Kula mihogo mibichi kunasababisha uwe zezeta

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,240
12,764
Mihogo huwa ina sumu inayoitwa cyanide. Sumu hii hupatikana kwa wingi sana kwenye mihogo michungu. Lakini pia ipo kwa kiasi fulani kwenye mihogo ile mitamu. Sumu hii ni kali sana, ikizidi inaua mara moja. Ndiyo hata wqle majasusi unaona wnajiua kwa kutumia cyanide iwapo wamekamatwa na hawataki kutoa siri.

Kwa mtu anayetumia sumu hii kidogokidogo kwa miaka mingi, huwa inamletea matatizo ya akili. Anapoteza uwezo wa kufikiri vizuri na kumbukumbu. Jambo zuri ni kuwa kupika mihogo huwa kunaivunja sumu hii, hatari ya kupata uzezeta wanayo wale wanaokula mihogo mibichi.

Unaweza dhani unaongeza 'nguvu' za kiume(Sijui aliyeanzisha huu uzushi wa mihogo kuongeza 'nguvu' ni nani?) kumbe unajiletea uzezeta polepole.

====

Je, ni kweli mihogo mibichi inasababisha uzezeta?

Screenshot_20230226-180743_Chrome.jpg


Tembelea Jamii check kupata jibu sahihi: UZUSHI - Ulaji wa Mihogo mibichi husababisha Uzezeta
 
Mi nimekua kahama uko.. mihogo nimekula sana na sijawa zezeta... Mihogo mkomboz wa jamii nying sana... Hii tafiti ya pdf
Mihogo ni kweli ina sumu, na madhara yake hayaonekani hapo hapo, ni progressive yanawez chukua hata miaka kuonekana! Kukubwa usile miogo MIBICHI... Iliyopikwa iko safe
 
Mihogo inaongeza hamu ya kunyanduana mbichi sijui Kuna mechanism Gani ,ukila hiyo mtalimbo unaweza toboa bukta,nikiwa mbali na wife siku hizi sili
Mihogo ina kiwango kikubwa cha carbohydrates ambayo ndo inahusika na uzalishaji wa nguvu mwilini, ila kuhusu hamu si kweli.. labda Nguvu sawa
 
Mihogo huwa ina sumu inayoitwa cyanide. Sumu hii hupatikana kwa wingi sana kwenye mihogo michungu. Lakini pia ipo kwa kiasi fulani kwenye mihogo ile mitamu. Sumu hii ni kali sana, ikizidi inaua mara moja. Ndiyo hata wqle majasusi unaona wnajiua kwa kutumia cyanide iwapo wamekamatwa na hawataki kutoa siri.

Kwa mtu anayetumia sumu hii kidogokidogo kwa miaka mingi, huwa inamletea matatizo ya akili. Anapoteza uwezo wa kufikiri vizuri na kumbukumbu. Jambo zuri ni kuwa kupika mihogo huwa kunaivunja sumu hii, hatari ya kupata uzezeta wanayo wale wanaokula mihogo mibichi.

Unaweza dhani unaongza 'nguvu' za kiume(Sijui aliyeanzisha huu uzushi wa mihogo kuongeza 'nguvu' ni nani?) kumbe unajiletea uzezeta polepole.
Coca-Cola na Pepsi zaongeza nguvu za kiume wazungu wajanja sana kila kitu chao kinacho wanufaisha ni chema ila kila kitu cha mwafrica ni kiovu na kibaya
 
Coca-Cola na Pepsi zaongeza nguvy za kiume wazungu wajanza sana kila kitu chao kinacho wanufaisha ni chema ila kila kitu cha mwafrica ni kiovu na kibaya
Akili za kipumbavu sana hizi, madude ya viwandani yenye kemikali, rangi, sukari kali sana(KK), ladha bandia na maji hayana madhara lakini vitu asilia ambavyo vilipelekea Wazazi wetu watuzidi akili na afya kwa kuishi miaka miiingi zaidi ya 120 bila ya kuugua kansa, TB, pressure na kisukari ndiyo yana maana PUMBAVU
 
Hiyo ni mihogo ya pwani. Kanda ya ziwa wanatofautisha kati ya mihogo ya udaga na mihogo ya kuchemsha. Ingekuwa inasababisha tatizo basi Wasukuma na Waha wangekuwa mabubu.
Na Kanda ya ziwa ndiyo inaongoza idadi ya wasomi wengi kwa zaidi ya Maprofesa 600 TZ nzima, afu Taahira lililojikalia tu kwa Shemeji limejisikia kuja kupotosha Watu hapa jinga sana hili.

Haya ndiyo yale yale yanayokwambia mahindi ni chakula cha nguruwe ilihali kila jioni unalikuta stendi likiwa limekaza fuvu kutafuna mahindi ya kuchomwa
 
Uchagani hatuli mihogo wala kisamvu. Ukila miogo lazima ukate kamba. Hik ni kutokana ardhi hii ina sjmu nyingi kama sumu za lava za alvocano iliyolipuka hapo zamani na sumu za mashambani mfano zile za kuua wadudu shambani. Uchagani hata kisamvu kinaogopwa sana. .

Hili ni ukweli mihogo inahifadhi sumu na pengine wangefanya utafiti kuhusu maeneo mengine husika na aina za sumu ambazo mwanadamu anaweza zapata kutokana na kula miogo au baadhi ya mazao mengine. .

Angalizo: Pia natoa angalizo kwa serikali. Kuna tabia watu wanapiga dawa nafaka kuzihifadhi kwenye maghala ili yasiliwe na wadudu. Kuna mda maalumu dawa ile inatalkwa ipite ili yawe mazuri kiafya kwa mwanadamu. Cha ajabu unakuta mahindi yanauzwa huku yakiwa yamepuliziwa sumu hizi na mwisho yanasagwa na walaji wanapelekewa. Tunaharibu sana vizazi vyetu kwa sumu z ajabu. .

Hata samaki na kuku wa broila wanatakiwa wachunguzwe kwa umakini sana. .
 
Back
Top Bottom