Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,253
- 144,322
Marhabaan wana JF,
Natumaini nyote mu amul 'an takunuu jamieaan bikhayr.
Sasa bana kuna suala nilikutana nalo mwishoni mwa juma lililopita.
Mimi na bi mdogo [Kisura] tuliamua kutoka kwenda kula sehemu moja hivi. Au niseme alinitoa kwenda kunipa ofa ya mlo wa jioni.
Wakati tunatoka, kwa nje karibu na mlango wa kuingilia tukakutana mdada aliyekuwa ametoka kuagana na jamaa mmoja hivi.
Basi tukajikuta tumeanzisha mazungumzo madogo. Katika mazungumzo hayo ndo akafunguka kwamba alikuwepo hapo mgahawani kwenye mtoko wa kwanza na huyo jamaa.
Akasema jamaa ni mtu mzuri na mwenye mafanikio na kwamba ameufurahia huo mtoko.
Nami kwa nia njema kabisa nikamwuliza 'vipi, kwa hiyo kutakuwepo na mtoko wa pili?' Akacheka kidogo halafu akajibu kwa kusita sita na akasema 'hadhani'.
Nikashangaa kidogo, hivyo ikabidi nimwulize swali jingine kuwa kulikoni kusiwepo na mtoko wa pili wakati huu wa kwanza umesema umeenda vizuri tu na kwamba jamaa ni mtu poa.
Akanijibu na kusema kuwa licha ya kwamba jamaa ni mtu poa na mwenye mafanikio maishani, bado hadhani kwamba jamaa ndo anayemfaa.
Akasema kuwa mara nyingi huwa anajua tu mara moja kama huyu jamaa ndiye ama siye.
Nikabaki na maswali lukuki: hivi kweli mtu unawezaje kujua kwa uhakika kuwa huyu ndiye na huyu siye kutokana na mtoko mmoja tu tena ambao umeuelezea kuwa umeenda vizuri na umesema kuwa jamaa ni mtu poa.
Huko siyo kuhitimisha jambo kwa kutumia kielelezo kimoja na kisichotosha kweli?
Kwa nini usimpe mtu hata fursa mbili au tatu kabla hujafikia hilo hitimisho?
Na mara kadhaa nimeshasikia hivyo kutoka kwa wadada. Ni kweli?
Karibuni kwenye mjadala.
Wenu katika ujenzi wa taifa,
Alhaj Ngabu wa Kibadiru.