Kujivua kwa magamba,sio kwamba sina sumu,

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
La mgambo limelia, kila mtu kasikia,
Magamba nayatupia,kujiweka asilia,
Wengi walinililia,hamsini tanzania,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Sio kwamba sina sumu,nilipovua magamba,
Mafweza yote haramu,ufisadi wa makamba,
Atai face hukumu,kutufanya si manamba,
Kujivua kwa magamba,sio kwamba sina sumu,

Walianza na Lowasa,la macho changa jamani,
Mdanganyika nakwasa,si kafara ni ilani,
Wa Taifa aliasa,hakuzaliwa chamani,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Balali naye kauliwa,kaburi liko hewani,
Kwa mandishi kazikwa,kihalali ni kapuni,
Mbongo hakualikwa,ngawa yuko marekani,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Vijisenti vililiwa, Uswizi vimetulizwa,
Chenge ni mshitakiwa, lakini anashangiliwa,
Mkulu kadavuliwa,kitu hapa tunafichwa,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Richmond ikaletwa, Rostam ju zaidi,
Kwenye rada ni mtajwa,alikuwa ka kuwadi,
Hazina mfukoni mwa,ikulu kashaifaidi,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Wametoa eti baba, mtoto sasa apanda,
Wamevua lipi gamba,zao ndo propaganda,
Januari ndiye makamba,nec kamwe hatoponda,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Sumu zote si anazo, upuuzi usoisha,
Watuona hamnazo,danganyika tusobisha,
Wao wote si wanazo,sumu zao kututisha,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,

Hapa ngoja niyatue,maisha yanilemea,
Karibu yakhe nitue,sisiemu makwelea,
Wako radhi wakuue,Chengeni chupu ponea,
Kujivua kwa magamba, sio kwamba sina sumu,
 
Back
Top Bottom