Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,280


Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,
 
Cha muhimu fanya kile kitachokupendeza kulingana na uwezo wako.

Yaani maskini ajenge nyumba ya vyumba viwili na Bakhresa nae ajenge hivyo hivyo si matumizi mabaya ya utajiri?

Mola akikiruzuku mali basi pamoja na mambo mengine ishi sehemu nzuri, kula vizuri, vaa vizuri, tembelea gari zuri nk
(usisahau kuwasaidia wasiojiweza)
 
Mleta mada umezungumza ukweli kwa wenye mtazamo kama wako. Sisi wengine tuna mtazamo tofauti. Tokea tumeanza kujitambua malengo yetu ni kupambana ili tuje kujenga nyumba ya ghorofa moja na vyumba 6 vya kulala. Tusipoweza kulitimiza hili then we are a failure on this beautiful earth regardless of other factors.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…