Kujizuia na 'personality change' ........

Kujizuia na 'personality change' ........

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,675
Maisha tunayoishi yana Pressure na Stress tele siku hizi

ni ngumu kukuta watu wana 'peace of mind'
watu wengi ama wanakumbana na changamoto mbalimbali za maisha
au wamezipitia na zimeacha alama mioyoni mwao

hizi alama au makovu ya maisha kwenye mambo mbalimbali
mfano
talaka
kufukuzwa kazi
kufilisika
kukimbiwa na mke/mume
kufiwa na mke/mume/watoto/wazazi
kupata ajali
magonjwa na kadhalika wa kadhalika hupelekea baadhi ya watu wakabadilika kabisa
kiasi kwamba akawa mtu tofauti na uliyemzoea

Wengine walizaliwa wacheshi na tabasamu kutwa unakutana nao after years wana sura za huzuni
na kisirani au hasira kiasi hadi unawamiss ,una miss their old personality.....

Inawezekana hata sisi bila kujijua tunabadilika na kupelekea wapendwa wetu watu miss
ingawa tuko nao au ingawa tuko available..lakini kutokana na life experiences mtu anabadilika
hadi unashindwa ku relate nae kabisa.....

Swali hapa je unajizuia vipi na hali hiii?
au unapokutana na mpendwa wako katika hali hii unafanyaje?

Tunajizuia vipi kutoleta 'matatizo tunayokumbana nayo' kutubadilisha haiba(personality) zetu ?
unaweza kugundua kama umebadilika?na kama watu wako wa karibu they miss the old you?
umewahi kummis mtu wakati yupo.ila una miss his or her old personality?

note:wataalamu wa lugha wanaweza saidia ninachojaribu kukisema
haiba,tabia,personality na kadhalika
 
The Boss may be sijui nitaenda nje sana ila haya yapo sana yaani kupoteza ule uhalisia wako haiba yako au ucheshi wako yaani kwa kifupi wewe unakuwa umepotea haupo kama ulivyokuwa. Umebaki mtu tofauti sana
Na hizi ni kutokana na mambo ambayo tunakutana nayo kwenye maisha na stress za maisha
 
Last edited by a moderator:
hutokea na siyo rahisi kulizuia ... huanza kama acute response to frustration/stress na inapaswa kuresolve baada ya muda .....ila kama itajijenga na kuwa tabia yako ndiyo things zinapoanza kufall apart na mwisho wa siku unajikuta mwenyewe kwenye maisha yako.
 
naamini mawazo yako kweli maisha haya mimi mama yangu alinifia mikononi nikiwa na 15yrs mpaka leo imenisababishi kila msiba naona ni kawaida tu wala silii tena maana naona its not worth that muchjinsi nilivoumia naishia kukodoa macho tu wala silii tena kama zamani so watu walionizowea waweza sema lol mwanamke anaroho mbaya huyu hata kutoa chozzziiiii.kumbe that scenario change my personality

Unayoyasema ni kweli kabisa boss. Uvumilivu wa kufikwa na mambo makubwa kama hayo uliyoyataja unatofautiana kati ya mtu na mtu. Kwa mfano wazazi wengine wanapofiwa na mtoto kifo kile husababisha stress kubwa ndani ya ndoa yao na wengine kufikia hata ndoa kuvunjika lakini kwa wazazi wengine tukio hili kubwa ndio linaweza kuwafanya wazidi kuwa karibu ndani ya ndoa yao.

Kama unajifahamu vyema basi utajigundua tu kwamba kuna hitilafu fulani katika mienendo yako ya kila siku au watu walio karibu na mhusika wanaweza kabisa kuyaona mabadiliko ya kitabia na kama wanafahamu yaliyomkuta wanaweza kujaribu kumsaidia na wale ambao hawajui ni yepi yaliyomkuta kuuliza kulikoni mbona siu hizi umekuwa tofauti hivi na jinsi tulivyokuzoea!?

Kama unakutana na mpendwa ukiwa katika stress ni vizuri kufunguka tu na kumwambia ukweli wa kile kinachokusibu na kumhakikishia kwamba siku za usoni hali itakuwa nzuri. Kuwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu pia husaidia sana kumrudisha yule aliyeathirika na mikanganyiko ya kimaisha ili aweze kurudi haraka katika hali yake ya kawaida kabla ya kukutwa na mikanganyiko hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Great topic,haya mambo yapo kabisa mkuu ngoja tusubiri busara za wengine
 
Nasikitika hujatuwekea music kusindikiza maneno yako
 
Last edited by a moderator:
ushawahi kujimiss mwenywe!
ILE LIKE YU MISS THE OLD YU!
inaumiza sana!
unajua tabia au personality ya mtu inajengwa na vitu vingi!
wakati mwingine unabadilika pengine hata bila mwenywe kujijua na unafiki tulio nao miongoni mwetu hakuna anayekwambia uv changed au hata ukiambiwa u pretend kuwa uko sawa au unamanage!
hii nayo ni shida nyingine
well maisha wakati mwingine yanakuwa sio fair kwa baadhi ya maisha ya watu,matokeo yake mtu haoni sababu ya kuwa fair kwa wengine!like if i miss this na nyie will miss this!

