Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Naamini kila mtu anajua kuchemsha kuku na kukaanga, ni pishi la kawaida sana.
Ingawa pishi hili ni rahisi, watu wengi wanalikosea sana,na matokeo ya pishi lao hayawi mazuri.Unaposoma pishi hili na unapopika kuna hatua tatu naomba uzingatie,kwani hatua
hizi hubadilisha sana matokeo ya pishi hili
Hakikisha umeelewa namna sahihi ya kufanya hatua hizi tatu kwani hatua hizi ndio hubeba ubora wa pishi hili.
Mahitaji
1.Unapokata kuku,ondoa ngozi yote
2. Katika Bakuli weka Nyama ya kuku ,swaumu,tangawizi,maji ya limao na chumvi, changanya vizuri,funika bakuli, weka frijini kwa saa moja.
3. Weka nyama na mchuzi wake wote kwenye sufuria,chemsha bila kuongeza maji, Nyama itatoa maji yanayotosha kuivisha. Chemsha kwa moto mdogo(simmer) na funika sufuria. Ikiwa tayari acha ipoe kabisa.
4. Katika kikaango weka mafuta,chemsha yapate moto wa wastani kisha weka nyama ya kuku na ukaange adi iwe na rangi ya brouni inayovutia, usiache ikakauka sana. Toa jikoni na weka juu ya sahani iliyotandikwa karatasi ili Nyama idondoshe mafuta. Nyama ya kuku tayari kwa kula.

- Namna ya kuweka viungo kwenye nyama
- Namna ya kuchemsha Nyama
- Namna ya kukaanga yama
Hakikisha umeelewa namna sahihi ya kufanya hatua hizi tatu kwani hatua hizi ndio hubeba ubora wa pishi hili.
Mahitaji
- Kuku kilo 1
- Swaumu vijiko 2i vya chai
- Tangawizi kijiko 1 cha chai(twanga au sugua iwe laini)
- Limao vijiko 3 vya chakula
- Chumvi kwa ladha upendayo
- Mafuta ya kukaangia vikombe 2 au zaidi.
1.Unapokata kuku,ondoa ngozi yote
2. Katika Bakuli weka Nyama ya kuku ,swaumu,tangawizi,maji ya limao na chumvi, changanya vizuri,funika bakuli, weka frijini kwa saa moja.
3. Weka nyama na mchuzi wake wote kwenye sufuria,chemsha bila kuongeza maji, Nyama itatoa maji yanayotosha kuivisha. Chemsha kwa moto mdogo(simmer) na funika sufuria. Ikiwa tayari acha ipoe kabisa.
4. Katika kikaango weka mafuta,chemsha yapate moto wa wastani kisha weka nyama ya kuku na ukaange adi iwe na rangi ya brouni inayovutia, usiache ikakauka sana. Toa jikoni na weka juu ya sahani iliyotandikwa karatasi ili Nyama idondoshe mafuta. Nyama ya kuku tayari kwa kula.
- Kaanga kwa mafuta mengi,ili unapoweka nyama izame kwenye mafuta(deep frying)
- Mafuta yasiwe ya moto sana.Kaanga kwa moto wa wastani ili Nyama iive vizuri na isiungue nje kabla haijaiva ndani.
- Ukikaanga kwa moto mkali,mafuta huruka sana na kunauwezekano mkubwa sana wa wewe kuungua na mafuta hayo yanayoruka.Katika kukwepa hili pia ni vyema kutumia kikaango kilichojichimba.
CHAKULA KIZURI HUONGEZA FURAHA KATIKA FAMILIA