Kukamatwa kwa Mbowe, jaji mkuu Chande anahusika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa kwa Mbowe, jaji mkuu Chande anahusika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 5, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakuna mashaka kwamba kukamatwa kwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini kumetokana na maelekezo ya Jaji Mkuu, Othuman Chande ambaye ameigeuza mahakama kuwa idara ya siasa ya serikali.

  Chande aliyehudhuria semina elekezi wiki iliyopita, nimeelezwa amechukua hatua hiyo ili kumnusuri mdogo wake, Othuman Rashid ambaye idara ya usalama wa taifa imemshinda kwa kuwa sasa imegawanyika mapande mawili - moja linaongozwa na yeye na jingine linaongozwa na Zoka.

  Taarifa zinasema hatua ya Chande ya kushinikiza Mbowe akamatwe inakusudia kumsaidia Kikwete kupata nafuu ya kisiasa baada ya kutuhumiwa na wenzake kuvuruga chama. Gazeti mashuhuri la kila wiki nchini - MwanaHALISI lilijadili hatua ya Jaji Chande kuhudhuria semina elekezi katika toleo lake la wiki iliyopita na bila shaka yanayotokea leo, ni sehemu ya matunda ya semina hiyo.

  Jaji mkuu ni sehemu ya serikali?

  Na Isaack Kimweri​

  SEMINA elekezi iliyoandaliwa kwa ajili ya watendaji serikalini wiki tatu zilizopita mjini Dodoma imeibua jambo zito.
  Jambo hilo ni ushiriki wa mihimili mingine miwili ya dola Bunge na Mahakama katika semina hiyo ambayo ililenga mhimili wa tatu – watendaji wakuu serikalini.
  Katika hali ya kawaida, mihimili hii haitakiwi kuingiliana katika utendaji wake wa kila siku.
  Kwa bahati mbaya na kwa kweli kwa utashi wa kiitikadi, katiba ya Jamhuri imempa ruhusa rais kuteua wabunge kuwa mawaziri na hivyo kulifanya bunge kuwa sehemu ya serikali. Kelele nyingi zimepigwa juu ya kasoro hii na naamini kuwa katiba mpya itashughulikia kasoro hii ili mihimili hii itenganishwe.
  Wengi tunaamini mahakama haipokei amri wala maelekezo kutoka serikali wala bunge. Ni matumaini ya wengi kuwa mihimili hii itaendelea kutenganishwa kwa ajili ya kuboresha utawala bora katika taifa letu.
  Kilichoshangaza katika semina elekezi ile ni uwepo, siku ya ufunguzi, wa Jaji Mkuu Othman Chande. Baadaye nilidokezwa kuwa alikuwa mmoja wa watoa mada (mwezeshaji).
  Uhusika wa Jaji mkuu katika semina elekezi ya viongozi wa serikali unatia shaka na kuna kila sababu ya kuhoji utaratibu huu mpya wa utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne.
  Jamhuri yetu si ya muungano wa mihimili ya dola kiasi cha kumfanya Jaji Mkuu kuwa sehemu ya serikali. Ili kumwepusha na majaribu yanayoweza kutia dosari maamuzi yake na uendeshaji wa mhimili wa mahakama, Jaji mkuu anapaswa kuwa mbali na maelekezo ya serikali – asiyasikie wala kuhusika kama chombo cha kuyatoa kwa watendaji wa serikali.
  Hii ni kwa sababu, baadhi ya watendaji wa serikali wanaweza kujikuta wakitenda kazi zao kwa kuongozwa na jinsi jaji mkuu alivyosema au kujikuta wanamtumia kama shahidi wao ili kuwatisha waathirika wa maamuzi yao.
  Jaji mkuu, kama mwanadamu, ana utashi binafsi na vionjo vya kiitikadi. Unapomhusisha katika semina elekezi ya watendaji wa serikali, unachokoza vionjo vyake na matamshi yake kiitikadi yanayoweza kuamsha na kuingilia maamuzi yake ya baadaye anaporejea katika wajibu wake wa kazi zake.
  Ikumbukwe kuwa serikali iliyo madarakani ina sera maalum na ilani yake ya uchaguzi ambayo ni tofauti na vyama vingine ambavyo havijazuiwa kuchukua madaraka ya nchi wakati jaji mkuu akiwa bado madarakani. Hali hiyo ikitokea, jaji mkuu huyo atapokea au kushiriki semina elekezi ngapi?
  Jaji mkuu ni kiongozi mkuu wa mhimili wa mahakama lakini si kiranja mkuu mwenye wajibu wa kuhakikisha majaji na mahakimu wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata maelekezo yake katika jukumu la utoaji haki.
  Majaji na mahakimu wana uhuru kamili wa kuendesha na kutoa maamuzi juu ya kesi mbalimbali na kwa hiyo ili kuutunza uhuru huo, jaji mkuu anapaswa ajiepushe na mazingira yoyote yanayoweza kumfanya kuingilia uhuru wa majaji na mahakimu.
