Kujinyonga kwahitaji ujasiri!

Kujinyonga kwahitaji ujasiri!

Hmaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
346
Reaction score
86
Kuna mzee fulani mwenyeji wa Mbeya alikuwa anajitahidi sana kuwahusia mabinti zake wawe na maadili mema na kila mara alikuwa akijisifia kwa wenzake kuwa binti zake si kama wa wenzake: si malaya, si walevi, hawavai vibaya, anawasomesha nk. Siku moja alipigwa na butwaa baada ya kumwona mwanaye amefukuzwa shule sababu ya mimba. Mzee kwa namna alivyokuwa akijigamba kwa wenzie aliona ni pigo kubwa kwake. Akaamua eti ajinyonge afe. Akatoka nyumbani kimyakimya na kamba yake hadi polini, akaifunga kisha akajitundika na kujiachia ili aning'inie kwa madumuni hayo. Kamba ikakaza kweli na akaanza kuhangaika kana kwamba anataka kujiokoa. Ghafla akatoke mchoma mkaa; alipoona mzee anahangaika akawahi kuifungua ile kamba ili amuokoe. Alipofanikiwa kufanya hivyo akamuuliza kwa nini aliamua kufanya vile na mzee akamjibu kwa kifupi "aibu kijijini mwanangu". Kwa vile yule mzee alielewa yote kuhusu mzee yule akamweleza "kama lengo ni hilo basi una sababu za msingi chukua kamba na endelea na zoezi lako maana utasakamwa sana kijijini". Akiwa anategemea kutokea msiba kijijni, jamaa yule akashangaa kumkuta mzee akipata pombe na wazee wenzake tena yeye ndo anawanunulia wenzie huku akishukuru kwa kuepuka kifo siku hiyo bila kueleza kisa. Jamaa akaishia kucheka na kuamini kumbe kujinyonga kazi.
 
Ile kitu haikuwa imeshamtoka?Angekuwa mtani wangu pale IR ingekuwa kitu ndogo sana hii..
 
Angekuwa Mnyalu wala isingekuwa kazi ngumu!!
 
Mimi, Wanyalu si wasema maana Wengine ni Wakwe zangu na Shemeji zangu.
 
Kuna jamaa naye alipata hasira akataka kujinyonga porini, kwa bahati akatokea simba, asitoke mbio nini, na mayowe juu... "Jaamaaniii siiimbaaa nafwaaaa ukuuu....!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom