Kukamatwa kwa Mbowe, jaji mkuu Chande anahusika?


Hakika inashangaza kwa nini alihudhuria hiyo semina elekezi. Kishaingia katika mfumo wa kifisadi wa CCM, Mahakama inazidi kukosa uhuru wake kikatiba na hivyo haki kupotea.

Halafu huyo Chande hakustahili kupata wadhifa huo mkuu kwani kuna majaji wqengine wanne wa Mahakama ya Rufaa wamerukwa (katika order ya seniority). Kwa hali hii maamuzi yake yote yanayohusu serikali ya JK yatatiliwa shaka.
Nchi hii inazidi kupotea njia.


Mkuu aliingizwa kufanya kazi maalumu na sasa ameianza rasmi! God Bless Tanzania!!!!!!!!!!!!!
 
Najiuliza huyu Lipumba amekuwa mzuri leo kiasi cha kumuweka katika harakati zenu? Vipi ile ndowa uliyomfungisha kuwa ameolewa na Magamba?
 
Kwani tunaposema Serikali tunamaanisha nini hasa?,

Na je,ni vitu vipi hasa vinaunda Serikali?

Nadhani hapa unachanganya kati ya Government na Executive branch of the Government.Kwa kiswahili hivyo vyote vinaitwa SERIKALI.

Jaji Mkuu anatoka a judiciary branch of the government ambayo kwa kiswahili tunaita MAHAKAMA.Akina Makinda wapo legislative branch of government ambayo tunaita BUNGE.

Mgawanyo huo wa matawi hayo ya Government ni muhimu sana katika separation of powers.Na separation of powers ni muhimu sana katika kuhakikisha mgawanyo sawa wa mamlaka (authority) na kuzuia uwezekano wa executive branch kumeza hizo taasisi nyingine muhimu.

Naamini unaelewa kuwa bunge linatunga sheria,mahakama inatasfiri sheria na serikali kwa maana ya executive brancho of government inasimamia sheria kama zilivyotungwa na bunge na kutafsiriwa na mahakama.
 
Is the Chief Justice part of the executive branch?

Absolutely not. Lakini hata hao wanaotetea sidhani kama wanajua executive branch ni nini. Wao wanajua tu Serikali thats it. Ndio tatizo letu bongo ushabiki unapita kiasi, na wala hatujishughulishi kujielimisha.
 
No suprise kwani kama tunavyojua ndani ya ccm hakuna tofauti na heshima yeyote kati ya serikali, mahakama wala chombo cha bunge. Kuna wa makada wengi akiwemo mwinyi, kikwete na mkapa hawajajua jinsi gani constitution za dunia nzima zinajengwa kutofautisha hizi institutions za kitaifa kwa lengo la kuleta check and balance. Kama kada wa ccm anateuliwa kuwa jaji mkuu na mwingine mkuu wa polisi kwa sababu walienda chuo cha sheria na kupata A au kwasababu wameapa kwa kikwete watamlinda hata akifanya makosa au wanauhusiano. Tunategema nini kutokana na ideology ya ccm kujilinda na kujitengenezea sheria zao wenyewe humo humo ndani ya katiba yao? jaji mkuu wa Tanzania ameteuliwa kwa lengo moja tu, kumlinda kikwete kwanza na pili kuhakikisha hakuna mtu ataisumbua ccm na makosa yao. Mifano si tunaijua, hukumu za Radar, EPA, Richmond na Dowans. Leo hii we are expecting something new kutoka kwa jaji mkuu au mahakama au mkuu wa polisi au jeshi....We as Tanzanians must take control of our country there no one will come and hand us these changes. Ndio sababu kubwa za kuanza mapamabano ya kuondoa bunge na kuwatoa Mbowe na wanasiasa wengine leo na wiki hii nzima. The get Start Yeah ....
 
- Hili taifa hakuna wa kumsaidia mwignine wote hatujui kuihsi kwa kuheshimu sheria, Chadema kunahitajika marekebisho makubwa sana kabla hatujenda mbaali maana sasa hivi wananchi tutashituka kama vile enzi za Mrema!

