Kujamba (kutoa ushuzi) kuna faida kiafya?

Evelyn Salt na Miss Chagga wamemaliza kila kitu. majibu yao yamenikumbusha wakati wa kukanyaga dongo la kujengea nyumba. Ukitaka kujua dongo liko tayari ukizamisha mguu na kuchomoa gafla utasikia sauti kama kijambo. Sasa kama kuna watoto karibu utasikia wakizomea "umejamba"
 
ni hewa na inasababisho na kuacha distance kubwa ktk kupampu na unaachajee ni ile chomekaa chomoaa yotee unaingiza tenaa unatoa yoote na pale kati men umejibana so kale kahewa kanakokuzunguka unakasukumia huku kwa push up yko sasa by z time umeacha mwanya ktk ile chomua yote ndio hivyo puuu pruuu pruuu na kikopo utakuwa ushakitumia saana maana mwazo kwa kukianza tu hakiwi hivyooo hapo umemminyia mtu 20mn nakuendelea lzm kijae hewa na hiyo hewa haina pa kwenda lzm irudi nje kupitia ilipoingilia. Kama umeshawahi zibua sink la vyombo lililozma kujaa sasa ukifakiwa kuzbua vzr hewa inaingia ikiingia sikilzia nao mlio wake
 
Huu sio ugonjwa....Wakati wa kufika kileleni mwili hutumia nguvu kubwa kusukuma ute wa uume au uke...hiyo kasi hupelekea hewa kupita katika sehemu mbali mbali mfano...mdomoni....kwenye njia ya haja kubwa etc. ndio maana baada ya kufika kileleni watu huwa wana hema sana. sasa ndio maana wengine hupitaisha hewa kwenye haja kubwa kulingana na nguvu iliyo ambatana na mshindo wa kileleni
 
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu, lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.

1.Kujamba ni nini hasa?

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa, ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria. Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans, ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya. Kujamba huambatana na sauti, hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa. Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio usababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama soda, maharage, kabichi na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6, anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde. Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba, hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako.
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya. Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara. Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini kwao husalimiana kwa kujamba na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

7. Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu. Methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8. Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming". Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama na hiyo huzalisha gesi ya methane.

9.Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini
Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia, hii huambatana na milio ya kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA MUDA JAMBA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom