Kulikoni mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga kuhamishwa mapema hivi?

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
WanaJF naomba kufahamishwa kidogo kama kuna mtu anafahamu; hivi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyeteuliwa hivi karibuni anaitwa nani?

 
WanaJF naomba kufahamishwa kidogo kama kuna mtu anafahamu; hivi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyeteuliwa hivi karibuni anaitwa nani?

Anaitwa Ludovick Mwananzila. Alikuwa Mbunge wa Kalambo (Mkoa wa Rukwa) kabla ya kuangushwa kwenye kura za maoni uchaguzi uliopita. Aliwahi pia kuwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi kwenye baraza la kwanza la Mkwer'e.

Swali jingine?!!
 
Wakuu, habari zimeenea huko shinyanga kuwa mkuu wa mkoa mteule wa mkoa wa Shy bw. L. Mwananzila amehamishwa leo kwenda mkoa wa Lindi na mkuu mpya wa mkoa ameripoti leo mchana. Habari za kuamika kutoka kwa mtu aliyepo Shinyanga katika viwanja vya Shycom ambako maadhimisho ya miaka 50 yanafanyika kimkoa amesema ameona makundi ya watu wakiwa wanajadili juu ya uhamisho huo wa ghafla.

Wengi wakihusisha uhamisho huo na kauli yake aliyoitoa akiwa bungeni ya kuwatimua wasukuma kutoka jimboni mwake huko Rukwa.

Nawasilisha
 
Mungu wangu wote mmekosa jawabu sahihi!!!! Mnatakiwa muwe mna google kila baada ya dakika kumi!! Mambo katika nchi hii hayatabiriki!!
 
Reactions: Ame
Ludovick Mwananzila.NEXT TIME Ugoogle tu.huna haja ya kuuliza JF,swali kama hili

Nikiwa miongoni mwa great thinkers najua siwezi kuuliza swali kwa kukurupuka!!! Google wewe sasa hivi upate jibu sahihi!
 
Anaitwa Ludovick Mwananzila. Alikuwa Mbunge wa Kalambo (Mkoa wa Rukwa) kabla ya kuangushwa kwenye kura za maoni uchaguzi uliopita. Aliwahi pia kuwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi kwenye baraza la kwanza la Mkwer'e.

Swali jingine?!!

du. Wewe uko nchi gani. Mwananzila ni mkuu wa mkoa wa lindi
 
du. Wewe uko nchi gani. Mwananzila ni mkuu wa mkoa wa lindi

Afadhali Polisi!! Watu hawako nchini wanajibu maswali ya mitego bila kufikiri kwanza!! Sina hakika kama Mwananzila amewahi kuikanyaga Shinyanga kama Mkuu wa Mkoa!! Na aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi amefika tu hata kabla hajakabidhiwa ofisi akahamishwa kwenda Shinyanga!! Sijui hata kama vyombo vya habari vinalijua hili!
 
Reactions: Ame
kumbe ni kitendawili?

ngoja nipite kwanza.

Unaambiwa siku nyingine uwe una google!! Watu wanaamini kila kitu kinapatikana kwenye google!! Hii ni Tanzania, leo unasimamishwa kazi kesho unarudishwa kwa mamlaka aliyopewa anayekuridisha lakini kabla hujakaa sawasawa inakuja mamlaka nyingine inakurudisha likizo!!
 

Mkuu alikuwa amesharipoti na ziara za kula kuku alishazianza. Leo ilikuwa azindue maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru
 

mimi nilijaribu ku-google nikaletwa hapa:

Ikulu Mawasiliano

labda utupatie keyword.
 
Kama amepelekwa kuwaongoza wasukuma alioahidi kuwatimua kalambo, bila shaka azma yake itakuwa imesita kwakuwa sasa atafanya kazi ya kuwazuia kwenda huko badala ya kuwatimua!

Tehe tehe teheee...................... kweli Tanzania viroja havitakaa viishe, kahamishwa kimya kimya!?
 
Duh! Bongo hakuishi vituko kwa kweli! Hao waliofanya vetting kabla ya uteuzi hawakuliona hilo la kauli ya kibaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…