William @ NYC, USA.
Ndugu yangu William,
Huu ujumbe wako ungemshauri the late Martin Luther King Jr. katika miaka ya sitini usingeeleweka kabisa. Huwezi kuheshimu sheria kandamizi, na lazima mmoja ajitolee kafara ili sheria kandamizi zijadiliwe na zibadilishwe. That is what happened in the US. Yule Mama Rosa Parks (rip) alichoka kukalishwa kiti cha nyuma cha basi kwa sheria kandamizi, akagoma. MLK alifungwa jela mara kadhaa kwa kukaidi sheria kandamizi. Wewe ungekuwepo wakati huo nina hakika ungesema shame Dr. Martin Luther King Jr, shame black Americans, for not following the laws. Inastaajabisha. Na kwa mantiki hiyo katika karne hii ujumbe wako huo haueleweki kabisa.
 
Nadhani hapa unachanganya kati ya Government na Executive branch of the Government.Kwa kiswahili hivyo vyote vinaitwa SERIKALI.

Jaji Mkuu anatoka a judiciary branch of the government ambayo kwa kiswahili tunaita MAHAKAMA.Akina Makinda wapo legislative branch of government ambayo tunaita BUNGE. Mgawanyo huo wa matawi hayo ya Government ni muhimu sana katika separation of powers.Na separation of powers ni muhimu sana katika kuhakikisha mgawanyo sawa wa mamlaka (authority) na kuzuia uwezekano wa executive branch kumeza hizo taasisi nyingine muhimu)

Well said mkuu, Hiyo mihimili mitatu inasaidia kwenye "check and balance" kama ulivyosema. Bunge likitunga sheria zinazoenda against katiba -mahakama itawakosoa, the same way serikali iki-abuse sheria zilizowekwa- bunge linatakiwa liikosoe/lihoji serikali. That being said; lazima kila muhimili uwe- independent. Rais hatakiwi kuingilia shughuli za mahakama/judicial system, and the same applies to the parliament. Otherwise hakutakua tena na usawa kwenye mzani.

.
 
in this, really hate the kiwete's governance. its such a stupidity phenomenon to have ccm,poliCES,kiwete. die you diiie hell is ur specific place. we are victims rejuice by the common bond GOD is good and he's love is so strong.....

viva freeman mbowe vivi chadema, viva free generation.
 
Hakuna mashaka kwamba kukamatwa kwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini kumetokana na maelekezo ya Jaji Mkuu, Othuman Chande ambaye ameigeuza mahakama kuwa idara ya siasa ya serikali.

Chande aliyehudhuria semina elekezi wiki iliyopita, nimeelezwa amechukua hatua hiyo ili kumnusuri mdogo wake, Othuman Rashid ambaye idara ya usalama wa taifa imemshinda kwa kuwa sasa imegawanyika mapande mawili - moja linaongozwa na yeye na jingine linaongozwa na Zoka.

Taarifa zinasema hatua ya Chande ya kushinikiza Mbowe akamatwe inakusudia kumsaidia Kikwete kupata nafuu ya kisiasa baada ya kutuhumiwa na wenzake kuvuruga chama. Gazeti mashuhuri la kila wiki nchini - MwanaHALISI lilijadili hatua ya Jaji Chande kuhudhuria semina elekezi katika toleo lake la wiki iliyopita na bila shaka yanayotokea leo, ni sehemu ya matunda ya semina hiyo.

Jaji mkuu ni sehemu ya serikali?

