Kukithiri kwa wizi mkubwa wa mabilioni na matrilioni nchini; Ipi nafasi ya TISS kuzuia matukio haya?

Hivi nikiwaita TISS ni vibaraka wa CCM nitakuwa nakosea?

Kwangu mimi TISS ni tawi la CCM, kama ambavyo tunayaona matawi ya CCM huku mitaani wameweka mawe yao ya msingi.

Nategemea siku za karibuni TISS nao pale nje ya ofisi yao waweke jiwe la msingi wafungue tawi la CCM, watuambie nani kafungua hilo tawi kama ni Bashite itapendeza zaidi, na tarehe ya ufunguzi wasisahau...

Sasa wewe mleta mada unajiuliza iweje hili tawi la CCM linashindwa kuudhibiti wizi wa matrilion unaotokea nchini, hivi umewahi kuona wapi mwizi akijikamata?!

Wizi unaofanywa na CCM ni kama chain, mara nyingi unahusisha wengi toka idara tofauti, ndio maana huwezi kukuta wanakamatana, kwasababu wanajua watamalizana, hayupo atakayebaki salama miongoni mwao.
 
Habari wanaJF.

Kwa wafuatiliaji wa mambo nchini,matukio ya wizi wa mabilioni ya pesa nchini sio jambo la ajabu.Tunasema ni wizi kwa sababu mazingira yenyewe yamejaa ukakasi na hata Serikali imeshindwa kutoa majibu yenye mashiko.

Kwa mfano EPA,IPTL,MEREMETA,NDEGE MBOVU YA RAIS,RADA MKWECHE,ESCROW n.k. Haya matukio mpaka leo 'yameishia hewani'.

Sasa nilitaka kupata elimu kwa wajuzi wa masuala ya kiusalama nafasi ya Idara nyeti ya TISS katika kuzuia matukio haya na pia nataka kujua ni kwa namna gani wizi wa namna hii si hatarishi kwa usalama wa Taifa.

Karibuni tuelimishane.
Kumbe kuzuia wizi nayo ni kazi yao?
Mimi nilikuwa nadhani ni watu wanaojulikana tu.
 
Back
Top Bottom