Uzembe ktk hospitali unaua sana. Tuchukue hatua!

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,415
8,816
'Everything happens for a reason'. Ni msemo ambao umekuwa maarufu na kuaminika sana katika maisha yetu wanadamu. Ni msemo ambao mara nyingi umekuwa pacha na msemo huu mwingine wa 'Mipango ya Mungu'.

Ila mimi binafsi, nafikiria kwamba kuna msemo huu 'Everything happens by an act or omission' ambao pia inabidi wanadamu tuuzingatie sana katika maisha yetu ya kila siku.

I have been heartedly touched na uzi huu UZEMBE WA MADAKTAR UMEUA TENA ulioanzishwa na mkuu Urio kimiroI. Mleta uzi alianza kwa maneno haya (namnukuu kwa ufupi):

'' Imefikia wakati Madaktari wetu kushtakiwa wanaposababisha Vifo vya watu kwa Makusudi au uzembe katika matumizi ya Taaluma yao.

Tunahitaji kuleta nidhamu katika matumizi ya Taaluma.Huwa tunapenda kukimbilia ni mapenzi ya Mungu hata kwa watu tuliowaharakishia mauti.

Sostenes Mitti, majira ya Saa kumi na Moja Jioni Jana tarehe 06 February 2016 alijihisi vibaya akaondoka mwenyewe kwenda Hospital ya DDH Bunda kucheck Afya yake. Madaktari walimuattend na kumwekea Drip ya Maji kushusha Pressure, wakaendelea na shughuli zao wakimuacha, mpaka marafiki walipokuja kumuona na kukuta amefariki ndipo wakawaita madaktari na wao kuanza kushangaa tu... ,

Ninapoambiwa Sosteness katuacha katika Mazingira Yale Yale inaumiza sana. Tunahitaji kufuatilia kwa karibu utoaji huduma za Afya katika Hospital ya DDH, Vinginevyo wananchi watakatiliwa Maisha kila kukicha.

Tangulia Mdogo wangu Mitti uliokoa maisha yangu, mimi nimeshindwa kuwepo kukuokoa. Bwana alitoa na BWANA ametwaa. Jina la Mungu wetu lihimidiwe. '' MWISHO wa kunukuu.

Nime-underline hiyo phrase ili kuonesha msisitizo kwa kile kilichonigusa. Ofcourse Daktari/Nesi hana guarantee ya kuzuia kifo cha mgonjwa, ila anaweza kukisababisha pia. Najaribu tu kuwaza by common sense kwamba mgonjwa alie kwenye critical condition anawekewa dripu then wanamuacha wanaondoka zao, mgonjwa anafariki na hawana habari !! Hili ni tatizo kubwa sana. Professional negligence, yes... ni uzembe tu au incompetence!

Katika uzi huo ulionigusa sana, mkuu mshana jr nae akachangia hivi (namnukuu):

'' Nilimpeleka ndugu yangu ocean road hospital alikuwa na shida ya cancer. Kufika Pale kuonekana yuko dhaifu saana akapewa drip ya sukari bila vipimo. Baadae doctor alipokuja kufanya vipimo akakuta sugar iko 32 normal ni 4-7, wakastopisha ile drip haraka sana but it was too late alifariki siku ileile jioni. Hii imetokea mwezi uliopita'' MWISHO wa kunukuu.

Hapo nilipo-underline, ni kuonesha jinsi gani baadhi ya madaktari wamegeuka kuwa wapiga ramli. Mgonjwa bila hata kufanyiwa kipimo cha haraka kwanza, anatundikwa dripu la sukari, eti baada ya dripu ndo wanafanya vipimo na kukuta sukari ishakuwa excessive mwilini. Ina maana walitumia 'macho' tu kutazama na kuconfirm kwamba mwili wa mgonjwa unahitaji sukari. Hii ni sawa na ramli. Tatizo kubwa sana hili. Professional negligence, yes... ni uzembe tu au incompetence!

Katika uzi huo huo, mdau mwingine KikulachoChako , nae pia akashea mkasa huu (namnukuu):

'' Nakumbuka kisa kimoja cha mtu fulani aliyekuwa amelazwa kwenye kituo fulani cha afya.....
Nesi alipomkuta kazimia akawaambia ndugu zake kuwa amefariki na ndugu wakaanza kuangua kilio.....ikawa wanaandaa mipango ya mazishi na maiti wakaipeleka nyumbani.....wakati wanamuaandaa maiti kwa ajili ya mazishi mara ghafla marehemu akazinduka na kuwashangaa wao.