Na Isaack Kimweri​

SEMINA elekezi iliyoandaliwa kwa ajili ya watendaji serikalini wiki tatu zilizopita mjini Dodoma imeibua jambo zito.
Jambo hilo ni ushiriki wa mihimili mingine miwili ya dola Bunge na Mahakama katika semina hiyo ambayo ililenga mhimili wa tatu – watendaji wakuu serikalini.
Katika hali ya kawaida, mihimili hii haitakiwi kuingiliana katika utendaji wake wa kila siku.
Kwa bahati mbaya na kwa kweli kwa utashi wa kiitikadi, katiba ya Jamhuri imempa ruhusa rais kuteua wabunge kuwa mawaziri na hivyo kulifanya bunge kuwa sehemu ya serikali. Kelele nyingi zimepigwa juu ya kasoro hii na naamini kuwa katiba mpya itashughulikia kasoro hii ili mihimili hii itenganishwe.
Wengi tunaamini mahakama haipokei amri wala maelekezo kutoka serikali wala bunge. Ni matumaini ya wengi kuwa mihimili hii itaendelea kutenganishwa kwa ajili ya kuboresha utawala bora katika taifa letu.
Kilichoshangaza katika semina elekezi ile ni uwepo, siku ya ufunguzi, wa Jaji Mkuu Othman Chande. Baadaye nilidokezwa kuwa alikuwa mmoja wa watoa mada (mwezeshaji).
Uhusika wa Jaji mkuu katika semina elekezi ya viongozi wa serikali unatia shaka na kuna kila sababu ya kuhoji utaratibu huu mpya wa utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne.
Jamhuri yetu si ya muungano wa mihimili ya dola kiasi cha kumfanya Jaji Mkuu kuwa sehemu ya serikali. Ili kumwepusha na majaribu yanayoweza kutia dosari maamuzi yake na uendeshaji wa mhimili wa mahakama, Jaji mkuu anapaswa kuwa mbali na maelekezo ya serikali – asiyasikie wala kuhusika kama chombo cha kuyatoa kwa watendaji wa serikali.
Hii ni kwa sababu, baadhi ya watendaji wa serikali wanaweza kujikuta wakitenda kazi zao kwa kuongozwa na jinsi jaji mkuu alivyosema au kujikuta wanamtumia kama shahidi wao ili kuwatisha waathirika wa maamuzi yao.
Jaji mkuu, kama mwanadamu, ana utashi binafsi na vionjo vya kiitikadi. Unapomhusisha katika semina elekezi ya watendaji wa serikali, unachokoza vionjo vyake na matamshi yake kiitikadi yanayoweza kuamsha na kuingilia maamuzi yake ya baadaye anaporejea katika wajibu wake wa kazi zake.
Ikumbukwe kuwa serikali iliyo madarakani ina sera maalum na ilani yake ya uchaguzi ambayo ni tofauti na vyama vingine ambavyo havijazuiwa kuchukua madaraka ya nchi wakati jaji mkuu akiwa bado madarakani. Hali hiyo ikitokea, jaji mkuu huyo atapokea au kushiriki semina elekezi ngapi?
Jaji mkuu ni kiongozi mkuu wa mhimili wa mahakama lakini si kiranja mkuu mwenye wajibu wa kuhakikisha majaji na mahakimu wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata maelekezo yake katika jukumu la utoaji haki.
Majaji na mahakimu wana uhuru kamili wa kuendesha na kutoa maamuzi juu ya kesi mbalimbali na kwa hiyo ili kuutunza uhuru huo, jaji mkuu anapaswa ajiepushe na mazingira yoyote yanayoweza kumfanya kuingilia uhuru wa majaji na mahakimu.
Uhuru walionao majaji na mahakimu, anao pia Jaji mkuu. Lakini kwa kitendo cha kuhusishwa katika maelekezo maalum ya serikali kwa watendaji wake, amejifanya kuwa mtendaji kama wao na hivyo kupokea maelekezo ya mkuu wa serikali. Athari za kitendo hiki zitaonekana hivi punde katika utendaji wake.
Nasema haya kwa sababu uhuru wa mahakama umekuwa ukilalamikiwa na wengi. Uteuzi wa Jaji mkuu na majaji unaoacha maswali mengi, pamoja na mbinyo wa bajeti ya mahakama unaosababisha mahakama iwe ombaomba kwa serikali, vinaufanya uhuru wa mhimili huu uwe wa kinadharia zaidi.
Kuna mambo mengi ya kuhoji. Mathalani wakati wakuu wa mihimili ya serikali na bunge wana uhuru wa kuteua au hata kuongoza michakato ya kuchagua watendaji fulani katika mihimili yao, mhimili wa mahakama, jaji mkuu anateuliwa na rais na anapokea pia majaji atakaowaongoza kutoka kwa rais.
Hata kama rais anaweza kumshirikisha wakati wa uteuzi, bado hana mamlaka itoshayo juu ya majaji wengine kwa sababu aliyemteua yeye, ndiye aliyewateua wao. Utaratibu huu unaufanya mhimili wa mahakama kuwa sehemu ya mhimili wa serikali.
Matokeo ya mchakato huu wa kisiasa unaolazimishwa kuingia mahakamani, haki za watu zinacheleweshwa na hivi sasa bila fedha au kujuana na mtu mkubwa katika mahakama zetu ni ndoto mtu kupata haki yake kwa wakati.
Madhambi yaliyozagaa katika vyombo vingine vya dola na ndani ya serikali, yamezagaa pia katika mhimili wa mahakama kiasi cha kutishia amani ya taifa letu.
Imani ya maskini katika mahakama zetu imetoweka na kwa hiyo badala ya jaji mkuu kuhudhuria semina elekezi za serikali angeendesha za kwake ili kutafuta suluhu ya matatizo ya ndani ya mahakama.
Baba wa Taifa aliwahi kusema wakati akiwahutubia majaji kuwa, uhuru wa mahakama ni dhana kwanza kabla haijawa vitendo. Dhana hii inatakiwa ionekane uhalisi wake katika mwenendo wa majaji wenyewe na jinsi wanavyohusiana na viongozi wa serikali.
Mwenendo na maisha binafsi ya majaji vinahitaji visiache maswali juu ya uhuru wao katika kutoa maamuzi ya haki kwa Watanzania. Hivi sasa kuna wakuu wa mikoa (RC) na wilaya (DC) wanadiriki kuandika barua za maelekezo kwa mahakimu au kutoa maelekezo kwa watendaji wa chini yao kisha kuwapa nakala mahakimu kana kwamba wanataka barua hizo zitumike kama ushahidi dhidi ya watakaokiuka maelekezo hayo na kufikishwa mahakamani.
Imetokea hadharani mahakimu kuagizwa na ma-DC na ma-RC kujificha ili kuwakwepa wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutosaini viapo vyao nyakati za uchaguzi. Siyo siri tena kuwa majaji kupitia jaji mkuu wanapokea maelekezo ya nini kifanyike katika kesi nyeti zinazogusa maslahi ya kisiasa ya chama fulani au wanasiasa fulani.
Tumeshuhudia mahakimu wakipokea maelekezo maalum kutoka kwa wakuu wao juu nini kifanyike katika kesi fulani zenye mvuto wa kipekee. Tumeshuhudia masharti ya dhamana za washtakiwa fulani zikifanywa kuwa ngumu ili kuwaridhisha wakubwa fulani.
Vitendo vya namna hii vinaiondolea mahakama heshima na hadhi yake mbele ya jamii. Hata kukithiri kwa rushwa katika chombo hiki nyeti ni dalili tosha kuwa hakina uhuru wowote juu ya maamuzi na uendeshaji wake.
Uhuru kamili wa mahakama ni tishio kwa watawala dhalimu kuliko ulivyo tishio kwa wahalifu wa kawaida wa sheria. Kwa mantiki hiyo, kuongezeka udhalimu katika utawala wa nchi ni dalili kuwa uhuru wa mahakama unapungua.
Uwiano huu wa ongezeko la udhalimu wa watawala na kupungua kwa uhuru wa mahakama, ndicho kiini cha mwaliko wa jaji mkuu Othman Chande katika semina elekezi ya watendaji wa serikali kule Dodoma.
Tujiulize, siku serikali hii ikishtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma kupitia semina elekezi, Jaji Mkuu atakuwa mshatkiwa au shahidi?
Mwisho