  Uhuru walionao majaji na mahakimu, anao pia Jaji mkuu. Lakini kwa kitendo cha kuhusishwa katika maelekezo maalum ya serikali kwa watendaji wake, amejifanya kuwa mtendaji kama wao na hivyo kupokea maelekezo ya mkuu wa serikali. Athari za kitendo hiki zitaonekana hivi punde katika utendaji wake.
  Nasema haya kwa sababu uhuru wa mahakama umekuwa ukilalamikiwa na wengi. Uteuzi wa Jaji mkuu na majaji unaoacha maswali mengi, pamoja na mbinyo wa bajeti ya mahakama unaosababisha mahakama iwe ombaomba kwa serikali, vinaufanya uhuru wa mhimili huu uwe wa kinadharia zaidi.
  Kuna mambo mengi ya kuhoji. Mathalani wakati wakuu wa mihimili ya serikali na bunge wana uhuru wa kuteua au hata kuongoza michakato ya kuchagua watendaji fulani katika mihimili yao, mhimili wa mahakama, jaji mkuu anateuliwa na rais na anapokea pia majaji atakaowaongoza kutoka kwa rais.
  Hata kama rais anaweza kumshirikisha wakati wa uteuzi, bado hana mamlaka itoshayo juu ya majaji wengine kwa sababu aliyemteua yeye, ndiye aliyewateua wao. Utaratibu huu unaufanya mhimili wa mahakama kuwa sehemu ya mhimili wa serikali.
  Matokeo ya mchakato huu wa kisiasa unaolazimishwa kuingia mahakamani, haki za watu zinacheleweshwa na hivi sasa bila fedha au kujuana na mtu mkubwa katika mahakama zetu ni ndoto mtu kupata haki yake kwa wakati.
  Madhambi yaliyozagaa katika vyombo vingine vya dola na ndani ya serikali, yamezagaa pia katika mhimili wa mahakama kiasi cha kutishia amani ya taifa letu.
  Imani ya maskini katika mahakama zetu imetoweka na kwa hiyo badala ya jaji mkuu kuhudhuria semina elekezi za serikali angeendesha za kwake ili kutafuta suluhu ya matatizo ya ndani ya mahakama.
  Baba wa Taifa aliwahi kusema wakati akiwahutubia majaji kuwa, uhuru wa mahakama ni dhana kwanza kabla haijawa vitendo. Dhana hii inatakiwa ionekane uhalisi wake katika mwenendo wa majaji wenyewe na jinsi wanavyohusiana na viongozi wa serikali.
  Mwenendo na maisha binafsi ya majaji vinahitaji visiache maswali juu ya uhuru wao katika kutoa maamuzi ya haki kwa Watanzania. Hivi sasa kuna wakuu wa mikoa (RC) na wilaya (DC) wanadiriki kuandika barua za maelekezo kwa mahakimu au kutoa maelekezo kwa watendaji wa chini yao kisha kuwapa nakala mahakimu kana kwamba wanataka barua hizo zitumike kama ushahidi dhidi ya watakaokiuka maelekezo hayo na kufikishwa mahakamani.
  Imetokea hadharani mahakimu kuagizwa na ma-DC na ma-RC kujificha ili kuwakwepa wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutosaini viapo vyao nyakati za uchaguzi. Siyo siri tena kuwa majaji kupitia jaji mkuu wanapokea maelekezo ya nini kifanyike katika kesi nyeti zinazogusa maslahi ya kisiasa ya chama fulani au wanasiasa fulani.
  Tumeshuhudia mahakimu wakipokea maelekezo maalum kutoka kwa wakuu wao juu nini kifanyike katika kesi fulani zenye mvuto wa kipekee. Tumeshuhudia masharti ya dhamana za washtakiwa fulani zikifanywa kuwa ngumu ili kuwaridhisha wakubwa fulani.
  Vitendo vya namna hii vinaiondolea mahakama heshima na hadhi yake mbele ya jamii. Hata kukithiri kwa rushwa katika chombo hiki nyeti ni dalili tosha kuwa hakina uhuru wowote juu ya maamuzi na uendeshaji wake.
  Uhuru kamili wa mahakama ni tishio kwa watawala dhalimu kuliko ulivyo tishio kwa wahalifu wa kawaida wa sheria. Kwa mantiki hiyo, kuongezeka udhalimu katika utawala wa nchi ni dalili kuwa uhuru wa mahakama unapungua.
  Uwiano huu wa ongezeko la udhalimu wa watawala na kupungua kwa uhuru wa mahakama, ndicho kiini cha mwaliko wa jaji mkuu Othman Chande katika semina elekezi ya watendaji wa serikali kule Dodoma.
  Tujiulize, siku serikali hii ikishtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma kupitia semina elekezi, Jaji Mkuu atakuwa mshatkiwa au shahidi?
  Mwisho


   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hakika inashangaza kwa nini alihudhuria hiyo semina elekezi. Kishaingia katika mfumo wa kifisadi wa CCM, Mahakama inazidi kukosa uhuru wake kikatiba na hivyo haki kupotea.

