Kuku wa kukaanga aliyelowekwa kwenye viungo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Naamini kila mtu anajua kuchemsha kuku na kukaanga, ni pishi la kawaida sana.
Ingawa pishi hili ni rahisi, watu wengi wanalikosea sana,na matokeo ya pishi lao hayawi mazuri.Unaposoma pishi hili na unapopika kuna hatua tatu naomba uzingatie,kwani hatua

hizi hubadilisha sana matokeo ya pishi hili


    1. Namna ya kuweka viungo kwenye nyama
  1. Namna ya kuchemsha Nyama
  2. Namna ya kukaanga yama

Hakikisha umeelewa namna sahihi ya kufanya hatua hizi tatu kwani hatua hizi ndio hubeba ubora wa pishi hili.

Mahitaji

  • Kuku kilo 1
  • Swaumu vijiko 2i vya chai
  • Tangawizi kijiko 1 cha chai(twanga au sugua iwe laini)
  • Limao vijiko 3 vya chakula
  • Chumvi kwa ladha upendayo
  • Mafuta ya kukaangia vikombe 2 au zaidi.

1.Unapokata kuku,ondoa ngozi yote

2. Katika Bakuli weka Nyama ya kuku ,swaumu,tangawizi,maji ya limao na chumvi, changanya vizuri,funika bakuli, weka frijini kwa saa moja.


3. Weka nyama na mchuzi wake wote kwenye sufuria,chemsha bila kuongeza maji, Nyama itatoa maji yanayotosha kuivisha. Chemsha kwa moto mdogo(simmer) na funika sufuria. Ikiwa tayari acha ipoe kabisa.


4. Katika kikaango weka mafuta,chemsha yapate moto wa wastani kisha weka nyama ya kuku na ukaange adi iwe na rangi ya brouni inayovutia, usiache ikakauka sana. Toa jikoni na weka juu ya sahani iliyotandikwa karatasi ili Nyama idondoshe mafuta. Nyama ya kuku tayari kwa kula.


  • Kaanga kwa mafuta mengi,ili unapoweka nyama izame kwenye mafuta(deep frying)
  • Mafuta yasiwe ya moto sana.Kaanga kwa moto wa wastani ili Nyama iive vizuri na isiungue nje kabla haijaiva ndani.
  • Ukikaanga kwa moto mkali,mafuta huruka sana na kunauwezekano mkubwa sana wa wewe kuungua na mafuta hayo yanayoruka.Katika kukwepa hili pia ni vyema kutumia kikaango kilichojichimba.
Utamu wa pishi hili huanzia kwenye viungo,na uchachu wa limao, kumbuka kwamba umuhim wa kuacha nyama ikae kwa saa moja baada kuiwekea viungo ni kuruhusu viungo viingie ndani ya nyama ili kuipa ladha nzuri na pia kuilainisha.
CHAKULA KIZURI HUONGEZA FURAHA KATIKA FAMILIA
 
Mzizi mkavu, mkuu hizo sentensi mbili za mwisho hapo juu, ndio bado utatraa kwangu. Naomba ufafanuzi wa kina lasivyo naondoa shilingi....!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom