Kulikoni bunge haliko live?

Kulikoni bunge haliko live?

hizo ni fikra kama za mtoto! huko bungeni wanajadili mambo yanayotuhusu sisi na mustakabali wa taifa letu. au ndio wanataka kutuzulumu?
 
TBC1 ni makapi makapi ya maCCM wanaoidhalilisha taaluma ya habari, seem wapo kutumikia watawala dhalimu! Siku zinavyokwenda tutajionea mengi sana ya ajabu, TV nyingine zikiomba haki ndo hapo utakaposhangaa zengwe linaanza...nafikiri kuna haja aya kupata chombo huru cha habari kisichofungamana na upande wowote ama idadi sawa ya vyombo kutoka kila upande wa kada.
 
Hii ni historia kwa mara ya kwanza bunge kutoonyeshwa wakati linafunguliwa! Kweli lema ni nouma
 
Hapo ndo tunaona umuhimu wa kuwa na chadema tv wakuu...hili wazo limeishia wapi? Sidhani kama wakitaka wachangiaji wa hali na mali tutakosa...
 
Hivi hii TV bado ipo? Inapatikana kwa kisimbusi gani siku hizi?? Mi nilishaitupia kwenye recycle bin siku nyingi sana
 
Wanakula njama watuuze, nadhni mikataba itasainiwa leo, subirini tukirudishwa studio.
 
Ni kawaida kila mkutano wa bunge unapofunguliwa sisi tulioko nyumbani tunasubiria kwenye tv zetu kuangalia nini kinaendelea huko mjengoni dodoma, lakini leo hakuna hata tv moja inayoonyesha mkutano huo wa bunge. Je ni sababu gani zimefanya hata tbc ya serikali kuacha kuonyesha mkutano huo muhimu? Hata star tv haionyeshi! Hali hii siyo nzuri wanayotutendea serikali.

Hivi Waziri Mkuu ameshatoka Mtwara?,inawezekana bado Mawaziri wanatetea na BOSS[JK].!!
 
TBC wametoa sababu ya kijinga kabisa.... but kikubwa hapa ni ujio wa lema live hawataki kuuona ata star tv nayo imebuma.

But tutaona tu kwenye source nyingine makini.

Hivi hakuna hata radio inayorusha kwenye mtandao? Please assist
 
Hata kwenye redio hamna kitu! Kweli ccm imefeli!
 
Hivi tukiamua kwenda kunyang,anya station yetu na tukaiendesha wenyewe wananchi serikali itasema nini yaani Bi Mkora chuki binafsi na Lema ndio inamfanya anyime haki ya habari wananchi ,anadhani Bunge ni mali yake anaweza akaamua kitu chochote wakati wowote,tukija tukamtoa kwenye kiti chake hicho hivi atalaani hatua hiyo,bi mkora ajiangalie asifikiri nchi hii ni yake na anaweza kuamua na kutenda chochote na sisi tukabaki tunamwangaklia tuu oooh haya bwana
 
RAIS WA ARUSHA ANATISHA SANA kale kabibi kiroboto safari hii tusishangae kakijivua uspika.hakawezi tena kusimamia bunge
 
serikali dhaifu sana hii,inakimbia kivuli chake.
 
Bob Marley aliwahi kusema you can run from people but you cannot run from yourself! CCM haiwezi kujikimbia, haiweza kukimbia kuvuna ilichopanda! hata wakijificha namna gani matendo yao yatawafuata tu!
 
Híi ni ajabu kabisa kwa mtambo wetu wa walipa mpaka Bunge linaanza leo TBC wanatuambia mtambo mbovu , au ndo hujuma zile walizosema na kupendekeza Bunge lisiwe linarushwa live ndo zimeanza, hii wanaJf mkumbuke bunge lililopita wabunge wengi wa CCM walipendekeza hivyo
 
Back
Top Bottom