nchini Japan, mwaka 1945.

Einstein alifariki Aprili mwaka 1955 kwa maradhi ya tumbo. Kabla ya kufariki, aliomba mwili wake uchomwe moto, lakini tukio la kushangaza mtaalamu wa magonjwa ya damu (pathologist), Thomas Harvey aliondoa ubongo wakati mwili wake ukifanyiwa uchunguzi. Harvey alichukua ubongo ili kutafuta siri ya kiwango cha akili yake (genius).

Baada ya kupata kibali ambacho kilikuwa kinakataliwa kutoka kwa mtoto wa kiume wa Einstein, Harvey baadaye aliukata ubongo wa Einstein vipande vipande na kuupeleka kwa wanasayansi mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi. Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusiana na ubongo wake tangu miaka ya 1980, lakini matokeo yake yamekuwa yakikataliwa au kutopewa heshima yoyote.

Lakini mwaka 1999, uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Canada ilichapisha utafiti wenye utata unaodai Einstein alikuwa na ukuta usio wa kawaida katika sehemu ya ubongo uliompa uwezo wa Hisabati.

Wakati Albert Einstein anaendelea kutengeneza fedha nyingi, ingawa alifariki mwaka 1955; mwaka huu jarida la Forbes lilimtaja katika nafasi ya 10 kuwa miongoni mwa watu waliokufa lakini wanaendelea kuzalisha fedha. Einstein mwaka huu pekee amezalisha Dola za Marekani milioni 10 kutokana na jina na sura yake kutumika katika bidhaa, mabango, kompyuta, roboti na mifuko.
 
Einsten ni noma, mwaka 1919 alisababisha wanasayansi wajae Africa baada ya kusema "during solar eclipse sun light will be deflected at 90 degree at the equator" on his theory of Reletivity. Kwa hiyo mwaka 1919 kulikuwa na total solar eclipse na ikweta inapita Afrika. Sasa yeye alipata tu kwa kutumia calcuation zake sio kupima, hivyo wanasansi walikuwa na shauku ya kuona ukweli na uwongo wa Einsten, waliamua kwenda huko kwenye ikweta ili wapime hiyo angle, mwisho wa siku Einsten akaibuka mshindi
 
Kumbee
Einsten ni noma, mwaka 1919 alisababisha wanasayansi wajae Africa baada ya kusema "during solar eclipse sun light will be deflected at 90 degree at the equator" on his theory of Reletivity. Kwa hiyo mwaka 1919 kulikuwa na total solar eclipse na ikweta inapita Afrika. Sasa yeye alipata tu kwa kutumia calcuation zake sio kupima, hivyo wanasansi walikuwa na shauku ya kuona ukweli na uwongo wa Einsten, waliamua kwenda huko kwenye ikweta ili wapime hiyo angle, mwisho wa siku Einsten akaibuka mshindi
 
Wazungu siwaaminiigii saaanaa..wamekaaa kujifanyaga wanajua kila kitu, japo of course wanajua kila kitu. Afrika maginiaz tupo wengi huenda na wewe ukawa mmoja wapo lakini mazingira tunakulia, aina za familia tulizonazo n.k. Ni nani atakaa chini ya mti anaenjaa anasubiri tunda lianguke ale. Mwenzetu tunda au jani limeanguka mtini ameshatengeneza na kufikiria theory. Kwanini tunatembea hatuanguki kwenye sayari hii ya dunia na inasemekana kwenye sayari ingine huezi tembea?

Tutasema yote mwisho wa siku mwanzo ndo msingi wa kila kitu.
 
Huwa nahisi kuna siri kubwa kwenye vyakula tunavyo kula, ukiachilia mbali mfumo wetu wa elimu. Mbona hatugundui na kuvumbua km wazungu? Japo tunapata AAA za PCM etc.
Theoretical tutapata hata a+ lakini kuiaaply hiyo a+ kwenye real life situations hapo ndo kimbembe...elimu ya Tanzania imetudhulumu saaana sisi wasomi local. Ada 1.6 m lakini kukiapply tulivyosoma collage ni mtihani mwingine. Ili tufike pale mambo mengi yanapaswa kubadilishwa..kuanzia mfumo mzima wa elimu mpaka mitaala.
 
Wazungu siwaaminiigii saaanaa..wamekaaa kujifanyaga wanajua kila kitu, japo of course wanajua kila kitu. Afrika maginiaz tupo wengi huenda na wewe ukawa mmoja wapo lakini mazingira tunakulia, aina za familia tulizonazo n.k. Ni nani atakaa chini ya mti anaenjaa anasubiri tunda lianguke ale. Mwenzetu tunda au jani limeanguka mtini ameshatengeneza na kufikiria theory. Kwanini tunatembea hatuanguki kwenye sayari hii ya dunia na inasemekana kwenye sayari ingine huezi tembea?

Tutasema yote mwisho wa siku mwanzo ndo msingi wa kila kitu.
Kuna kijana alitengeneza bom lenye uzito wa juu alikamatwa Mara mwungine katengeneza radar kakamatwa mwingine redio kashtakiwa mwingine katengeneza helicopter sijui yuko wapi hawa wange wezeshwa au wangeenda kupimwa IQ nahis ingefika 200
 
Kuna kijana alitengeneza bom lenye uzito wa juu alikamatwa Mara mwungine katengeneza radar kakamatwa mwingine redio kashtakiwa mwingine katengeneza helicopter sijui yuko wapi hawa wange wezeshwa au wangeenda kupimwa IQ nahis ingefika 200
Hapo ndipo tulipokomea. Hatuangalii the other side of coin. Tanzania ya viwanda ni meipenda kwa moyo yote coz rasilimali tunazo, hapa nazungumzia malighafi. Rasilimali watu bado. Technolojia kwetu bado tatizo. Kampuni za simu zote ma co na executive officers ni wageni most of them. Kwanini? Ndivyo tulivyo. Aliyetengeneza rada awe sponsored, apelekwe kwenye vyuo mashuhuri ajifunze aje atusaidie. Tuende tukajifunze kwao, wao wanafanyaje na sisi tushindwe.

