Kulinda rasilimali kwa Export Ban on Concentrate: Kama tuliuzuia ili tusiibiwe kwa kutokujua kilichomo, tunawezaje kuruhusu bila kujua kilichomo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa ya kujadili maendeleo yetu na nchi yetu, kupitia makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye maswali fikirishi kuhusu mustakabali wa taifa letu Tanzania, leo nimepata fursa na naulizia kuhusu lifting export ban on copper concentrate, kuruhusu mchanga wa makinikia kuendelea kusafirishwa nje ya nchi kwenda kuchenjuliwa kwenye nchi za wenzetu wenye vichenjulio, je tume-lift this ban?

Tangu kusainiwa kwa mkataba kati ya serikali yetu na Barrick, mpaka sasa bado sijabahatika kujua the contents za kilicho sainiwa, lakini based on the draft iliyowahi kuletwa humu, draft ile ilionyesha mkataba ukiisha sainiwa, Tanzania tuta lift the export ban na mchanga utaruhusiwa kuondoka, "lifting the export ban on copper concentrate".

Leo from nowhere, usingizi umekata usiku mkubwa, something just tells me, mchanga unaondoka. Hicho kinachoniambia mchanga unaondoka, ni just some voices from within, hivyo hizi voices from within sio vitu vya kuviaminia sana, kwasababu unaisikia tuu sauti tuu bila uthibibisho wowote na haikumbii sababu, wala haikupi uhakika wowote wa hicho unachoambiwa.

Hivyo ukitokea ukaisikia sauti inakuambia chochote, the best way ni kuuliza na ku confirm hicho sauti ilichokueleza, na hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili.

Rais Magufuli alipopiga marufuku kusafirisha mchanga wa dhahabu, tulimpongeza kwa hatua hiyo.

Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Kwavile siku tunayazuia makontena yale ya mchanga wa makinikia, tuliyabaini kufuatia ziara ya kushukiza ya Mhe. Rais Magufuli bandarini Dar ndipo yakashitukiwa kutaka kutoroshwa, tukayazuia, na taifa sio tuu tukaambiwa bali tulionyeshwa, nashauri siku tukiyaruhusu pia tuambiwe na ikiwezekana tuonyeshwe, maana kuona ni kuamini.

Katika ziara ile ya kushtukiza, naomba kukiri mimi niliipinga ziara ile kuwa sio ziara ya kushtukiza kweli bali ni igizo la ziara ya kushtukiza.

Kupata maendeleo ya kweli, Tanzania inahitaji systems not dramas, Ze Comedy na one-man shows

Lakini ikitokea ni kweli mchanga umeruhusiwa, then Watanzania tuna haki ya kupatiwa taarifa rasmi.

Kwa vile mpaka ninapoandika hapa, bado hakuna taarifa yoyote rasmi kama the export ban imekuwa lifted na mchanga unaondoka, kuna hili swali la msingi sana Watanzania tunapaswa kuelezwa na kuelimishwa.

Katika vita ya kulinda rasilimali zetu zisiibiwe, kama tuliuzuia ule mchanga wa makinikia usisafirishwe nje ya nchi kufuatia kuibiwa kwa kutokujua kilichomo na kinachopatikana, hivyo tulifanya export ban on concentrate ili kuzuia kuibiwa kwa kutokujua kilichomo, je tunawezaje ku lift the export ban na kuruhu mchanga uendelee kusafirishwa nje, bila kujua kilichomo?

Jibu la swali hili litajibiwa baada ya ama serikali kutangaza wazi the lifting of export ban on copper concentrate or kwa media kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam kwa ruhusa ya Eng. Kakoko, na media kuonyeshwa yale makontena ya ule mchanga yaliyokuwa yamehifadhiwa hapa, mahali ambapo ni juani, (sasa hayapo), yamehifadhiwa mahali pengine kivulini, kufuatia yangeendelea kukaa pale juani ule mchanga ungeweza kuathirika kwa kupigwa jua, ukayeyuka na kuishia baharini, hivyo siku ya siku mwenye contena zake, akaja kushanga kukuta contena zake 277, zilizokuwa na mchanga wa makinikia zikiwa tupu kufuatia mchanga huo kuyeyuka na kutumbukia baharini.

