Kuishi na mwanamke yahitaji uvumilivu sana

Kuishi na mwanamke yahitaji uvumilivu sana

Jenseny

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
1,742
Reaction score
1,743
Sijaoa naishi na mwanamke ambaye japo anatabia zinazonikera najitahidi kuvumilia tabia nisizozipenda ni kama hizi;

Ubanaji wa matumizi anajibana kama anajenga lakini sijaona cha maana anachonunua au anachowekeza.

Msafi kupitiliza yaani ukitoka kazini kabla hujaingia anakuambia FUTA VIATU VYAKO Na uoshe miguuu kabla hujaingia (kama umevaa sandals)

Anamfokea sana dada (mfanyakazi wa nyumbani) yaani hata kama glass hajaiweka sehemu yake atapiga kelele masaa mawili.

Anaweza kukuamsha kitandani ili atandike kitanda anaboa hadi natamani nimtimue nilete nyumba ndogo ila nikiwaza mtoto wangu mdogo napata shida kidogo.

Wote tunafanya kazi ila nampa hela ya matumizi kwa kila kitu anachoniambia na kuniandikia kwa mwezi ila bado anataka kujua hela yangu iliyobaki imeenda wapi (sisi ni wafanyakazi serikalini so anajua scale ya mshahara wangu )

Juzi niliishiwa na nilitaka kununua kitu cha muhimu kwa ajili ya maisha yetu nilipungukiwa na laki 2 tu akanambia hana hela wakati last transaction yake (aliniagizia nimtolee hela alikuwa na mill 2 na laki 4.

Nilishamwambia akanambia atajirekebisha ila hajajirekebisha ndo anazidisha.

NB; BADO SIJAMUOA NIENDELEE NA MCHAKATO WA KUOA AU NIACHE?
 
Biblia inasema uishi nao kwa akili, kwa sababu kuna kaz ya ziada kuwaelewa
1473959731446.jpg
 
Mwenye nyumba unaambiwa kanawe miguu,shuka kitandani nitandike[emoji32]
 
Pole sana unang'ang'ania nini sehemu kama hio!!?? Mtu ambae unamwambia hasikii wanini??
 
asanteni wote kwa ushauri wenu
 
Pole sana. Watu wengi huwa tunakosea sana pind tunapotaka kuoa.
Ukikosea kuoa unaharibu maisha yako yote na huwezi kuwa na furaha hata kidogo. Na ukumbuke si kila mwanamke anafaa kuoa.
mwanamke asiyekuonea huruma huyo hafai hata kidogo.
Ndugu yangu km anakufanyia hivi ukiwa mzima, je, siku umesimamishwa au umefukuzwa kazi ataweza kukusaidia?
Au unaumwa taabani ataweza kukusaidia. Hebu tafakari kwa kina mr.
All in all ww ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho. Jaribu kuongea naye tena na tena. Ukiona habadiriki. Ww ndiyo mweny maamuzi yako.
Kumbuka wanawake ni wabinafsi sana, kuoa mwanamke mweny kazi haimaniishi umepunguziwa mzigo. Ni wanawake wachache sana kweny kundi la wanawake 100 ni 2 wanaojitambua.
Ndiyo maana usije kushangaa mtu anadegree anaoa wa darasa la 7. Kwa sbb hata akioa mweny degree mwenye kazi mshahara wa mwanamke unaweza usiguse na usiujue kbsa.
Pole sana
 
Usioe best utajuta baadaee huyo huwa namuita "MCHWA"
atakusumbuwa sana kwano kuzaa Nae ndo nini?
Piga chin then tafuta mwingine ambaye anaMit vigezo vyako unavyovitaka Failure to do that you will Regret your whole life starting from your house upto your Closely Relatives
 
Acha tu....

Ukiona mtu amekua na mwanamke mrembo over 3 years na akafanikiwa kumpeleka pale alter na kufunga nae ndoa muheshimu sana huyo mtu, ni mtihani/challenge kubwa mnooo !!

Plus ukiona mtu miaka hii amedumu kwenye ndoa na huyo mwanamke for more than 5 years plus amekua happy, financially stable nd appreciating each year akiwa na huyo mke wake. Muheshimu sana huyo mtu ni kupitia neema za baraka za Mungu tu .

I kno how its like living wit a stubborn woman.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom