Kukamatwa Kwa Freeman Mbowe: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa Kwa Freeman Mbowe: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Jun 6, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  AFRIKA kuna mambo. Na Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia. Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!

  Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi. Lakini mie ni mmoja kati ya wachache, ambao, kwenye pambano kama hilo, hupenda kusimama katikati, hata kama ni kazi ngumu.

  Na punde tu imemalizika raundi ya kwanza ya mpambano wa majogoo; Freeman Vs Police. Ndio, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa kambi ya Upinzani ameachiwa huru leo kule Arusha baada ya kujisalimisha polisi juzi na kisha kulazwa rumande. Na tumesikia, kule Arusha amesafirishwa kwa ndege!

  Kimsingi, Freeman alichemka kwa kutokuwa makini na kufuAtilia taratibu za Mahakama. Kama mwenyekiti wa Chama na Kiongozi wa kambi ya Upinzani alitakiwa awe mfano katika umakini. Lakini, Polisi walichemka zaidi kwa kumkamata Freeman aliyekwenda mwenyewe kituoni kujisalimisha na hata kumlazimisha avue viatu na kumsweka rumande.

  Hivi, kulikuwa na lazima ya polisi kutumia rasilimali zote zile kwa mtu mmoja Freeman Mbowe? Ni kiasi gani haswa kimetumika kugharamia 'operesheni' ile ya kumfikisha Freeman mahakamani Arusha? Freeman Mbowe hafanani hata kidogo na Mulla Omar!

  Kwa kilichofanyika , Freeman Mbowe na Chadema yake walijikuta wakipigiwa penalti mikononi. Ningalikuwa afande wa polisi ningeelekeza moja tu; Kama Freeman kajisalimisha, aambiwe vema na aamrishwe kurudi kituoni alfajiri siku inayofuata tayari kwa safari ya Arusha akiongozana na polisi wa kiraia. Safari hiyo iwe ya kipolisi na wala asisindikizwe na viongozi wa Chadema wala mashabiki wake.

  Na sharti ni moja tu; asipoonekana kituoni kumi na mbili alfajiri, basi, akamatwe na kusafirishwa akiwa na pingu mikononi. Makubaliano hayo yatiwe saini na Freeman mwenyewe.

  Hivyo basi, kiungwana, Freeman angeambiwa arudi nyumbani kwake, akaungane na familia yake. Awaage kwa amani kuwa kesho yake ana safari ya kwenda Arusha akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa kiraia. Juu ya yote, Freeman ni mheshimiwa mbunge, na kiongozi wa kambi ya upinzani, anastahili hata kuwa na body guard anayelipwa fedha za walipa kodi.

  Hatua hiyo ya kiungwana ya polisi ingebakisha pigo kwa Freeman, maana, focus ingebaki kwenye uzembe wake mwenyewe ( Freeman) wa kutofuatilia kwa makini taratibu za kimahakama.

  Badala yake, kitendo kile cha polisi kumweka rumande Freeman na kumsafirisha kwenda Arusha katika mazingira tuliyoyaona kimehamisha focus ya tatizo la msingi la Freeman, uzembe. Kimeipa Chadema sympathy ya umma kwa dhana ile ile, kuwa wanaonewa. Na juu ya hapo Chadema inanunua umaarufu kwa gharama nafuu. Na siasa inahusu kutafuta umaarufu kwa wapiga kura. Ukifanikiwa kumwonyesha mwingine si makini, basi, unampunguzia umaarufu.

  Si tumeona, sasa Freeman anaonekana ' shujaa'. Tena kamanda ngangari, si amelala hata rumande! Afrika U-Mandela ni sifa ya ziada kwenye CV ya mwanasiasa. Na mahabusu za Afrika zinatofautiana. Watu wanajua, kuwa mahabusu wengine hutayarishiwa ' makao' yao, iwe Keko au Ukonga.

  Si tulisikia habari za Keko kufanyiwa ukarabati kuandaa ' makao' ya akina Grey Mgonja na Basil Mramba. Naam, Mahabusu wengine ni 'Waheshimiwa'. Hata Keko wanalala kwenye viyoyozi na kuangalia runinga bila kubughudhiwa na mahabusu wengine. Na hapa ndipo wengine wanaziona chembe za uonevu.

  Na katika hili la Freeman na polisi limemwibua hata Profesa Ibrahim Lipumba aliyepotea kwenye 'game'. Ndio, Lipumba kwa kipindi kirefu sasa amepotea uwanjani. Ghafla, naye ameiona krosi hii iliyopigwa na Chadema baada ya kuudaka kirahisi mpira wa penalti.

