Kujitegemea mwenyewe

Hao Wazazi bado wana mawazo ya kizamani kuwa binti hawezi kuishi mwenyewe kabla hajaolewa ataonekana hana nidhamu. Na umri utakapokwenda sana akaamua kuzalia hapo nyumbani watamruhusu? au ndio atapokea kipigo?
na ndio wanachotakiwa wakisubirie hicho
 
wanao ila bado wako vyuoni huyo ndio first born na ameanza kazi kama mwaka na nusu sasa
 
Kama ananyimwa kutoka/kuchelewa nyumbani, na kama ananyimwa hata kwenda saluni....atampataje mme?? au hawataki aolewe (sababu za kiuchumi) labda....
Ila ukubwa wa huyo dada anaujenga mwenyewe...anawaachia wazazi wake wamuamulie uwezo wake wa kumudu maisha?? Nadhani yeye ndo anafanya wazazi wake wamwone bado mdogo!
 
kwa kweli alitueleza mengi sana mpaka tulimuonea huruma mengine ya ndani sana mwenyewe hata akienda saloon hivi wanamuandama wanamwambia unatumia hela nyingi kujiremba wakati unaona mboga kwenye fridge zimepungua si bora utumie hiyo hela kununulia nyama watu wale
kama imefikia hatua anasimangwa namna hii noway asepe tu.

nyumbani ni kutamu wala huwezi lazimishwa kukaa hasa kwa mtoto wa kike,ila kwa story hii inaonekana wazazi wana maslahi binafsi na binti yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom