KUKWEPA KODI Ya PAYE

HIMO ONE

Senior Member
Sep 6, 2010
128
7
NAOMBA KUFAHAMU KAMA MFANYAKAZI AKIGUNDULIKA KUWA ANALIPA KODI KIDOGO KULINGANA NA MAPATO YAKE NI HTUA GANI ANAWEZA KUCHUKULIWA NA JE KODI INAYOTAKIWA KULIPWA INATAKIWA ITOKANE NA MAPATO YOTE AU NI MSHAHARA TUU??

ahsanteni
 
Kodi ya PAYE anayekulipa mshahara ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa anakokotoa kiwango sahihi cha kodi anayotakiwa kukukata kutoka kwenye mshahara wako na kuiwasilisha TRA. Ikigundulika kuwa umekuwa ukikatwa kodi ndogo kuliko inavyostahili (kwa bahati mbaya au kutojua), ni mwajiri ndiye atabanwa kuilipa pamoja na adhabu na riba. Ikigundulika kodi ilikuwa inalipwa kidogo kwa makusudi, hilo linakuwa ni kosa la jinai na lina adhabu zake (eg kufungwa etc).

Kimsingi, mwananchi wa tanzania anapaswa kulipa kodi ya mapato kwenye mapato yake yote (ya hapa Tz na kwengineko kote) yantokanayo na ajira, uwekezaji ama biashara.
 
Wabongo tunapenda sana miserereko. Tunafikiria kukwepa hadi PAYE!!!!!
Hii ni hatari
 
NAOMBA KUFAHAMU KAMA MFANYAKAZI AKIGUNDULIKA KUWA ANALIPA KODI KIDOGO KULINGANA NA MAPATO YAKE NI HTUA GANI ANAWEZA KUCHUKULIWA NA JE KODI INAYOTAKIWA KULIPWA INATAKIWA ITOKANE NA MAPATO YOTE AU NI MSHAHARA TUU??

ahsanteni

Kwanza kumbuka kuwa kulipa kodi ni 'price' ya kuishi katika nchi yoyote ile
Soma Income tax Act 2004 Section 7 (1 & 2)- Income from employment. Kwa kifupi ni gains zote i mean mshahara, posho zote na benefit zingine ambazo hupewi pesa moja kwa moja mfano usafiri, nyumba, kulipiwa ada ya wanafunzi n.k. Pia ukisoma sec.7 (3) utaona baadhi ya benefits ambazo hazitozwi kodi mfano matibabu n.k
Kuhusu adhabu soma part III ambayo inazungumzia non- compliance na kwa case yako specifically go to sect.104- offence of failure to comply with Act nanukuu 'where the failure results or, if undetected, may have resulted in an underpayment of tax in an amount exceeding sh. 500,000, to a fine of not less than sh. 100,000 and not more than sh. 500,000.

Hata hivyo sikushauri ufikirie kukwepa KODI iwe ni mtumishi au mwajiri. Kumbuka pia kuwa kodi ya PAYE anakusanya mwajiri, hivyo atakayebanwa ni mwajiri kwa kushindwa kukukata kutoka katika mshahara na marupurupu yako
 
NAOMBA KUFAHAMU KAMA MFANYAKAZI AKIGUNDULIKA KUWA ANALIPA KODI KIDOGO KULINGANA NA MAPATO YAKE NI HTUA GANI ANAWEZA KUCHUKULIWA NA JE KODI INAYOTAKIWA KULIPWA INATAKIWA ITOKANE NA MAPATO YOTE AU NI MSHAHARA TUU??

ahsanteni

Both employer and employee are liable for the liability meaning employer will extend the liability to the employee who was under deducted
 
Lakini hii PAYE mbona inakuwa kubwa sana kwa wafanyakazi walio katika sekta rasmi.
Kwani inumiza mno.
Ndio maana watu wanafikiri jinsi ya kuikwepa, japo ni muhimu kulipa kwa maendeleo ya nchi but ni kubwa sana kwa wafanyakazi
 
Je kwa wageni walioajiriwa hapa nchini au wanaojitolea ila wana kipatoo na wao wanalipa paye??na kama wanalipa kiasi kidogo kulingana na mapato yao sheria inasemaje??
 
Back
Top Bottom