Hawa JHPIEGO ni shirika la Kimarekani ambalo kimsingi halifai kuwepo Tanzania kulingana na maadili yetu. Hawa watu bila ya kumumunya maneno wanaunga mkono ushoga pamoja na ukahaba, sijui wana malengo gani!
Mathalani tar 06/04/2016, Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga waliitisha kikao cha dharura ili kuliruhusu Shirika lisilo la serikali liitwalo Rafiki SDO(chini ya JHPIEGO) kuendelea na shughuli za kutoa elimu ya UKIMWI kwa wanawake wanaojihusisha na biashara ya ngono pamoja na mashoga.
Hii ni hatua iliyochukuliwa baada ya kulisitishia shirika hilo kuendesha shughuli zake mwezi Machi kutokana na tabia yao ya kuhamasisha watu kuendelea na ushoga kwa kuwapa vilainishi(lubricants).
Hawa watu machoni huwa wanatoa maelezo mazuri sana ila katika utekelezaji ni tatizo. Eti wanadai watawakusanya mashoga na wadada wanaojiuza katika vikundi ili wawasaidie kiuchumi.. Hili ni changa la macho! Unapowaweka mashoga pamoja unategemea nini?? Tutegemee kuanzishwa kwa soko la video za ngono baada ya miaka kadhaa ikiwemo maandamano ya mashoga Tanzania wakidai eti haki zao za kutambuliwa kama watanzania wengine.