Mapenzi ulevi ndugu yangu na mlevi hakubali kuwa anachafuwa akili yake. Hivyo hayo unayoyasema wewe mwenyewe unayaamini. Bahati yako kuwa jukwaani hapa ni baa ( kijiwe cha walevi).
Hivyo kitendo alichofanya Mbowe alielekezwa na huyo Zoka au ulikuwa uamuzi wake mwenyewe? Mbona hili ni jambo dogo sana la kupigiwa kelele kama hivi? Si kuna mbunge anasotea ndani nae Chande na Othman wanahusika?
Wanachama wa CHADEMA wamezoelea kuona Craps posting zote zinazopingana na hoja zao za nguvu lakini hii hoja yako imevunja rekodi ya kuwa haina maana. Hata hivyo walevi wenzio wako , usiwe na wasiwasi mtaendelea kulewa.
 
Wewe usijitie ujinga fujo zimeanza tokea Slaa alipotangaza nchi kutotawaliwa,hutosikia mimi wala mtoto wa mbowe kapigwa bomu la machozi ila ni ninyi wapuuzi ndio mtakao kufa kama kuku kwa kupenda kutumiwa kama kondomu kwa manufaa ya wachache.

Dogo usilete ujinga hapa na akili zako mbovu,kama hujui kinachoendelea kaa hapo hapo ndani ule na ukajaze choo na sio kushabikia usilolijua....
 
Ndio, Jaji Mkuu ni mdogo wake Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Hakuna kurithi! Ibara ya 118 ya Katiba haina restrictions za nani anaweza kuteuliwa kuwa jaji mkuu, zaidi ya requirement kwamba awe na sifa za kuwateuliwa jaji wa kawaida.