Hitimisho
1. Je, zile containers 277 za mchanga wa makinikia zilizozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam bado zipo?

2. Je, export ban ya mchanga wa makinikia imekuwa lifted?

3. Kama tuliuzuia mchanga ili kuzuia kuibiwa kwa kutojua kilichomo, tunawezaje kuruhusu export bila kujua kilichomo?

Nawatakia Jumatano njema.

Paskali.
 
Comrade Mayalla

Wawekezaji hasa hawa MABEBERU ni wajanja sana...walichogundua ni nini Serikali inataka kusikia..nao wakaanza kupuga huo wimbo na Serikali ikaanza kucheza muziki wao.

So long wao ndio majority shareholder (84:16), sauti ya mwisho ya uendeshaji wa TWIGA ni ya BARRICK chini ya CEO waliyemleta kutoka Nchi ya MALI.

Gharama za uendeshaji hasa vitu kutoka Nje huwa wana inflate Sana na hivyo faida inakuwa very minimal kumbe wanakula kwa mlango wa nyuma.

16% yetu ilipaswa iwe kwenye mauzo ya Gold (TWIGA akipata 1kg ya Gold, tunagawana kwa 84:16 ratio) na sio kusubiri faida ambayo hutaipata au utapata kidogo mnooo.

Hii structure ya profit share, Tanzania tutaendelea kupigwa tu lazima tubadili terms....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swali la msingi sana.

Hata hivyo kwenye mkataba na Barick tumekubaliana kutowasumbua tena kwenye ishu ya makinikia. Tumewaachia wajichukulie tu, hatutawauliza huko duniani wamechenjua madini gani ya ziada ukiachilia mbali dhahabu na pia hatutawauliza wameyauza sh ngapi huko!

Sisi tumekubali kupokea chochote kitu tutakachopewa, hayo yaliyomo kwenye makinikia sasa tunajifanya kama hatuyaoni sasa

Ukurupukaji mtupu toka hapo awali
 
Prof. Mruma alikwisha onyesha kilichomo kitaalamu zaidi.
Kilichomo ni gramu 700 za dhahabu na silver katika container 1 la 20 feet hata Prof Mruma anajuwa hivyo kwa mujibu wa ripoti ya awali aliyopeleka kwa Jiwe. Of course kuna madini mengine madogo madogo yenye thamani duni. Ile ripoti iliyosomwa kwenye makabidhiano rasmi pale Ikulu huku Tundu Lissu akipigwa rısası ilikuwa 'doctored' purposefully na Jiwe mwenyewe.

Lengo la 'kui-doctor' ilikuwa ni kuthibitisha hisia zake za uwongo kuwa container lina lina kilo 7, kwa hiyo tulikuwa tunaibiwa kama kilo 6.3 kwa container kwa miaka 1998-2017. Na thamani ya kodi iliyokwepwa na ACACIA kuwa USD 190 Bilioni aka noah moja kwa kila mtanzania.

Ukweli umedihiri na uwongo umejitenga, Tundu Lissu alijeruhiwa kwa hisia tu.
 
mkuu Paskali, kipindi kile makinikia yanazuiwa na JPM, kuna mahali nilieleza thamani ya ule mchanga kwetu Watanzania kwa kutumia metaphor inayofanana na hii hapa chini:

mtu unajikuta upo katikati ya jangwa.
jangwa limezungukwa na mchanga tu.
upepo mkali sana unavuma 24/7.
akiba pekee ya chakula iliyopo ni viroba kadhaa vya mpunga.
huna maji.
huna nyenzo za kukobolea mpunga.
huna kuni wala mkaa.
so, huwezi kugeuza ule mpunga kuwa chakula kwako na wanao.
mara kinapita kifaru cha jeshi eneo hilo.
baada ya kuwaelezea njaa yako, wanakupa offer ya cartons kadhaa za mikate na maji ili wao wachukue walau kiroba 1 cha mpunga.
choice ni straightforward hapo.. unless huyo aliyekwama jangwani ni Mirembe case (of course)!

nimeeleweka I hope....
 