-wakati mwingine kama personality ya mwanzo ilichangia kufanya upate matatizo mahala fulani likely huwezi kuwa yule lazima utabadilika!

-wakati mwingine hujui hata personality yako ni ipi so ukijikuta kwenye mazingira ya upepo wa kimaisha wowote tu unajiadaptisha personality ya mtu

-wakati mwingine unahisi kuwa na personalty flani kunakuepusha na maumivu ya moyo so i rather be this way ili moyo wangu uwe mbali kufikika kiasi kila kitu kwako nia sawa!ushakutana na mtu yeye msiba mkavu harusi mkavu,sijui nimeeleweka?(yani hataka kuruhusu akili yake itoe na kupeleka taarifa yoyote kwenye moyo wake kuwa jambo hili ni zuri smile,na hili ni baya nuna)

-wakati mwingine personality yako halisi inakucost pakubwa!unaona nabaki kuwa wakuchonga,nikicheka simaanishi nikilia simaanishi.

MY TAKE
iwe mvua liwe jua!
maisha yako yana tafsiri sahihi ukiamua kuyapa tafsiri sahihi
wengi wetu hatukubali kuwa pamoja na kupenda sana pamoja na kuwa na busara sana kuna muda one needs to spoil her /his one self!tunajisahau sana!mno!
kazi fine.biashara fine,talaka fine,kufiwa fine ,kufilisika fine yote hayo ni changamoto tu za maisha!na pengine kwa kujua kuwa utayamudu na ukayamaliza ukiwa mshindi ndo mana Mungu alikuletea wewe!
kwa hiyo si nyakati zote tunapaswa kufanya yote ili wote wafurahi au waumie,wakati fulani tunapaswa kufanya kitu fulani ili nafsi zetu ziwe na amani!
 
Ninakubali mkuu...

Mfano nikikutana na msichana anadai..'siku hizi mapenzi hamna, imebaki kudanganyana tu..' huwa najua tayari ni kovu la kudumu hilo..watu walishauponda moyo (mbaya sana tuache!!)..

Mambo kama kufukuzwa kazi, kuanzisha biashara ikafeli, kuondokewa na mtu wako wa karibu n.k..nadhani suluhisho lake ni kuchukua muda na kutafakari, kujifunza ku-relax, meditation, kusocialize zaidi na kusali (if you believe)...nakumbuka hii serenity prayer;

God grant me the serenity to accept the things I can not change,
the courage to change the things I can,
and the wisdom to know the difference.

Ni vizuri kujifunza ku-let go na kusahau maumivu ya maisha yaliyopita..la sivyo ni chanzo cha maumivu kwa walio karibu nawe, mpenzi wako ajaye, ubora wa utendaji wako wa kazi, furaha yako ya kila siku, afya yako, urefu wa maisha yako na kadhalika....
 
niliwah kujimiss the real me ilikuwa ngumu kurudi hali yangu ya kawaida thanks to god im better now
 
Mandela ndio katika hilo kundi la watu waliojaliwa shock absorbers za hali ya juu. Pamoja na kukutwa na matatizo chungu nzima kwa miaka mingi yeye na familia yake lakini bado alipopata nafasi hakuamua kulipiza kisasi au kuendelea kuhuzunika bali kuwasamehe wote waliomtesa kwa miaka chungu nzima, hili la kusamehe lilimletea furaha kubwa sana maishani mwake na heshima kubwa kila kona ya dunia hii.

The Boss, hivi Mandela aliwezaje kukaa 27 years in custod halafu mind yake was sharp with no corruption? I think that comes with what we feed our subconcious mind...mostly by our self talks...Garbage in Garbage Out
 
Very true Mkuu Bujibuji :yo::yo::yo:

The Boss Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!
 