  Ndio, Profesa amerudi tena uwanjani. Ameishutumu vikali polisi na kutamka kuungana na Chadema kwenye kuandama. Na media imempa Profesa coverage ya kutosha. Wako wapi sasa wanaosema CUF ni CCM 'B'? Profesa ni mzoefu kwenye mchezo wa siasa.

  Lakini, kuna mchezaji kwenye timu ya upinzani ambaye hata kwenye jukwaa la watazamaji haonekani siku hizi. Si Unamjua? Au labda nikusaidie; Ni James. Alipata kuwa mshambuliaji hatari sana. Lakini sasa hata kivuli chake hakionekani. Ni James Mbatia wa NCCR.

  Kulikoni NCCR? Au inahusu ugomvi wa jimbo la Kawe na madai ya bilioni moja kwa Chadema? Lakini hata Profesa si ana kaugomvi na Chadema, lakini, kwa penalti ile ya Polisi kuwapigia Chadema mikononi, Profesa ameamua kusahau ya nyuma na kurudi kwenye ' game'.

  Na swali ni hili; Je, Profesa naye amerudi|? Au ni shambulizi la msimu tu?

  Na tusubiri tuone.
  Maggid,
  Iringa,
  Jumatatu, Juni 6, 2011
  mjengwa.blogspot.com
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Maggid,
  Umehukumu mapema. Ukishasikia kilichojiri na kusababisha Freeman asiwepo mahakamani utakula matapishi yako.
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mhhhhhhh mjengwa bwana
  uchammbuzi wako umetulia
  ngoja tuone nini kitajiri ktk hili
  kimsingi ccm wamefanya faulo itakayowagharimu
  nasema ni ccm kwa sababu ndo wamewatuma mbwa wao
  harafu ndo kwanza wamewapandisha chati chadema
  yaani wamejipiga bao la kisigino pasipo kutarajia
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nadhani chadema wameshaeleza kwa nini freeman hakutokea mahakani na inaonekana taarifa zilimfikia hata hakimu aliandika waraka wa kumkata. ndo maana binafsi naamini kuwa ccm waliwatuma mbwa wao kufanya vile wamefanya wakilenga kumdhalilisha freeman
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Leo kaka nimekusoma mwanzo mwisho..na nimekuelewa..maoni kama haya ya uwazi bila upendeleo yatafanya niibookmark maggid blog kwenye pc yangu
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Maggid, nimekuwa nasoma makala zako na nadhani nyingi ni 'tafsiri' yako juu ya current issues.

  Sasa mimi ningeshauri ubadili hii heading yako kidogo 'Tafsiri ya Majjid' x,yz... kwa hiyo kila week tunajua or expect kusoma tafsiri ya Majjid juu jambo fulani. Kwa mfano week hii inaweza kuwa Tafsiri ya Majjid: Kukamatwa kwa Mbowe. next week ikawa Tasfiri ya Majjid... Bajeti ya serikali yakwama:) n.k. Nadhani umenipata. Sorry wanaJF nimetoka nje ya mada lakini ni wazo nimekuwa nalo kwa muda.
   
 7. K

  KAPIRIPIRI Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu Majjid kama mwandishi tafiti kilichomfanya Freeman Mbowe asiende mahakamani.Usimhukumu bila kujua kilichojili....
   
 8. 911

  911 Platinum Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Yanini kuanzisha thread mpya kwa jambo ambalo kuna thread lukuki zikilijadili.Muda mwingine huwa deliberately mnaamua kuwachosha mods.Grrrr..
   
 9. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Maggid ni nomaaa umewachana balaaaa
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Tafsiri ya mahakama Mbowe ameonekana hana kesi ya kujibu, kwahiyo miguvu yote iliyotumika = 0.

  Sahihisho: Mbowe hakuchemka kwa lolote kwenye sakata hili bali ni mkanganyiko wa mdhamini wake. nakuomba ondowa hii thread yako uiedit halafu ndio uilete tena hapa jamvini, ukiiacha hivi ilivyo itakushushua heshima utaonekana unaokoteza habari vichochoroni. ni ushauri tu mkuu.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,869
  Trophy Points: 280
  haya kamwene, wasalimie makamanda wako wale mzee
   
 12. g

  graceirene Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mjegwa ,
  Kilichotokea ndani ya mahakama ndiyo hoja ya msingi kwamba licha ya hakimu kuagiza mbowe akamatwe aletwe mahakama lakini hakumuuliza chochote yaani mdhamini wake ndiyo aliyehojiwa kwa nini hakufika mahakamani siku ya kesi , mbowe alikaa mahakamani km msikilizaji tu
  Embu endelea kujadili kwa msingi huu
   
 13. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakati mwingine wendawazimu huongea maneno yaliyo changanyikana na point! hivyo inakuwa vigumu sana kuwasaidia.........
   