Ndugu Pascal, Tatizo tulilonalo ni kutokuwa na Honest, Nationalist strategist and long term Intelligent and realistic planners. Mullti purposeSmelter ingeweza kujengwa na nchi ingenufaika kwa njia nyingi sana.

1. Our Planners and Business planners, wangeweza kuwashauri viongozi, tupunguze ununuzi wa ndege mbili au tatu, na kununua Smelter Moja au mbili. Hizi smelting Plants zingeanza kufanya kazi immediately after commisioning, na wateja wa kwanza ni Tanzania yenyewe, Nchi jirani nyingi zingetumia kiwanda hicho.

2.Kiwanda kingetoa agira na uzoefu wa kazi kwa vijana.

3. Utoroshaji wa madini ungepungua san, Tungejua idadi na aina ya madini tunayo safirisha, Kodi nyingi ingepatikana.

4. Local Investors wangeweza kuwekeza kwenye madini.Masoko ya aina za madini zingefumuka hapa nchini.

Kwa hao walioshauri tununue Ndege badala ya Smelter au Viwanda vya kusindika mazao kama matunda, sijui wako wapi au wan sura gani. Jana economist wametangaza kuwa Mashirika ya ndege yatapata hasara ya zaidi ya US$30 Billions ( Coronavirus Outbreak Will Cost Airline Industry Nearly $30 Billion), hebu imagine tungekuwa na smelter tungekuwa wapi, au makontena 300 yangesafirishwa kwenda njee.
 
Ujinga ni mzigo mzito na majanga.

Si tumefungua kampuni mpya "Twiga" ambayo ndiyo mbia wa kusafirisha hayo makinikia Kwa sasa. Nini kisichoeleweka hapo?

Namshangaa aliyedhami kuwa tutaondoka videdea Kwa ushindi wa 100%.

Unafikiri watu watoe mitaji yao nje waje kuwekeza hapa kwa rasilmali ya teknolojia, uzoefu na fedha taslim halafu wawaachie iwe sadaka?

Kama ulifikiri hivyo basi elewa kuwa hayo ni mawazo mfu.

"Rule" ni "simple"; "You are either with us or you're against us".

Maana yake, ukikataa kwa hiyari kuwachia tunachokitaka, tunachukuwa kwa nguvu na hauna cha kufanya.
 
Pascal Mayalla,
Ndugu pascal kabla ya kuendelea na mada hii ningekuomba kwa kuwa wewe ni.mwandishi ungetupa taarifa ya haya makontena wakati wa mwanzo yalikuwa na thamani ya shilingi ngapi ambazo watendaji na ACACIA walithaminisha, lipoti ya pili ya kina muruma ilitoa thamani ya shilingi ngapi?

na bariki wao niliona mwisho wametoa kama bilioni 280, je tumeliwa au tumepata? ndo tujadili export burn, nadhani ingependeza zaidi, naombaututafute hizo ripoti uweke humu ili tupate mawazo mazuri.
 
msambaa1, Nadharia yako ni nzuri sana lakini kiuhalisia hutafanikiwa kama unavyofikiria.

Serikali ya Indonesia walijenga concentrate smelter kwa $700m. Imefungwa na haikuwahi kutengeneza faida yoyote. Concentrates zimerudi kusafirishwa nje.

Kwanza hii smelter siyo kama zile smelter za single mineral commodity. Hii ni smelter aghali. Lakini ujue kuwa anayesafirisha concentrates siyo Barrick bali ni mnunuzi. Concentrates zinajulikana zina kiasi gani cha madini yenye thamani ya kibiashara. Mnunuzi analipa kisha anaamua yeye akachenjulie wapi. Mnunuzi hawezi kupeleka tu kwa mchenjuaji yeyote bali kwa yule ambaye anamwamini na ana mkataba naye. Utajenga plant yako Tanzania lakini concentrates toka Zambia na DRC zitaendelea kwenda Japan.

Pamoja na teknolojia waliyo nayo US na Canada, bado wanapeleka concentrates Japan.