Si kweli!!!! Labda nikukumbushe hili: inaangaliwa na kesi alizowahi kusikiliza in other words uzoefu na record kwenye mahakama zetu za Tanzania etc. Tuseme ukweli, Jaji Othman amesikiliza kesi 18 tu miaka yote aliyofanya kazi mahakama za Tanzania. Further than that, mpaka ninazungumza sasa hivi hakuna aliyeweza kupata record ya hukumu yake hata moja alishowahi kutoa kwenye mahakama za Tanzania. (Kumbuka kusikiliza kesi sio kutoa hukumu). Lakini kama ipo na wewe unaushahidi wa hiyo hukumu naomba ui-post/au nielekeze pakuipata. (In short kwenye kumbukumbu za mahakama hamna/hazionekani.
 
Facebook by William Malecela on Sunday, June 5, 2011 at 9:01am


@ NEW YORK: Tumezipokea kwa mshituko mkubwa sana habari za kukamatwa kwa Mheshimiwa Mbowe, kutokana na amri ya mahakama huko Arusha. Ninashangazwa sana na ukaidi huu wa kiongozi wa chama kikuu sana cha upinzani nchini, ambacho baadhi yetu tumekua tukifarajishwa sana na kuwepo kwake kwani tunaamini sana kwamba kinatusaidia sana wananchi wa taifa hili kwa kumkosesha sana usingizi Tembo CCM na kuwafanya wajitahidi kutuheshimu wananchi, japo hata kidogo!

- However, sheria za jamhuri yetu ambazo Chadema mmekua mstari wa mbele sana kuzililia zifuatwe na CCM, ni lazima pia ziheshimiwe na Viongozi wenu, sio wa Chadema tu bali wa chama chochote cha siasa nchini. My very friend Mh. Mbowe una makosa sana kisheria kukataa amri ya mahakama ya jamhuri na ni matumaini yangu kwamba mahakama hii itafuata sheria na kukupa kifungo japo cha wiki moja ili kuweka mfano kwetu wananchi kwamba sheria ni msumeno. Na wapi pazuri pa kuwaonyesha mfano wananchi kama sio kwenye kiongozi wa juu kama wewe? Kwa wale mnaojaribu sana kuigeuza hii ishu kuwa ni politics please tuoneeni huruma sana wananchi wa hili taifa, kwa sababu it is not! hii ni simply ishu ya kutoheshimu sheria na kwa Mh. Mbowe na Chadema kujiona kwamba mko juu ya sheria, yaani hata hamjashika nchi tayari mnaanza kutuonyesha makucha yenu, inakatisha sana taamaa! I mean Chadema na Mbowe nini hasa mnachotaka kutuambia sisi wananchi na hiki kitendo cha kutoheshimu sheria ya jamhuri?

- Chadema tumewaambia sana kwamba zile dakika 15 za fame zimekwisha siku nyingi, sasa fanyeni kazi ya kujiimarisha vijijini uchaguzi uliopita mmeweza kuongeza viti vingi sio kwa sababu wananchi wanawapenda na kuwaamini kuliko CCM, hapana zilikuwa ni kura za magomvi ya CCM kwa CCM. I mean hizi siasa za fujo na magomvi na kutoheshimu sheria wananchi wa taifa hili hatujazizoea kabisa na wala hatuzihitaji katika mwendo wa kutaka kulikomboa taifa letu, tujadili hoja kwa hoja sio fujo kama mnavyotaka kutufundisha sasa!, Chadema kumbukeni kwamba taifa hili tulipata uhuru kwa hoja na sio mafujo kama yanayofanywa na Mwenyekiti wenu!

Chadema na Mheshimiwa Mbowe, Shame On You All!

William Malecela @ NYC, USA.


I suspected long ago that u don't have the balls to step up when it matters. All matters to u is ur interests & CCM's.
 
Ridhiwan F........... .*.*you know what just tell uer dad we dnt fear anymore FREEDOM IS COMING TOMORROW
Ikiwa hili ndio zao la Chama kinachotaka madaraka, Mungu atuepushie nacho kama ukoma! Hoja huwa inajibiwa kwa matusi! Loh mnahitaji dictator nyie awaongoze1
 
wewe au ndugu zako mna kinga gani kiasi kwamba mtiti ukianza iwe impossible kudhurika? hata huyo rais wa yemen nae kaonja shubiri licha ya kuwa analindwa vikali sembuse mbwiga kama wewe?
Pengine nyie hamna silaha kama walivyokuwa nazo wale wa Yemen. Busara ya huyo unaemkana naona ina hoja kwani makelele hayafui dafu kwa silaha. TTumeshaona kuwa washujaa wanachokula ni sherehe za mizinga lakini wale wenye busara ndio hutumia mafao ya vifo vya mashujaa.
 