Last edited by a moderator:
Bila Neema ya Msaada huwezi kujizuia kuwa mtu mwingine hasa baada ya kupitiwa magumu tuliyoyapitia. Namjua binti mmoja ana cancer na yupo l think Mwaka 4 St. Joseph University of Engeenering yaani mwenyewe nina muadmire sana pamoja na mama yake ambaye sio tu alikimbiwa na mumewe for his secretary lkn pia naye ni mbovu na watoto wake ni wagonjwa (mmoja diabetic na ni form 3 tu). Lkn Yule mama alivyo mstari wa mbele kusahau matatizo yake na kuhangaika na ya wengine.

Hivyo bila some sort of Tumaini ambalo kwa believers tunasema death is a commar and not a fullstop inakuwa ngumu kutokuwa chizi pindi upitiapo magumu.
 
Maisha tunayoishi yana Pressure na Stress tele siku hizi ni ngumu kukuta watu wana 'peace of mind'
mfano
talaka
kufukuzwa kazi
kufilisika
kukimbiwa na mke/mume
kufiwa na mke/mume/watoto/wazazi
kupata ajali
magonjwa
na kadhalika wa kadhalika
Just imagine alafu yote yatokee katika wakati mmoja au yanapishana wiki hii then wiki inayokuja linaibuka lingine!
 
Maisha tunayoishi yana Pressure na Stress tele siku hizi

ni ngumu kukuta watu wana 'peace of mind'
watu wengi ama wanakumbana na changamoto mbalimbali za maisha
au wamezipitia na zimeacha alama mioyoni mwao

hizi alama au makovu ya maisha kwenye mambo mbalimbali
mfano
talaka
kufukuzwa kazi
kufilisika
kukimbiwa na mke/mume
kufiwa na mke/mume/watoto/wazazi
kupata ajali
magonjwa na kadhalika wa kadhalika hupelekea baadhi ya watu wakabadilika kabisa
kiasi kwamba akawa mtu tofauti na uliyemzoea

Wengine walizaliwa wacheshi na tabasamu kutwa unakutana nao after years wana sura za huzuni
na kisirani au hasira kiasi hadi unawamiss ,una miss their old personality.....

Inawezekana hata sisi bila kujijua tunabadilika na kupelekea wapendwa wetu watu miss
ingawa tuko nao au ingawa tuko available..lakini kutokana na life experiences mtu anabadilika
hadi unashindwa ku relate nae kabisa.....

Swali hapa je unajizuia vipi na hali hiii?
au unapokutana na mpendwa wako katika hali hii unafanyaje?

Tunajizuia vipi kutoleta 'matatizo tunayokumbana nayo' kutubadilisha haiba(personality) zetu ?
unaweza kugundua kama umebadilika?na kama watu wako wa karibu they miss the old you?
umewahi kummis mtu wakati yupo.ila una miss his or her old personality?

note:wataalamu wa lugha wanaweza saidia ninachojaribu kukisema
haiba,tabia,personality na kadhalika

Napenda nijikite kwenye eneo la Mungu na dini katika suala hili.
PERSONALITY CHANGE haiepukiki in most cases.Na ukitaka kujua how much people are suffering nenda makanisani na ndipo utakapojua people are really desperate.Wakati mwingine huwa naangalia vipindi vya Emanuel Tv.Watu wamechanganyikiwa na matatizo kiasi kwamba wanamfanya TB Joshua kama ndio Mungu sasa.
Wengi wanakimbilia KUOKOKA..na japo lengo kubwa la kuokoka ni kumpenda Mungu lakn inakuwa kinyume..Matokeo yake kwa sababu wanaenda huko bila kuamua kweli kweli basi wanakumbana na kadhia au hawapati kile wanahitaji na matokeo yake wanaacha huko Kuokoka na wanakuwa na hali mbaya zaidi.Kwa wale wasoma bible ni kama wana Israel walipotoka utumwani Misri na walitegemea mambo yatakuwa bambam.Lakn wakaenda kukutana na jangwa na shida lukuki na walitamani warudi tena utumwani..
Hata hivyo Hii njia ya kumwamini Mungu ni nzuri sana kuwasaidia waliokata tamaa na kuwafanya wazuie personality change kama tu mtu akiwa juhudi binafsi na uvumilivu.Lakn ni wachache waliofanikiwa
 
The Boss may be sijui nitaenda nje sana ila haya yapo sana yaani kupoteza ule uhalisia wako haiba yako au ucheshi wako yaani kwa kifupi wewe unakuwa umepotea haupo kama ulivyokuwa. Umebaki mtu tofauti sana
Na hizi ni kutokana na mambo ambayo tunakutana nayo kwenye maisha na stress za maisha

Mkuu hujatoka nje ya mada..
maisha yanaweza kukubadili hadi we mwenyewe ukashangaa
 
Back
Top Bottom