Kulipigania penzi kunaweza kuwa ndio sababu ya anguko lako na majuto ya milele maishani mwako.....weka ukomo wa uvumilivu....(True story)

Kulipigania penzi kunaweza kuwa ndio sababu ya anguko lako na majuto ya milele maishani mwako.....weka ukomo wa uvumilivu....(True story)

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,759
Reaction score
39,493
Habari za muda huu waungwana wa hapa.....

Leo nimemkumbuka mdogo wangu wa kike mtoto wa mama yangu mdogo.....
Mdogo wangu ambaye alikuwa binti ambaye familia ilikuwa na matumaini makubwa sana kwake kutokana na wajihi na tabia zake njema.......

Kwa kufupisha story safari yake ya kielimu ikamfikisha kwenye fani ya ualimu wa shule ya msingi....na kwa bahati nzuri aliwahi kupata ajira bado binti mdogo tu.........

Katika kupambana na upweke akakutana na kijana ambaye kwa wakati huo hakuwa na ajira lakini kama unavyojua PENZI ni upofu dada akazama na ndoa ikafungwa ingawa wazazi walikuwa na shaka juu ya kijana huyo lakini waliogopa kumkwaza binti yao aliyeonekana mwenye furaha.......

Mashaka ya wazazi yalikuwa sahihi kwani yule kijana miezi michache ya ndoa alianza kuonyesha makucha yake.......

Tulianza kupokea kesi mfululizo zilizokuwa zinahusiana na mambo ya usaliti wa wazi kutoka kwa dada lakini kila tunalomshauri halisikii kwa maana penzi ni zito kuliko akili.......

Walikokotana mpaka wakafanikiwa kupata mtoto mmoja na ndio mambo yakazidi kuwa magumu........lakini dada kwa uzito wa penzi alichagua kuvumilia.......

Hata pale ambapo akili ilimuambia kuwa upo kwenye hatari lakini yeye aliamua kuvumilia.......

Kufupisha mambo
Yule mdogo wangu shujaa wa PENZI ni muathirika wa VVU na yule mumewe tulishamzika.........

Anaishi kwenye majuto baada ya kuutaka ushujaa wa kulipigania PENZI.........

NB
Weka ukomo wa uvumilivu wa mambo kwenye maisha yako......
 
Ni hatari sana kuacha akili nyuma na kuweka hisia mbele hasa kwenye nyakati hizi ambapo mioyo ya watu imeharibika
Umetisha, wanasema watoto wa mjini. Ukishaona ndoa ina vi-mgogoro vidogo vidogo vya kila siku, tena endelevu, kimbia kabla hayajakukuta. Ndoa karibu zote zinazokuwa na mwisho mbaya, wa mmoja kudhurika na hata kufa, huwa zinaanza na chokochoko ndogo za kila siku lakini zinapuuzwa.
 
Back
Top Bottom