  Halafu huyo Chande hakustahili kupata wadhifa huo mkuu kwani kuna majaji wqengine wanne wa Mahakama ya Rufaa wamerukwa (katika order ya seniority). Kwa hali hii maamuzi yake yote yanayohusu serikali ya JK yatatiliwa shaka.

  Nchi hii inazidi kupotea njia.
   
 3. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii nchi inabdi cku tunaamua tunaandamana kwenda ikulu wote,tumechoka kuona na kusikia nchi hii ikiendeshwa kijingajinga.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Asante Mkuu kwa kutufumbua macho katika yale yanayoendelea katka idara ya UWT. Hivi kuna kitengo gani katika srikali ya JK ambacho hakuna makundi? kila mahali tunasikia kuna makundi mawili au zaidi -- na utakuta kundi moja linapinga ufisadi wa serikali ya JK na moja kutetea. Hii imekuwa b.f. country!!! Na bila shaka utawala wa kimakundi ndiyo husababisha siri kubwa kubwa za serikali kuvuja kwa akina Dr Slaa.

  Maana yake ni kwamba yote asemayo Dr Slaa kuhusu uozo serikalini ni ukweli mtupu.
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo hoja ya udini inapopata mashiko kuwa JK ni mshabiki mkubwa sana wa udini na udini huo huo ndiyo utakao mng'oa madarakani.
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MMMMH
  kunakitu chaja
  kila mtu ktk seriklai analinda kitumbuwa chake,sijui kama tutafika kwa mtindo huu,
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Jaji mkuu,Semina elekezi,Kukamtwa kwa Mbowe,Usalama wa taifa?????????????
  Tuombe Mungu.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  andaeni dhana tayari kuwang'oa wakoloni weusi ktk taifa hili. Mko tayari. ?
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kwani tunaposema Serikali tunamaanisha nini hasa?,

  Na je,ni vitu vipi hasa vinaunda Serikali?
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kikwete kikwete tumekufanya nini mpaka utuharibie nchi yetu? Ufisadi ulioufanya na kuingiza nchi yetu kwenye mikataba feki bado hujakoma unazidi kutuchafua na kutuharibia taifa letu, Ipo siku tutadili na wewe fisadi usiye na haya
   
 11. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Uko wapi uhusiano wa kukamatwa kwa Mhe. Mbowe, Jaji Mkuu na Semina Elekezi?

  Mwandishi alikuwa na lengo zuri la kutuelimisha kuhusu athari za ushiriki wa mara kwa mara wa Mhimili wa Mahakama katika shughuli za Serikali, Sioni ubaya katika hili na sioni ubaya pia kwa JAJI MKUU kutoa mada katika Semina Elekezi ya Watendaji wakuu Serikalini yenye lengo la kupanua uelewa wa Watendaji hao kuhusu Wajibu na Majukumu ya Mahakama.


  Naomba ufafanuzi hapa, kukamatwa kwa Mhe. Mbowe kumesababishwa na yeye kutenda kosa gani?

  Tujiandae kuondoa dosari zinazosababisha Viongozi wetu wa Upinzani kudhalilishwa sasa kwa kupendekeza kuondolewa kwa Ibara na Vifungu vya KATIBA ya sasa vinavyoendekeza mambo hayo.

  Pamoja daima.
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Mwandishi anahitaji maombezi. Keshasahau kuwa kuna mihimili mitatu ya DOLA na sina hakika kama anafahamu maana ya DOLA.
   
 13. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 530
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 80
  Kama mambo yanakera hivi secret snipers watumike..
   
 14. M

  Majasho JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wabunge wote wa chadema wanaanza safari ya kwenda arusha kumtetea mwenyekiti wao badala ya kwenda dodoma kutetea maslahi ya wananchi wao.

  Huu mpango wa makusudi wa mh mbowe kujikamatisha makusudi ili kupata headlines throughout the week sio jambo jema kwa maendeleo ya nchi yetu.

  Haya wabunge wote wa chadema wanaanza arusha. Bajeti itapita bila mchango wao na maendeleo hamna.

  ===================
  MODERATOR'S COMMENT:

  Wabunge wa CHADEMA wanaoenda Arusha ni wachache na si wote kama ambavyo mwanzisha hoja anajaribu kuufahamisha umma hapo juu. Hakuna mbunge aliyeshurutishwa ama kuamriwa kwa mujibu wa wabunge wa CHADEMA.
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,372
  Likes Received: 22,234
  Trophy Points: 280
  CCM mna ufinyu wa fikra, acheni kupotosha umma
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli, hii inatofauti gani na kudumisha 'fikra za mwenyekiti'?
   
 17. Josephine

  Josephine Verified User

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acha uzushi,subiri mje muone.
   
 18. M

  Mboja Senior Member

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sio ufinyu tu wa fikra wananuka uozo pia. Kwani kitu keoza kinauzika?
   
 19. O

  Omr JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na kama watakwenda Arusha na kuacha bunge basi hawa watakua ni wapumbavu wakubwa.
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  CCM SIKIO LA KUFA! Hamfanikiwi kwa mpango wenu wa kipumbavu, Headlines kitu gani? Kazipata sana 2005 akiwa mgombea. Kueni kifikra pls!
   
Loading...