Kuamini kuwa tunaibiwa kupitia concentrates ni ujinga na mawazo ya kimaskini kutoka kwa watu waliotopea kwenye ujinga wa taaluma.

Concentrates zinapimwa na certified laboratories zilizosajiliwa na taasisi za kimataifa na masoko ya hisa Duniani. Reports zao ni legal documents ambapo kama wamedanganya, upande wowote ule yaani Serikali, mnunuzi na muuzaji anaweza kuishtaki maabara, na hilo litakuwa janga kubwa kwa hiyo maabara maana itazuiwa kufanya kazi hiyo mahali popote Duniani, na kulipishwa gharama kubwa ya kifedha kuanzia mteja aliyeathirika mpaka na wanahisa waliouza au kununua hisia kwa kutegemea taarifa za maabara hiyo.

Maabara hizi zinafanya kazi hii Dunia nzima. Kule hakuna watu wapu.mbavu eti watoe report za uwongo, halafu waondolewe kwenye biashara Duniani nzima. Hizi maabara siyo zile za akina Mruma za pale Dodoma ambazo instrument inasoma 200g per ton, wanasema andika kilo 200 per ton.

Watanzania amkeni. Jielimishe msipende kulishwa ujinga nanyi mkauchukua ujinga mzobemzobe, kwa vile tu mmelishwa ujinga na watawala.

Kwa uhakika wa 100% hakuna chochote tulichokuwa tunaibiwa kupitia makinikia. Ujinga wa Watanzania wengi unawafanya watawala kuwalisha uwongo mwingi kwa kujua kuwa watanzania watameza taarifa wanazopewa kama zilivyo.

Taarifa zile za kijinga za akina Mruma, leo kwa aibu zimetupwa kwenye mashimo ya takataka kiasi cha kushindwa kuamini kuwa kazi ile eti ilifanywa na maprofesa! Report ile hata mwanafunzi wa Geology wa mwaka wa 2 angeweza kujua bila shaka kuwa ulikuwa ujinga mtupu. Maana viliandikwa vitu ambavyo havijawahi kuwepo tangu Ulimwengu uwepo.
 
Kupanga ni kuchagua
...ukishafanya Cost vs Benefits Analysis ya UHAKIKA, unachangia 16% ya Investment ambayo ni madini + mtaji.

Tunanua madege kwa CASH tunashindwa nini kutoa CASH kuchangia gharama za uwekezaji na uendeshaji??

Comparative Analysis kwenye Feasibility Study (How feasible the business) itakusaidia kuingia mkataba wa ubia wenye WIN WIN
Ukitaka hivyo itabidi uchangie gharama za uendeshaji kwa hiyo 16%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Sasa mkuu ushauri wako ni upi?
Je nini walifanya Japan ili smelter zao ziaminiwe? Je Tanzania tukifanya walichofanya Japan je tutaweza kupata wateja?
Siyo process ya siku moja. Kuwa na uwezo na kujenga uaminifu ni kazi ya miaka mingi.

Leo hii India inaaminika kwa matibabu Dunia nzima. Wanaaminika kwa ubora wa huduma kwa gharama nafuu. Wagonjwa wanatoka US wanakwenda kutibiwa India. Lakini Wahindi wamefika hapo baada ya kazi ya miaka mingi. Hawakulala na kuamka, na kuwa mahali walipo leo.

Minada ya Almasi inafanyika Paris wakati Ufaransa hawana Almasi. Ukitaka Almasi yako ipate soko zuri na iwe na thamani ya juu ni lazima ikatwe na Myahudi.

Kama ilivyo kwenye specialization kwenye fani mbalimbali, baadhi ya mataifa yameamua kuwa specialized kwa utaalam fulani. Wamewekeza kwenye maeneo hayo heavily kifedha, kiteknolojia na kitafiti. Wewe huwezi kulala na kuamka ukategemea utakuwa kama wao, ni process. Sisi tunadhani unaweza kulala na kuamka halafu ukawa kama Japan au kama US kwa sababu tu umeamua uwe kama wao.

