Kujitegemea mwenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujitegemea mwenyewe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Aug 18, 2010.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  Habari za leo wanajamvi?

  Jana jioni nimekutana na kioja mtaani kuna dada mmoja yuko single amerudi nyumbani saa 6 usiku (anakaa kwa wazazi) wakagoma kumfungulia geti (alikuwa na gari yake) na baadae baada ya kupiga honi sana mzee wake akatoka na kumwambia inabidi ufuate masharti ya nyumba yangu, nimesema simfungulii mtu akirudi zaidi ya saa 4 usiku kwa hiyo nenda huko huko ulikochelewa. Yule dada ni mfanyakazi wa benki kama cashier na anadai alichelewa kwa kuwa alishindwa kubalance hesabu na alikuwa na short kubwa sana hivyo alichanganikiwa na alisahau hata kuwajujulisha kwao.

  Sisi tukamshauri ahame kwa baba yake akajitegemee lakini akadai baba yake hataki kumruhusu ahame mpaka atakapo olewa ndio aende kwa mmewe lakini sio kupanga wakati baba yake ana nyumba nzuri na kubwa hapa mjini

  Naomba maoni yenu kwenye hili maana lilituacha njia panda

  Je mtoto wa kike anapopata kazi inabidi ahame kwao au asubiri mpk atakapoolewa? (hapa naongelea wanaofanya kazi ndani ya mji mmoja na walipo wazazi) maoni wandugu
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Duuh ngoja nipate lunch kwanza akili ikae fresh:confused2:
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  unakula nn na mie nikale hicho hicho?
   
 4. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani huyo mzee anakosea..sioni ubaya wa binti kuhama kwenda kupanga kwani hapo anaweza kujijenga vizuri na kuwa na ukomavu pindi akipata wa kumuoa..cha msingi ni ajue kujitunza na kuwa na staili nzuri ya maisha coz wengi wakiwa huru hutumia uhuru vibaya lakini sioni ubaya wa kuhama home ukipata kazi...unaweza kutohama na ukawa na tabia mbaya so sioni ugumu wa huyo mzee kumruhusu ahame au la ielezwe kuna sababu gani ya kumkatali...binafsi nafikiri kwa umri wa kuweza kufanya kazi na kuwa na gari ni kuwa unajipanga kimaendeleo..hofu yangu mzee anaweza kuwa mbogo pindi binti akianza kununua TV,friji na kadhalika kwa kisingizio "babako ninavyo so huna haja ya kuwa na vyako" as alivyotoa hoja ya kuwa na nyumba so bintio asihame..
  mi naona hakuna ubaya binti kuhama ila apewe miongozo sahihi kabla hajahama..vinginevyo mshaurini aombe wazee wamweleze baba'ke kuwa ili binti asimsumbue amruhusu kuhama kama alivyogomea kufungua geti basi awe ready kuacha binti akate kitovu vinginevvyo hatakua amekuwa na ataendelea kuwa mtoto tu hata decision zake lazma atapima kwanza mdingi atasemaje which is not right kwa mtu aliemature.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  mhhh!
  Hii kali........... kazi, kuolewa, kufuata masharti ya mzazi......au kuhama nyumbani...
  Hebu nitafakari kwanza kabla ya kujaribu kuchangia.
   
 6. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  kwa kweli alitueleza mengi sana mpaka tulimuonea huruma mengine ya ndani sana mwenyewe hata akienda saloon hivi wanamuandama wanamwambia unatumia hela nyingi kujiremba wakati unaona mboga kwenye fridge zimepungua si bora utumie hiyo hela kununulia nyama watu wale
   
 7. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  :welcome:
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,195
  Trophy Points: 280
  Kimaadili, mtt wa kike hatakiwa kupanga na kuanza maisha akiwa bado hajaolewa.
  Ladba tu ikiwa wazazi wake wanaishi miji tofauti. Lakini kama wanaishi mji moja haipendezi.

  Ndo mana kuna send off na ni kwa wanawake tu.
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :becky::becky::becky:
  Dah we mdada njoo ukae kwangu bureee
   
 10. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo kesi kama ya huyo dada unaingeleaje? mimi niko tofauti kimtazamo na wewe nadhani pale mtu anapoona yuko vizuri kujitegemea basi akajitegemee tu maana kuolewa ni majaliwa si w/wake wote wanaolewa sasa kama asipobahatika kupata mume ina maana atazeekea hapo hapo kwa wazee wake?
   
 11. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  kimbweka vya bure gharama shauri yako:becky::smile-big:
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mhhh KAZI, KUHAMA, KUOLEWA........Mzee hataki mtoto ahame kwake at the same time hataki aachelewe kurudi nyumbani naona dalili za msichana kuacha kazi ili amridhishe mzazi wake
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  tatizo binti ameshakuwa mtu mzima mzee akiona binti kachelewa ana assume watu washamramba kwa hiyo anaweka masharti magumu kama control measures
   
 14. g

  gnasha Member

  #14
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wazazi wanakosea sana, mwisho wa siku huyo msichana anaweza kufanya maamuzi ambayo sio sahihi ilimradi tu atoke hapo kwao mfano kuolewa. Halafu baada ya mwaka au miaka miwili ndoa ikavunjika sababu tu alilazimisha ndoa ili atoke kwao.
   
 15. g

  gnasha Member

  #15
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawezi kuzuia binti asirambwe kesha kuwa mkubwa huyo
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  ili tatiz linawakumba mabinti wengi sana ila tu hawasemi utakuta mtu ana kazi na kipato kizuri wazazi wanakomalia ake nyumbani mpaka aolewe
   
 17. g

  gnasha Member

  #17
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao Wazazi bado wana mawazo ya kizamani kuwa binti hawezi kuishi mwenyewe kabla hajaolewa ataonekana hana nidhamu. Na umri utakapokwenda sana akaamua kuzalia hapo nyumbani watamruhusu? au ndio atapokea kipigo?
   
 18. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo wako interested sana kipato chake na ndio maana hawataki ajitegemee. uwe mwanamke au mwaume kuna muda unafikia unahitaji uwe na uhuru, iwe umeoa/olewa au la!
  na wazazi wengine nao punguwani kweli!! unamwambia binti arudi alikotoka saa 6 usiku!? afu tena unakataa asijitegemee!:confused2:
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wanajua watakosa nini kutokana na kipato chake, yale matunda tunda, mboga nyama, ndizi za kupika anazowaletea akitoka kazini watavikosa:becky:
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  halafu unapopata kazi unakuwa na ndoto fulani unataka kuzitimiza ili kuweka msingi wa maisha wakati wazazi interest zao ni tofauti lakini watataka ufanye kama wanataka wao mara nyingi ili suala la kuishi na wazazi wakati una uwezo wa kujitegemea linaleta ugomvi sana baina ya wazazi na mtoto
   
Loading...