Sheria haina mkubwa wala mdogo.tusitake kuyumia umma uwe ngao ya maovu yetu na watu hatari ni wale wanaochukua suala la mahakama kisiasa zaidi.hata serikali haiwezi kuingilia maamuzi ya mahakama.mbowe aldharau mahakama ndio maana amekamatwa.hakuna aliye juu ya sheria.watanzania wenzangu tuheshimu sheria maana sheria ni msumeno.

Hapa kweli wewe unaonekana umezaliwa leo hii Muhimbili. Unajiuliza swali ambalo mtoto wa shule ya chekechea atakuzidi akili. Kosa la Mbowe limeanzia wapi? Aliepeleka kesi mahakamani ni nani? Waliteuliwa ktk nyadhifa za serikali kila mahali i.e. mahakama, jeshi la polisi na ulinzi, BOT, PM ni nani? Unafikiri kikwete na ccm hakuwa na madhumuni kujenga katiba ya namna hii? Lets follow this scenario, what if mkuu wa polisi au jaji wangeteuliwa na kufanyiwa screening and in a transparent ways wangapi wenye makosa wangeshitakiwa na kupelekwa jela? Unafikiri Mbowe angekuwa jela au hii kesi ingefunguliwa Arusha. Mimi kweli sipendi wananchi wanaotoa comments au for their ignorance or as makada wa ccm. If you have no clew au kwa uzembe wako hutaki kufanya researches za constitutions around the world, please don't inject false ideologies JF.
 
Fungua link hii ya yahoo news uweze kusoma

Tanzania judge urges arrest of opposition leader - Yahoo! News

NB: Japo kuna makosa madogomadogo kwa muono wangu wanapotumia Judge badala ya Magistrate, na pia kutumia postmodification baada ya Jina la Dr. Slaa kusema A LOSER kwenye uchaguzi uliopita, kawaida hio sio njia sahihi ya kumtambulisha mtu. Walitakiwa kusema mshindi wa pili, unaposema A LOSER inakuwa na Negative connotation. Naamini huyo mwandishi hawezi kumtambulisha John McCain au Kerry kama Losers kwakuwa walishindwa kwenye uchaguzi wa hapa Marekani

MAKULILO, Jr.
California
 
Ndugu yangu William,
Huu ujumbe wako ungemshauri the late Martin Luther King Jr. katika miaka ya sitini usingeeleweka kabisa. Huwezi kuheshimu sheria kandamizi, na lazima mmoja ajitolee kafara ili sheria kandamizi zijadiliwe na zibadilishwe. That is what happened in the US. Yule Mama Rosa Parks (rip) alichoka kukalishwa kiti cha nyuma cha basi kwa sheria kandamizi, akagoma. MLK alifungwa jela mara kadhaa kwa kukaidi sheria kandamizi. Wewe ungekuwepo wakati huo nina hakika ungesema shame Dr. Martin Luther King Jr, shame black Americans, for not following the laws. Inastaajabisha. Na kwa mantiki hiyo katika karne hii ujumbe wako huo haueleweki kabisa.

- Kesi za Martin Luther King zilikuwa na za kisiasa, hii ya Mbowe ni ya kisheria, kama una mashitaka mahakamani ukikosa kuhudhuria kesi yako unatakiwa kushikwa na kuwekwa ndani, hakuna siku hata moja Mrtin Luther king, aliwahi kukwepa kwenda mahakamani!

- Hiii kesi ya Mbowe haina anything to do na politics, ingawa naiona juhudi kubwa sana ya kuiiingiza kwenye politics ni ujuha sana kwa sababu mnaweka njia ambayo mkishika power itawaumiza wenyewe, ndio maana tunaoweza kuona mbaali tunakataa kwa nguvu zote kwamba kwenye hili Mbowe amekosea, ninakubali kwa 100% kwamba kukamatwa kwa Zitto jana yalikuwa ni makosa sana na pia kwa polisi kutomhamisha Mbowe haraka sana kwenda Arusha, nayo ni makosa makubwa sana!

- I hope hakuna mafisadi kabsia kwenye hiili tatizo maana kama nawaona wapo somewhere!


William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom