Serikali mnasubiria nini kupandisha hadhi Mji wa Ifakara kuwa Manispaa na Makao Makuu ya Mkoa Mpya wa Kilombero?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,727
Moja ya Miji inayokua kwa Kasi ya 5G Kwa Sasa hapa Tanzania basi ni Mji wa Ifakara.

Kwa miaka ya hivi karibuni umeibuka kuwa center kubwa ya biashara Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Ifakara ni Mji wa 12 Kwa Ukubwa hapa Tanzania Ukiwa na wakaazi zaidi ya 290,000 (Karibia Laki tatu). Cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba inakuaje Mji wenye watu wengi kiasi hiki haujapandishwa hadhi na kuwa Manispaa?

Kana kwamba haitoshi,Kwa Ukubwa wa Mkoa wa Morogoro,jiografia,idadi ya watu na mazingira yake inafaa ugawanywe na kuzaa Mkoa Mpya wa Kilombero ambao Makao Makuu yake yatakuwa Ifakara.

Aidha Serikali ufanye hima kujenga Barabara za lami kutoka Ifakara-Liwale/Masasi
Ifakara - Njombe
Ifakara - Kilolo/Iringa
Ifakara - Songea

Mwisho inapobidi kugawa maeneo Ili kuongeza Ufanisi, Serikali isisite na kuleta visingizio.Tuna Mikoa 26 ni mda muafaka Sasa wa kuwa na Mikoa 30 ambapo Mikoa ambayo inatakiwa kugawanywa ni Morogoro,Ruvuma,Lindi na Tabora bila kusahau Mkoa wa Chato 🤣🤣.

- Kama mkoa wa Morogoro ukigawanywa napendekeza mkoa mpya uitwe Kilombero wenye Wilaya hizi...
 
Back
Top Bottom