Kuitwa Kituo cha Polisi

goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
8,855
12,984
Wakuu kwema,

Nikiwa naendelea na harakati zangu za hapa na pale ghafla simu iliita, nikapokea sauti ya mwanaume basi alivyo jitambulisha na kunitaarifu kuwa nifike kituo kikuu cha polisi leo bila kukosa.

Hapa najiuliza kuna shida gani hadi kuitwa huko, sina rekodi yoyote ya kiuhalifu wala sina mdai anaenidai, nawaza sana nakosa majibu.

Najua huku kunamaadvocate, naomba ushauri wao ili kusudi wasije niweka rumande mnk kwani nini wanipigie siku kama ya leo kama siyo wana lengo baya.

Nawasilisha
 
1. Nenda na watu angalau wawili. If possible wawe na barua za kukudhamini.
2. Simu iwe na vocha. Mitandao yote angalau dakika 50.
3. Uwe na angalau laki 1 au 2 cash.
4. Kama una rafiki au jamaa mwanasheria nenda nae.
 
1. Nenda na watu angalau wawili. If possible wawe na barua za kukudhamini.
2. Simu iwe na vocha. Mitandao yote angalau dakika 50.
3. Uwe na angalau laki 1 au 2 cash.
4. Kama una rafiki au jamaa mwanasheria nenda nae.
Hivi watu ambao itatakiwa wamdhamini si lazima wawe watumishi wa umma au hata mtu yeyote??
 
Mkuu utatapeliwa...km hajajitambulisha na kukuambia sababu za wito usiende...mimi km mwezi hivi umepita walinipigia simu akinitaka nifike kituo cha Police Chang'ombe ila kila nikimuuliza Jina, Cheo au Dhumuni la wito anakua mkali na kunipiga biti ooho km hutaki tukufuate...nikawaambia njooni tu haina shida nipo Msamvu Morogoro...hawajawahi nipigia tena.
 
Siku zote siokei simu nisiyoijua. Kama mtu simjui ataniambia Nini?

Dah.. unapokea tu mzee. Sema usiwe wa kwanza kujitambulisha kabla ya mpigaji. Hii itakusaidia maana hizi simu za siku hizi zinaisha chaji mapema sasa anaweza kuwa mtu wako wa karibu labda simu imezima sasa aka-adjust simu kwa mtu akakupigia. Au connection tu zozote huwezi jua La msingi unapokea na kusubiri aliepiga ajitambulishe na aseme dhumuni la kukupigia, ukiona inafaa sasa ndio mnaendeleza mazungumzo. Hapo ni technique tu ya kumzubaisha katika maongezi hadi afunguke.
 
Back
Top Bottom