Kukaa na kinyongo ni kuendelea kujitesa

Kukaa na kinyongo ni kuendelea kujitesa

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
KUKAA NA KINYONGO NI KUENDELEA KUJITESA TU

Ni kwamba unakosa nafasi ya kufuatilia mambo mengine muhimu kwako.Unaweza kujiaminisha kwamba kinyongo ulichomwekea mtu unastahili kabisa.

Alininyanyasa sana nilipokuwa mdogo, alinitesa sana katika mapenzi/ndoa, alinisababishia hasara kubwa kwenye biashara yangu, alisababisha kifo cha mtu muhimu sana kwangu na sababu nyingine nyingi unazojipa kwamba kuweka kinyongo kwa mtu ni haki yako kabisa.

Lakini hebu niambie, kwa kuwa na kinyongo hiko kumekusaidia nini mpaka sasa? Je alichokufanyia mtu huyo kipindi hiko kimebadilika?

Kukaa na kinyongo ni kuendelea kujitesa, kujinyima nafasi ya kufanya mambo ya msingi kwako na yatakayokupeleka kwenye mafanikio na kinyongo hiko hakikusaidii wewe wala yule ambaye umemwekea.
 
Kabisa mimi nilikaa na ki nyongo for more than three years nilibakia kupata magonjwa Ya ajabu. I am learning how to Let go...
 
Kuna kinyongo na kumbukumbu!Kinyongo ni ninj na kumbukumbu ni nini?
Let say mtu alikutesa utotoni,ina maana ukikumbuka yale mateso ndo kinyongo?unaweza kupotezea ule ujinga ila huwez kusahau,uloyaandika hapa sio vinyongo ni kumbukumbu ya mambo ambayo mtu au watu walikufanyia na hutayasahau.
Kinyongo si hayo uloyabainisha
 
Kuna kinyongo na kumbukumbu!Kinyongo ni ninj na kumbukumbu ni nini?
Let say mtu alikutesa utotoni,ina maana ukikumbuka yale mateso ndo kinyongo?unaweza kupotezea ule ujinga ila huwez kusahau,uloyaandika hapa sio vinyongo ni kumbukumbu ya mambo ambayo mtu au watu walikufanyia na hutayasahau.
Kinyongo si hayo uloyabainisha
Kinyongo ni kuTokusamehe jambo pale unapokumbuka unakua na uchungu na kuwaza mabaya.. kumbukumbu ni fikra ya mambo yaliotokea. Yaweza kuwa baya au zuri.
 
Kukaa na kinyongo ni sawa na kunywa sumu ya panya alafu utegemee mtu mwingine afe.
 
Ndiyo! Kuna kumbukumbu na kinyongo ni tofauti. Wenye vinyongo mara nyingi hulipiza visasi. Bora usamehe usahau maisha yaendelee, lakini wenye moyo wa hivyo ni wachache.
 
Back
Top Bottom