Kujiepusha na HIV

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,033
Hiki ni kisa cha kweli hebu soma..

Mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya mawasiliano alikaribishwa kutoa
speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu
kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa.
Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo;

"Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini . Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa wingi
na gharama yake si kubwa.Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kupatikana kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.



Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina hatari kubwa mno.

Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu angalau ya ku beep, lakini hii nayo ni hatari,kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua kupiga kabisa.

Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu zitamaliza chaji, hii si kweli. Hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana. Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double skrini.. Hizo ni mbwembwe tu. Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya,usidanganyike.

Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana kwani simu ukitumia peke
yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi."
 
Administrator mbona hii topic ya miaka nenda rudi? Well ingawa issue yenyewe ni ya kukumbushana mara kwa mara.
 
miaka hiyo wengine tulikuwa hatujazaliwa mkuu, sio mbaya kukumbushana
Labda naye kaiona leo!!kwani siinategemea umeikutia wapi??Kama alikuwa akiishi mjini na nistory ya kijijini!!....lol!:becky::smile-big:
 
Back
Top Bottom