Kuku wa ndimu MTAMU; utamu wazidi hamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuku wa ndimu MTAMU; utamu wazidi hamu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 3, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuku wa ndimu mtamu
  Kwa huyo ninayo hamu
  Sitaki kula kwa zamu
  Nile niishe utamu!

  Kuku wa ndimu mtamu
  Simhitaji mwalimu
  Nile bila kulaumu
  Nimle kuku wa ndimu!

  Kuku wa ndimu mtamu
  Kakaangwa kitaalamu
  Nikaivunja saumu
  Nilipozidiwa hamu.

  Kuku wa ndimu mtamu
  Jirani sinidhurumu
  Kwa vitunguu na ndimu
  Ya kuzidisha stimu!


  Kuku wa ndimu mtamu
  Utamu wenye wazimu
  Sijivungi nina hamu
  mwenye kupika adumu!!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hahaaahaha, MMM leo unanifanya nilale kwa raha kabisa.

  Nimependa sana beti la pili.

  Duuhhh!! Kweli haihitaji Mwalimu wa kufundisha kula mchuzi wa ndimu.


  Karibu sana MMU, world free of political effluence, misdemeanor and tensions
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tugee tusiojua tuonje nasi utamu
  Sio kutuelezea na kututia hamu
  Maana wenye tamaa utatutia wazimu
  Na tunavyokula vitageuka chachu ka ndimu!
   
 4. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka naomba nikuficharing kwenye singo yangu ijayo
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmmmhhhhhhhhh
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Akipakwa Ndimu
  Huwezi jilaumu
  Mtafune kwa hamu
  pia kwa mbinu
  Asitafunwe kwa zamu

  Ukionja huwezi laumu
  hasa maeneno muhimu
  kwa mtu muhimu
  Asiyejua hawezi fahamu
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  ndiyo nini sasa; umenogewa, huamini au ndio hamu imezid?
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  naguna ajili ya maneno mawili ya mwisho ahahhahah lol

  heri ya mwaka mpya...
  [​IMG]
   
 9. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmmhhh BAK usimwage hivyo bwana... mmmhhhh
  siwajua tena mwaka huu ni mdogo mdogo tu...
  [​IMG]
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tena awe wa singida
  wamtafuna pasi shda
  Ukitelemshia na soda
  Hasa yule wa kienyeji
   
 11. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  HERI KUNG'WAKA NPYAA......:bump:
   
 12. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuku unayemsema, ni kuku wa aina gani
  nataka nimwambie mama, amuweke kaangoni
  nile bila kulalama, utamu tele mezani
  Kuku unayemsema, ni kuku aina gani

  Je ni kuku wa kienyeji, au ni wale wa kizungu
  Nambie mwanakijiji, ubarikiwe na Mungu
  Ntamsaka mpaka jiji, nimle kwa jasho langu
  Kuku unayemsema, ni kuku aina gani

  Hamu imeshanizidi, siwezi kuendelea
  nimeshikwa na midadi, kuku namfikiria
  mimi nitajitahidi, nimpate bila hila
  kuku unayemsema, ni kuku aina gani
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,417
  Likes Received: 22,328
  Trophy Points: 280
  Jamani mwamaanisha kuku gani?
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuku unaemla kwa ugali!Hamna tafsida hapo!
   
 15. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bora uulize na mie namaliza post za wau... lakini sijamuelewa.... kwa ajili hapa jf wallah ukisema samaki ana maana yake,,, ukisema bata ana maana yake... sasa leo ni huyo kuku bado ninjia panda..
   
 16. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mkuu MKJJ,,usije ukawa umekosea jukwaa,,huyo kuku wa hii singo ni urais au??
   
 17. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 35
  utamu wa kuku nyama si rangi ya manyoya...kuku wa hapo kwenye red wengi tasteless
   
Loading...