Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Ni pale tu Polisi wanapotoa matamko kama kusema Mangula amekutwa na sumu mwilini na hivyo kuna mtu alitaka kumuua watamtafuta kwa udi na uvumba, ndipo unagundua tuna jeshi la polisi lisilo professional, linakurupuka na kufanya kila njia kutaka kujikomba kwa CCM na uongozi uliopo madarakani.
Sikatai kwamba Mangula anaweza kuwa amekutwa na sumu mwilini, lakini suala la Polisi kusema chanzo cha hiyo sumu ni mtu kutaka kumuua Mangula wamelipata wapi? Kwa nini Polisi wanatoa matamko makubwa kama haya bila kuwa wamefanya uchunguzi wa kutosha, wakijua kwamba matamko kama hayo yanaweza kuleta machafuko nchini, iwe migongano baina ya CCM na vyama vya upinzani au ndani ya CCM?
Je, ni kwamba Polisi wamekosa hata chembe ya professionalism kujua kwamba ni mapema mno kutamka kwamba sumu katika mwili wa Mangula chanzo chake ni mtu fulani kutaka kumuua? Na kulikuwa na umuhimu gani wa kutoa hilo tangazo? Inawezekana hata Mangula alikula mihogo mibichi kwa kuamini inaongeza nguvu fulani mwilini, na ikatokea mihogo aliyokula ilikuwa na sumu ya cyanide kwa kiwango kikubwa, au haikumenywa sawasawa. Sasa utasema aliyemuuzia hiyo mihogo mibichi alitaka kumuua? Mangula ametoka kwenye kesi za kina Membe, Kinana na Makamba halafu unakurupuka kutoa matamko kama haya, ni busara kweli?
Chukulia mfano mwingine, ile ajali ya egg chops za Royal Bakery ambayo ilisababisha vifo vya watu kadhaa hapa Dar es Salaam. Ni wazi vifo hivyo vilitokana na sumu katika egg chops na sumu hiyo ingekutwa mwilini mwa waliokula egg chops. Sasa kwa namna hii, hawa Polisi wangekimbilia kusema hao watu kuna mtu aliwawekea hiyo sumu ingekuwaje? Si aibu tupu?
Tunatoa wito Polisi kuacha kufanya kazi kama waganga wa kienyeji bali wawe professional. Kutoa habari za namna hii wakati upelelezi haujafanywa kikamili ni kulidhalilisha jeshi la Polisi na Tanzania kwa ujumla. Pamoja na kuwa watu wanaweza kuwa na sumu mwilini kwa kuwekewa na watu wasio na nia njema, kuna sababu nyingi nyingine zinaweza kusababisha sumu mwilini, kama kula mihogo mibichi au almonds, au mbegu za apples na matunda mengine zenye kiwango kikubwa cha sumu ya cyanide. Hata karanga zisizokaangwa unaweza kula zikawa na aflatoxin ambayo ni sumu katika mwili wa mwanadamu.