kukumbukana wakati wa shida.

kukumbukana wakati wa shida.

Husninyo

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
24,167
Reaction score
10,226
mawasiliano yamerahisishwa sana siku hizi na kuna namna tofauti tofauti za kuwasiliana ingawa ni ukweli kuwa kuna watu unaweza maliza hata mwaka hujawasiliana nao hali ya kuwa una namba zao za simu au unaweza kuwapata kwa namna yoyote.

je inakuwaje pale mtu anapokutafuta wakati amekwama? yaani inakuwa ni tabia akikwama anakutafuta shida zake zikiisha humsikii tena mpaka akwame tena!

je tujifanye wajinga kwa kuwasaidia tu watu hivyo kama uwezo wa kufanya hivyo upo,? (kwamba tenda wema wende zako), tuwaonye tabia zao? tuwanyime msaada maana hawana uungwana? au tufanyaje wakuu?

cc Mbu, Eiyer, Lizzy gfsonwin The Boss Fixed Point AshaDii Kaizer Asprin Preta Mentor watu8 Heaven on Earth BAK king'asti Kongosho mwanajamii1 na wengineo.
 
Last edited by a moderator:
Mawasiliano kwa kawaida huwa mengi kwa watu ambao wako active socialy. Tunaingia kwenye era ambayo kuwa socially active kuna gharama sana hivyo wote tunajikuta kuwa inactive socially.
So kuna watu ambao naturally ni inactive socially na wengine wamefosiwa kuwa inactive socially na hivyo kupelekea asilimia kubwa miongoni mwetu kutokumbukana sana.

Tabia ya binadamu ni kuweka kumbukumbu ya watu wanaoweza kukupa msaada kulingana na aina ya shida uliyonayo. Kwa hivyo sasa aina ya mtu wa kukusaidia kwenye shida hii inapoangukia kwa aamtu ambaye hukuwa na mawasiliano active ndo haya majanga huanzia hapo!

Kiukwel mi nadhani unamsaidia tu mtu kwa sababu ana tatizo na wewe ndiye wa kumsaidia (Huu ndio ubinadamu). Factor zingine zinauma na kuathiri lakini hazitakiwi kuharibu maana hiyo.
 
mtu akiwa kazongwa na shida sometimes anakosa kujiamini

so akiwa anakuja tu kukusalmia,anaogopa kuonekana 'kaleta shida ingine'

so bora huyo ambae akikutafuta basi ana shida ya kweli.....
 
^^
Tuwasaidie kama tuna nafasi maana katika hao pia tumo na sisi tunazo namba ambazo ni kweli tunazitumia pale tu inapohitajika
^^
Mkuu kosa ni kosa tu
Halibadiliki kuwa sio kosa kwakuwa na sisi tunalifanya

Kama ni kupewa makavu live tupewe tu!
 
Nafikiri inapotokea hali kama hiyo unaweza kumfikiria huyo mwenzio na hali yake je ni kweli yuko bize kiasi hicho?au ye kutwa kushinda kwenye bao na bado hataki walau mawasiliano ya angalau mara moja kukujulia hali mpaka pale shida inapomkumba?,maanake kwa kweli kuna wenzetu wengine hata watoto zao wanawasahau sura maanake kuondoka bado hata jogoo hajawika na kurudi watoto washalala siku nyingi,na mwigine ye kazi yake kushinda kwenye vijiwe kunywa kahawa na kupiga soga na wenzie vijiweni kucheza bao asuuhi mapaka jioni 24/7,ukishajua hali halisi ya huyo mtu uamuzi unabakia wa kwako sasa eiza umsaidie au la.
 
Mkuu kosa ni kosa tu
Halibadiliki kuwa sio kosa kwakuwa na sisi tunalifanya

Kama ni kupewa makavu live tupewe tu!

^^
Kweli lakini pia kwa baadhi ya watu ukweli kwao si rafiki, na kwa wengine ukweli ni kichocheo cha kusonga mbele.
Ukiniambia ukweli mimi ntakuona wa maana na si mnafiki.
Katika misaada Tunasema kuwa usiwape samaki wafundishe kuvua.

Umesomeka!!!!!
 
^^
Tuwasaidie kama tuna nafasi maana katika hao pia tumo na sisi tunazo namba ambazo ni kweli tunazitumia pale tu inapohitajika
^^
ni kweli kuna namba hata tumeshasahau kama tunazo lakini ni vizuri kweli kutumia siku una shida tu?. yaani hujawasiliana na mtu kama miezi sita na siku unayopigia au kumtext unalia shida hapo hapo, ukishasaidiwa unapotea, siku unayoibuka unalia tena shida. kweli kipindi chote hicho unashindwa hata kutoa salamu mpaka shida nyingine ikukute!!
 
mtu akiwa kazongwa na shida sometimes anakosa kujiamini

so akiwa anakuja tu kukusalmia,anaogopa kuonekana 'kaleta shida ingine'

so bora huyo ambae akikutafuta basi ana shida ya kweli.....
we unajiskiaje mtu anakutafuta wakati wa shida tu?
 
Nafikiri inapotokea hali kama hiyo unaweza kumfikiria huyo mwenzio na hali yake je ni kweli yuko bize kiasi hicho?au ye kutwa kushinda kwenye bao na bado hataki walau mawasiliano ya angalau mara moja kukujulia hali mpaka pale shida inapomkumba?,maanake kwa kweli kuna wenzetu wengine hata watoto zao wanawasahau sura maanake kuondoka bado hata jogoo hajawika na kurudi watoto washalala siku nyingi,na mwigine ye kazi yake kushinda kwenye vijiwe kunywa kahawa na kupiga soga na wenzie vijiweni kucheza bao asuuhi mapaka jioni 24/7,ukishajua hali halisi ya huyo mtu uamuzi unabakia wa kwako sasa eiza umsaidie au la.

hiyo sasa ni kumpeleleza au! si utakuwa unapoteza muda kujua ratiba zake zipo vipi. lol
 
kusaidiana ni kuzuri ila hata mimi nawapigiaga watu kuna mda nikiwa na shida

shida ikiisha basi kila mtu ashike yake na mie akiwa na shida anitafute
 
swali ni kwamba mpaka mkaacha kuwasiliana wewe ulikua wapi tena msaidie tu maana we ni rafiki au ndugu ukimuhukumu anzia kwako maana hata wewe ulikua na uwezo wa kumtafuta.
 
Back
Top Bottom