Halafu pia, kama Taifa ni vema kuamua unataka uitawale Dunia katika nini? Kwenye eneo hilo ndiyo uwekeze heavily kifedha, kiteknolojia na kiutafiti. Huwezi kuwa mahiri kwa kutaka uwe maarufu kwa kila kitu.

Kuna mataifa kama Netherlands, kutokana na mazingira yao wameamua kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye usafiri wa anga.

Kuna mataifa kama Switzerland wameamua kuwekeza zaidi kwenye sekta ya fedha.

Kuna mataifa kama Japan wameamua kuwekeza zaidi kwenye magari.

Kuna nchi kama US wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye masuala sayansi ya anga na majini. Dunia nzima ukitaka mitambo ya kuchimbia mafuta au gas kwenye bahari ya kina kirefu, huna chaguo jingine zaidi ya US. Na hakuna wa kushindana naye.

Kuna mataifa kama Norway yamewekeza sana kwenye utaalam wa uchimbaji mafuta na gas kwenye deep sea.

Mataifa kama Australia yamewekeza sana katika elimu ya madini. Hakuna mgodi mkubwa Duniani, ukawakosa Waaustralia. Mashine bora za uchorongaji kwaajili ya itafiti wa madini, lazima ukanunue Australia.

Kuna mataifa kama Ujerumani yamewekeza sana kwenye teknolojia ya reli na treni. Na kwenye hiyo teknolojia, wanatamba. Wanajenga miradi mikubwa na kuuza teknolojia. Waliuza teknolojia ya ujenzi wa SGR kwa mchina kwa package ya $30 bilioni, wakati wao tayari wakiwa na teknolojia ya juu zaidi.

Sisi Tanzania, tunarukia rukia tu mambo yote. Huwezi kuwa mahiri kwa kila kitu. Mathalani, sioni kama ni muhimu kwetu kuwa maarufu kwenye usafiri wa anga wakati kuna maeneo ambayo tungeweza kufanya vizuri zaidi. Uchumi ni mashindano. Ukitaka kushinda, compete using your strenghts not your weaknesses.

Tungeweza kufanikiwa zaidi, kwa mfano kwa kuwekeza heavily kwenye utalii. Tungeweza kuboresha vivutio asilia vya utalii na tukaongezea vivutio vya utalii vya kutengenezwa ambavyo vingeongezea umaarufu wa vivutio asilia.

Tanzania pamoja na vivutio vyote asilia, mapato ya jumla ya utalii wote, ni kama $3 bilioni kwa mwaka. Mji wa Paris pekee yake ni kama $90 bilioni kwa mwaka! Halafu bado maneno mengi mdomoni eti tunaongoza kwa vivutio.

Compare $3 billion vs $90 billion.
 
Kupanga ni kuchagua
...ukishafanya Cost vs Benefits Analysis ya UHAKIKA, unachangia 16% ya Investment ambayo ni madini + mtaji.

Tunanua madege kwa CASH tunashindwa nini kutoa CASH kuchangia gharama za uwekezaji na uendeshaji??

Comparative Analysis kwenye Feasibility Study (How feasible the business) itakusaidia kuingia mkataba wa ubia wenye WIN WIN

Sent using Jamii Forums mobile app
Unachosema ni sahihi. Ndivyo walivyofanya Botswana. Lakini serikali yetu inapenda zaidi kuwekeza kwenye maeneo yanayojenga prestige popularity na siyo kwenye maeneo yenye faida kubwa za kiuchumi ambayo hayawezi kuleta simple popularity kwa wapiga kura.
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa ya kujadili maendeleo yetu na nchi yetu, kupitia makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye maswali fikirishi kuhusu mustakabali wa taifa letu Tanzania, leo nimepata fursa na naulizia kuhusu lifting export ban on copper concentrate, kuruhusu mchanga wa makinikia kuendelea kusafirishwa nje ya nchi kwenda kuchenjuliwa kwenye nchi za wenzetu wenye vichenjulio, je tume-lift this ban?

Tangu kusainiwa kwa mkataba kati ya serikali yetu na Barrick, mpaka sasa bado sijabahatika kujua the contents za kilicho sainiwa, lakini based on the draft iliyowahi kuletwa humu, draft ile ilionyesha mkataba ukiisha sainiwa, Tanzania tuta lift the export ban na mchanga utaruhusiwa kuondoka, "lifting the export ban on copper concentrate".