 14. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Hili ndilo tatizo la mtu kupata habari nusunusu na kuzitolea hukumu bila kuchunguza kwa kina,yaani unajikwaa na kuanguka na badala ya kuangalia ulipojikwaa wewe unaangalia ulipoangukia!!!!?
   
 15. Tonny

  Tonny JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wether ur wrong o right Mr Maggd, ths z ver bg advantage 2 Mbowe na Chadema
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Chambuwa, kokotowa, sasambuwa, lakini ukweli unabaki ukweli tu, Ukivunja sheria za mahakama unapelekwa kwa nguvu ya dola. Sasa bwan Maggid kama diplomasia haikutumika hayo si makosa na ingetumika ingekuwa ni makosa.

  Diplomasia kama uitakayo bwan Maggid ingetumika, kibri kingezidi, Mbowe ndio angekuwa kama kisha kuwa Rais tayari, hivi ni kiongozi wa upinzani tu, alishaanza kuifanyia kibri mahakama.

  Maswali ya kujiuliza ni kwanini wenzake kwenye kesi hiyo hiyo hawakufanya kibri na walitii amri ya mahakama? Alikuwa ana beep? kama ana beep basi dola imempigia na imemuonesha kuwa dola ni dola na upinzani ni upinzani.

  Bwan Maggid, hilo la Mbowe na cdm kwa ujumla kujitakia umaarufu wala lisikutie shaka sana, kwani, cdm wameonyesha "foul strategies" za kujitafutia umaarufu kila kukicha, tumeona wakijitafutia umaarufu mpaka wa kwenye maiti huko Tarime na kujifanya wao wana hisia saaana, hata kwa vibaka. Tumeona walivyomtanguliza gf (natumia GF kwani nikitumia neno stahiki "hawara" wengi hawatoridhika ingawa ndio ukweli) wake Slaa kule Arusha na kumpiga picha ilhali kajitapakaza tomato sauce. Tumeona wakijitafutia umaarufu kwa kutangaza maandamano kila kukicha. Kwa hayo, usiskitike sana kwa Mbowe kutumia tena "strategy" chafu kwa kujitafutia umaarufu.

  Ukweli utabaki kuwa ukweli, mahakama ni mahakama, Rais ni Rais na Bunge ni Bunge. Hii ni mihimili mitatu ambayo kila mmoja unatakiwa uheshimu maamuzi ya mwenzake na kanuni zake. Wala kuwa Mwenyekiti wa chama cha upinzani kusimtie kibri Mbowe na kuona kuwa dola litaogopa kutimiza wajibu wake inapobidi.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kama kuna mtu hajui mnafki yukoje basi hasipate tabu huyu ndio mnafki namba moja, yeye anadhani hili ni jukwaa la mashoga.


  [​IMG] JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 9th May 2011
  Posts : 795
  Thanks 130 Thanked 57 Times in 48 Posts

  Rep Power : 22


  [​IMG] Re: Mbunge wa cuf magdalena sakaya na viongozi waandamizi wa cuf wanyimwa dhamana mara ya pili.

  Huyo hakimu inafaa achunguzwe na au mtoa habari kama ni habari za kweli au walishindwa masharti mengine ya dhamana. Si vyema kuihusisha mahakama na CCM. Kama hakimu ana mapungufu basi huyo hakimu hatoungwa mkono na CCM. Na kama mwandishi wa hii habari ndio ana mapungufu nae pia achunguzwe.
   
 18. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rais sio muhimili rudi tena shule. Nimefurahi kusikia Kibri badala ya kiburi. Nimekutambua ni wa kutoka wapi.
  Sitashangazwa tena na post zako.
  Usiku mwema.
   
 19. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sema Faiza, sema!
  Unawachambua kama karanga, na wasukuma mikokoteni wanakugwaya!!!!
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kitu pekee nilichokiona kwenye tafsiri yaki Mjengwa ni kuwa wewe ni mwandishi mzuri sana katika kubalance story, ila weakness yako ni kutumia hypothesis badala ya conclusion. Kila siku jaribu kutafuta conclusion kwanza ili kuandika kitu kilichosahihi, yaani na wewe umeingia katika mtego wa propaganda katika uandishi wako.

  Otherwise hypothetically umejaribu kutengeneza win-lose situation na hii itaendeleza kilekile yaani nani ni zaidi.
   
Loading...