Kwa sasa hakuna cha kugundua kipya mpaka kesho theory za isaac newton na albert bado wanazitumia wazungu. Tufundishe kile kitakachomsaidia mwanafunzi mara baada ya kuhitimu masomo yake kwa maana elimu yake hapo ndipo inapoanzia.
 
izzo tusaidie hapa
Bomu la nuclear na Hydrogen bomb yote yanatumia mfumo unaojulikana Kama Nuclear fission ambapo wanatumia Uranium 235 au Plutonium yani E=MC2 yani Energey = Mass X Speed of light square yani kiwango kidogo cha Mass kinaweza kuzalisha kiwango kikubwa cha Energy kama unatengeneza silaha kiwango kidogo cha Uranium 235 kama cha mfuko wa Kg 20 mlipuko wake unaweza kuwa sawa na Tani 20 za baruti TNT Atomic bombs zikilipuka zinaacha kiwango kikubwa cha atomic fuel ambacho ndicho kinatoa radiations

Hydrogen bombs chanzo chake ni baada ya Atomic bombs na pia zote zinatumia malighafi za aina moja yani Uranium 235 na Plutonium mlipuko wake unatoa kiwango kikubwa cha nishati. Protium, Deuterium, Tritium lakini hapa tutazungumzia Deuterium na Tritium
Hydrogen ina isotopes tatu ambazo ni Deuterium na Tritium na Protium lakini kwenye Hydrogen Bombs zinatumika Deuterium (1 Proton na 1 Neutron) wakati Tritium ni (1 Proton na 2 Neutrons) hizi Isotopes mbili za Deuterium na za Tritium zikichanganyika pamoja zinatengeneza kitu kinaitwa fusion mchanganyiko huu kwa pamoja unatoa nishati nyenye joto kubwa sana karibu kiwango cha nyuzi joto million 50 yani thermonuclear bombs devices .


Bomu kubwa la Hydrogen ambalo linajulikana kama Tsar Bomba(AN602) ambalo ni 3 stage Hydrogen Bomb japo zinaweza kufika mpaka 7 stage lakini kubwa kabisa kwa sasa duniani ni 3 stage hydrogen ambalo ambapo ujazo na uwezo wake wa mlipuko ni sawa na Kiwango cha baruti cha tani elfu 5000 Note Hydrogen bombs zinatoa kiwango kikubwa sana cha nishati kuliko Atomic bombs zaidi ya mara 1000 cha Atomic bombs Msokwa1
 
izzo mkuu nashukuru kwa maelezo yako yaliyo shiba...
Swali. Hivi Tz kuna uwezekano nasi tukafika kwenye hio techn na inaweza garimu muda na fedha ngapi?

NB. Mkuu unapotea sana tunamiss michango yako humu
 
izzo mkuu nashukuru kwa maelezo yako yaliyo shiba...
Swali. Hivi Tz kuna uwezekano nasi tukafika kwenye hio techn na inaweza garimu muda na fedha ngapi?

NB. Mkuu unapotea sana tunamiss michango yako humu
Kwa Tanganyika mpaka kuweza Kuwa back Technology hii sidhani tuna vitu vingi Sana vya kufanya kuliko kujiingiza kwenye matatizo haya name kwa uzembe WA watu weusi sidhani Kama tunaitaji technology hii japo kwa sasa ni muhimu sana hasa kwa mambo ya source of energy

Nishati pekee ambayo dunia inategemea yani Mafuta na Gas inakwenda kuisha pia ni gharama sana kuendesha nishati hizo mpaka sasa 17% ya umeme duniani unazalishwa kwa nishati ya Nuclear huku Ufaransa 75% ya umeme wanaotumia niwanishati ya Nuclear Duniani kuna Nuclear reactor 440 ambazo zinazalisha umeme wa 390,000 megawatts (MWe) katika nchi 31 pia kuna Nuclear reactor 60 zinajengwa maeneo mbalimbali duniani na zingine 160 zinatarajiwa kujengwa so unaweza kuona matumizi ya Nuclear kuzalisha nishati yakizidi kuenea Duniani pia kuna reactor ndogo ndogo 200 zinazooperate kwenye meli na submarine 150
Nuclear reactor yenye 508 MW capacity ndani ya saa 24 inaweza kuzalisha umeme wa 12,192 megawatthours (MWh) pia kutengeneza bomu la Nuclear ni process kubwa sana si kumiliki kinu cha umeme cha nuclear ukaweza kutengeneza bomu, kwani zipo Uranium za aina mbili yani Uranium-238 (U-238) na uranium-235 (U-235) sasa maajabu ni kuwa Uranium-238 (U-238) ndio nying sana duniani karibu 99.3% huku Uranium 235 (U-235) ambayo ndio unaweza kutengenezea bomu la Nuclear ni 0.7% ya hifadhi yote duniani toka mwaka 1789 bwana Martin Klaproth mwanasanyansi wa Kijerumani alipogundua madini ya Uranium na mpaka uweze kutengeneza Bomu moja la Nuclear unaitaji kuwa na 50KG za Uranium 235(U-235) hili kuweza kukamilisha chain reaction kitu ambacho ni kigumu sana na inachukua miaka mingi sana
 
Back
Top Bottom