Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,128
- 8,058
Nimeona mada nyingi hapa JF zina makosa ya tahajia (spelling) za maneno ya Kiswahili. Na watu hawaoni kuwa hilo ni tatizo. Matatizo wanayoona ni ya kisiasa! Hii ni dalili ya ulegevu wa kiakili, kutokujali na kukosa bidii ya kujifunza lugha.
Lugha ni zana ya hekima na ufanisi. Mtu anayeijua lugha yake vizuri anaeleweka kwa urahisi na hupewa heshima. Ukikosea tahajia mara kwa mara, hasa kwa maneno ya kawaida, unadhihirisha kuwa huna bidii ya kazi, hupendi kujitahidi. Na hii ni ishara kwamba hata ofisini kwako au kwenye biashara yako unafanya makosa na hujali.
“Je! Umemwona mtu aliye mstadi katika kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme, hatasimama mbele ya watu wa kawaida.” (Methali 22:29)
Andiko hilo linaonyesha kuwa ustadi, hata katika kuandika, huinua mtu. Kinyume chake, mtu mlegevu hata kufanya "proof-reading" hastahili cheo kikubwa.
"Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakoenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.”
Kama unaandika mada, andika kwa bidii. Zingatia tahajia sahihi.
Methali 18:9
"Mtu mvivu kazini mwake ni ndugu yake mharibifu.”
Kukosea tahajia sio jambo dogo; ni ulegevu unaoweza kuharibu mawasiliano na kuathiri picha yako mbele ya watu. Mmenipata, wakuu? Ni Injili tu kila kona! 😎