Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,243
- 44,524
Nimetatizwa siku moja na inabidi niulize; hivi mtu anaweza kula huku amelala? Maana nasikia wengine wanaweza kukurupuka usingizini wakapika na kula na kurudi kulala! Wengine hata kukumbuka kuwa walikula hawakumbuki ila wanajua wameshiba! Au wanaacha ushahidi mkubwa kwamba "chakula kilikuwepo". Je ni vizuri kula usingizini? au kusubiri mwenzio yuko usingizini halafu unakula na unajua kuwa hatokumbuka kuwa mlikuwa mle pamoja, wewe unajilia halafu huyo unaendelea kuuchapa usingizi!
hehehehehehehe!hivi mtu anaweza kula huku amelala? Maana nasikia wengine wanaweza kukurupuka usingizini wakapika na kula na kurudi kulala!
miye sijui bwana.. siku moja enzi za ujana wangu niliachiwa tu ushahidi kuwa chakula kishaliwa na vyombo vimeoshwa nilipouliza mbona sikukaribishwa sijibiwi mtu anasema alikuwa na njaa tu!
Mdada,unaweza pata usingizi ukiwa na njaa?Hakyanani kama kweli njaa imekolea usingizi utausikia kwenye bomba.Nakumbuka enzi zile nilikuwa nasoma chuo kimoja hapo katikati ya jiji la Dar mambo ya madisco ya vyuo tulirudi silver sands enzi zile saa nane na njaa zetu hatukupata usingizi,tukalazimika kwenda Ushirika disco theque enzi hizzo tulipopata kula tukarudi kulala, tehe tehe tehe tehe! siwezi rudia tena kweli ujana maji ya moto...cha msingi unaweza kula usingizini tena hata sahani mbili inategemea njaa yako,labda sijui vyombo utaosha?.........Hii kali hivi kweli mtu unaweza kula huku umelala? Mie siwezi kula huku nimelala, hata kama tuna njaa nafuu tulale kwanza ili ukiamka utajisikia fresh zaidi kula chakula.
Huo usingizi unakuwa umerogwa au? Mbona ni hatari sana kama unaweza lala namna hiyo mpaka watu wanakula bila wewe kujitambua mh wanitia shaka mzee
Si ndo maana mi nkamwuliza kama anakuwa amemeza piriton? maana sasa huo usingizi unakuwa balaa. lol!
sijui wengine tukilala ndiyo inakuwa ile "fofofo"..