Kulikoni picha ya Raisi JMT?

Kulikoni picha ya Raisi JMT?

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Hadi sasa Picha ya Raisi inayotumika kwenye ofisi zote ni ya Jakaya Kikwete, zikimtambulisha kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kwa maoni yangu hili si jambo jema hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa tunae raisi mpya zaidi mwezi mmoja umepita.

Hatuweki precedence nzuri.

Isitoshe picha ya raisi huwa inauzwa tena kwa lazima (mwenye ofisi huwezi kwepa), hata kama fedha za kuichapisha hakuna serikali itoe tenda.

Wahusika walione hilo.
 
Raisi aliyeshinda kwa dhuluma huyo ndo maana unaona kimya .mimi ofisini kwangu nimeweka picha ya Edward Lowasa.

wewe unaweka picha ya mafisadi.....ngoja tukushukie
 
Raisi aliyeshinda kwa dhuluma huyo ndo maana unaona kimya .mimi ofisini kwangu nimeweka picha ya Edward Lowasa.
Mnatumia nguvu nyingi kumtetea Ngoyai, poleni sana! Raisi wa mioyo yenu...
 
Raisi aliyeshinda kwa dhuluma huyo ndo maana unaona kimya .mimi ofisini kwangu nimeweka picha ya Edward Lowasa.

Kumbe mabadiliko yenyewe ni ya picha ! ......... haya zungusha mikonoo !
 
Mbona ilishatolewa ?
Wewe unaishi Wapi?
Baadae walisimamisha matumizi yake.mkulu alitokea kachoka sana shauri ya mikiki ya kampeni.sasa ameiva kwa mihogo ya ikulu picha rasmi itatoka wakati wowote
 
Raisi aliyeshinda kwa dhuluma huyo ndo maana unaona kimya .mimi ofisini kwangu nimeweka picha ya Edward Lowasa.

Umesikika kwani iwapo ofisi yako ni ya shughuli za binafsi basi hulazimiki kuweka picha ya rais labda kwa uzalendo wako tu. Hata hivyo mahakama na ofisi zote za serikali zinatakiwa kuwa na picha ya rais pamoja na bendera ya jamhuri ya muungano. Nadhani swali la msingi linahusu hizo ofisi za umma, siyo ofisi yako binafsi.
 
Back
Top Bottom