Waafrika ndivyo tulivyo. Nilishangaa sana siku moja enzi za Kikwete nilipopita karibu na Ikulu na kuona jinsi uwanjwa wa ikulu ulivyo mchafu, vichaka, vimigomba vilivyo lundikana na vipara vya vumbi, hakuna ukoka sehemu nyingi ni vumbi. Niligundua kuwa nyumbani kwangu pazuri zaidi ya ikulu.Wakuu ukipita pale Ikulu ule ukuta wa fensi umezibwa na mabati kila mahali, kiasi kwamba huwezi ona chochote mle ndani!
Hivi nani aliwapa wazo la kuziba na yale mabati ambayo mwisho wa siku ni uchafu tu, kama hawataki eneo la ndani lionekane si bora wangepandisha ukuta.
Ile mibati inachefua sana, alafu ndo ofisi kuu ya serikali na taswira ya nchi.. Je wanajenga picha gani katika ofisi za kawaida na makazi ya watu huku mtaani?
Sent using Jamii Forums mobile app