Leo from nowhere, usingizi umekata usiku mkubwa, something just tells me, mchanga unaondoka. Hicho kinachoniambia mchanga unaondoka, ni just some voices from within, hivyo hizi voices from within sio vitu vya kuviaminia sana, kwasababu unaisikia tuu sauti tuu bila uthibibisho wowote na haikumbii sababu, wala haikupi uhakika wowote wa hicho unachoambiwa.

Hivyo ukitokea ukaisikia sauti inakuambia chochote, the best way ni kuuliza na ku confirm hicho sauti ilichokueleza, na hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili.

Rais Magufuli alipopiga marufuku kusafirisha mchanga wa dhahabu, tulimpongeza kwa hatua hiyo.

Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Kwavile siku tunayazuia makontena yale ya mchanga wa makinikia, tuliyabaini kufuatia ziara ya kushukiza ya Mhe. Rais Magufuli bandarini Dar ndipo yakashitukiwa kutaka kutoroshwa, tukayazuia, na taifa sio tuu tukaambiwa bali tulionyeshwa, nashauri siku tukiyaruhusu pia tuambiwe na ikiwezekana tuonyeshwe, maana kuona ni kuamini.

Katika ziara ile ya kushtukiza, naomba kukiri mimi niliipinga ziara ile kuwa sio ziara ya kushtukiza kweli bali ni igizo la ziara ya kushtukiza.

Kupata maendeleo ya kweli, Tanzania inahitaji systems not dramas, Ze Comedy na one-man shows

Lakini ikitokea ni kweli mchanga umeruhusiwa, then Watanzania tuna haki ya kupatiwa taarifa rasmi.

Kwa vile mpaka ninapoandika hapa, bado hakuna taarifa yoyote rasmi kama the export ban imekuwa lifted na mchanga unaondoka, kuna hili swali la msingi sana Watanzania tunapaswa kuelezwa na kuelimishwa.

Katika vita ya kulinda rasilimali zetu zisiibiwe, kama tuliuzuia ule mchanga wa makinikia usisafirishwe nje ya nchi kufuatia kuibiwa kwa kutokujua kilichomo na kinachopatikana, hivyo tulifanya export ban on concentrate ili kuzuia kuibiwa kwa kutokujua kilichomo, je tunawezaje ku lift the export ban na kuruhu mchanga uendelee kusafirishwa nje, bila kujua kilichomo?

Jibu la swali hili litajibiwa baada ya ama serikali kutangaza wazi the lifting of export ban on copper concentrate or kwa media kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam kwa ruhusa ya Eng. Kakoko, na media kuonyeshwa yale makontena ya ule mchanga yaliyokuwa yamehifadhiwa hapa, mahali ambapo ni juani, (sasa hayapo), yamehifadhiwa mahali pengine kivulini, kufuatia yangeendelea kukaa pale juani ule mchanga ungeweza kuathirika kwa kupigwa jua, ukayeyuka na kuishia baharini, hivyo siku ya siku mwenye contena zake, akaja kushanga kukuta contena zake 277, zilizokuwa na mchanga wa makinikia zikiwa tupu kufuatia mchanga huo kuyeyuka na kutumbukia baharini.

Hitimisho
1. Je, zile containers 277 za mchanga wa makinikia zilizozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam bado zipo?

2. Je, export ban ya mchanga wa makinikia imekuwa lifted?

3. Kama tuliuzuia mchanga ili kuzuia kuibiwa kwa kutojua kilichomo, tunawezaje kuruhusu export bila kujua kilichomo?

Nawatakia Jumatano njema.

Paskali.
Pascal Mayalla yaani unataka kutudanganya kuwa wakati wa kusaini ile mikataba ya uanzishwaji wa kampuni ya pamoja hukufuatilia hotuba za siku ile? Mh Raisi hakuagiza yale makontena yatafutiwe wateja? punguza kuchokonoa mambo yaliyokwisha kupita
 
Back
Top Bottom