Moja ya dalili kwamba utafeli maisha ni kuchukia wanaokuzuia usifanye mambo Mabaya

Moja ya dalili kwamba utafeli maisha ni kuchukia wanaokuzuia usifanye mambo Mabaya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
38,009
Reaction score
87,989
MOJA YA DALILI KWAMBA UTAFELI MAISHA NI KUCHUKIA WANAOKUZUIA USIFANYE MAMBO MABAYA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Ishara za mwanzoni kabisa za mtu kufanikiwa maisha sio katika bidii yake, sio katika Uchapakazi wake, sio katika uhodari na ujasiri wake.

2. Ishara za mwanzoni ukitaka ujue MTU Fulani atafika mbali ni kuwasikiliza na kuwapenda wanaomfuatilia na kumzuia asifanye mabaya.

3. Unakuta mtu humjui hakujui.
Sio Mzazi wako, sio ndugu yako.
Huenda ni jirani tuu. Au mwalimu wako.

4. Sauti ya wasiokujua hasa inapokuzuia kufanya mabaya mara nyingi ni sauti ya MUNGU.

5. Iko hivi Mungu mara nyingi atakusaidia na kukuokoa na watu usiowajua au msio na mahusiano nao kabisa. Tena ikiwezekana watu wa chini wasio na mbele wala nyuma. Ili kama unakiburi usiwasikilize. Na kama umnyenyekevu uwasikilize na ubadili tabia.

6. Shetani mara nyingi hutumia watu wako wakaribu, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kukuharibu.
Katika kanuni za kitibeli tunazingatia Sana kanuni hizo. Watu wa mbali ndio watakaosema ukweli wote.

7. Binti/kijana ameenda Mbali na home, aidha upo chuo au unatafuta chapaa!
Ukiona kuna watu wazima wanakushauri na kukupa mawaidha Fulani.
Jua unabahati Sana.

8. Bahati ni Jambo moja kufanikiwa ni Jambo la pili.
Ukiona unaonywa na hao watu na ukajikuta unapenda kusikiiza maonyo na unawaelewa, my friend ujue upo kwenye laini. Utafanikiwa tuu upende usipende.

9. Lakini ukiona ukiambiwa alafu unaona kama unafuatiliwa, unaungiliwa, unafuatwa fuatwa na haupendi, unachukizwa na Hali hiyo. My friend hapo ujue umeanza kuchochora. Umeacha barabara mkuu.

10. Unaingiza mademu hakuna MTU mzima yeyote anayekufuatilia. My friend umekwisha.
Hakuna jamaa yeyote anayekushtua. Umekwisha. Jua upo kwenye station ya kuzimu, anguko lako liko karibu.

11. Unakunywa pombe hakuna anayejali. No one care about you. Aiseeh! Ondoka hilo eneo. Umeachwa.

12. Binti unatoka na waume za watu. Hakuna anayekuonya, unakaa uchi hakuna anayejali. Ujue umedharauliwa.
Huna kitu cha maana. Ni roho iliyopotea.

13. Inasemwa mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.

Hawakuoni wa thamani ndio maana hawana habari za wewe.
Hakuna anayeumizwa na wewe. Ufe usife utajua mwenyewe.
Utiwe mimba usitiwe shauri yako.
Uvunje ndoa usivunje utajijua.

14. Unapochukia kufuatwa fuatwa sio kwamba hutaki kuingiliwa. Ni kwamba Una kiburi. Na huwezi ukawa na kiburi ukafanikiwa.

15. Wewe sio Mamaangu, wewe sio Babaangu. Huwezi nielekeza Jambo.
Mtu yeyote anayetumiaga kauli hizi hanaga mwendo mrefu lazima apige mzinga.

Imeisha hiyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Yupo wapi Mzee tupatupa wa Lumumba (jokes)
Kuna bwana mmoja tulikutana ofsini Moja hapa mjini hapo mwaka Jana. Yule bwana alikuwa na pesa wakati .
Alikuwa anataka kuanzia kuchimba madini mkoa flani hivi. Hana abc kabisa za hiyo biashara
Mm nipo nayo siyo ya shule lakini nimekaa na wachimbaji na wauzaki muda kidogo
Akawa ana nituma kwenye site zake kuweka mambo sawa.
Namshauri, namshauri tujenge hiki tununue kile
Siku Moja nikiwa porini baada ya machafuko akanipigia simu kuniambia hataki kushauriwa na pesa zake
Sikuweza kuendelea nae kwakweli
 
Back
Top Bottom