Sasa jiulize kesi kama hizo zipo ngapi ?? na ni wangapi wanazikwa hai....kama jamaa asingezinduka si ndio angefukiwa moja kwa moja ??? MWISHO wa kunukuu.

In the underlined, mgonjwa amelazwa hospitalini. Anazimia, kisha Nesi anathibitisha kifo just kwa kumtizama tu na kukisia, bila vipimo. Tatizo kubwa sana hili. Professional negligence, yes... ni uzembe tu au incompetence!

Mkasa mwingine wa kusikitisha ni huu ufuatao, katika uzi huo huo, namnukuu ehee kumbe:

'' Basi mwaka 1996 nilipeleka mwanagu hapo Bunda DDH alikuwa anaumwa homa Kali sana. Nikaonana na Dkt nikaandikiwa vipimo nikaenda maabara mtoto akapimwa nikapewa majibu kuwa ana homa Kali sana lakini hana maji kabisa muda wowote anaweza kufa. Ikabidi Dkt aache watu wako mwenye foleni akaondoka na mgonjwa wangu mpaka hodini akamwambia nesi mwekee huyu mtoto drip sasa hivi Fanya haraka. Nesi kaleta drip, yule Dkt akaondoka akawahi wagonjwa aliowaacho foleni.

Dkt alipoondoka tu, nesi akaning'iniza chupa ya Maji kwenye stand bila kumwekea mtoto, nesi akaenda kukaa kwenye kichumba chao akatutelekeza hapo. Kila nikimfata ananijibu kwa hasira 'ina maana unatufundisha kazi'. Nikaona hapa nikizubaa mwanangu anakufa, basi nikamfata nesi kwa hasira nikamukwida nimpe vibao! Ghafula Dkt mkuu WA hospt Dkt Sweya akatokea alikuwa anatembea Wodini anasalimia wagonjwa, akaona nilivyo mkwida nesi, akaja nikamweleza kila kitu. Nesi akakoromewa akatolewa akaletwa mwingine. Mwanangu akawekewa dripu na Dkt sweya.

Ajabu hata huyo nesi mwingine aliyeletwa nae ni jipu! Muda kidogo kitanda nilicholazwa akaletwa mtoto mmoja toka kijiji kung'ombe ameishiwa damu, wakamtoa babaake damu, ikaletwa ikatundikwa kwenye stand ikatelekezwa hapo.

Nikawa namsihi baba MTU nenda wafate ila anaogopa. Zaidi ya SAA moja hajawekewa damu yule mtoto akafa! Nesi akachukua ile CHUPA ya damu akaondoka nayo sijui alienda kuiuza.

Ukifikiria utadhani hawa manesi wana mkataba na kuzimu WA kuchomoa roho zetu.hawana huruma.'' MWISHO wa kunukuu.

LA MWISHO kabisa ambalo nusura linitoe machozi, ni mkasa alioshea mkuu luckyline kwenye huo huo. Namnukuu:

'' Imeniuma sana utafikiri yamenikuta mimi, hivyo na bugando ni zaidi ya hao, yaanikupeleka mgonjwa wako akiwa mahuhuti bugando ni sawasawa na kumzika kabla hajakata roho. Juzi kati nilikuwa pale kwenye folen mama mmoja alionekana mtu wa kijijini sana, akanivuta mkono akaniambia naomba elfu 70 mama yake yuko hoi anataka kufanyiwa operation tho operation ni laki 3 nikamwambia mbona sina?

Akanambia watamtumia baadae mpesa kwanza nimsaidie hiyo, kweli nilikuwa sina iyo 70 kwa mda huo maana nami nilikuwa na mtoto wa dada ana tatizo la mguu na ndo tulikuwa tunaingia kwa dr, nikwamwambia ebu wambie home wakutumie hela nikupeleke mpesa utoe, akanambia hana mpesa yeye anatumia halotel na pale bugando hakuna iyo huduma, dah nikaitwa kwa dr, mama alivyoona nimeondoka alimwaga machozi kumbe alikuwa alishaomba msaada kila mmoja anamkwepa.

Nilivyoingia kwa dr nikamwacha dada na mtoto nikarudi kumwona huyo mama alikuwa anatoka tarime,hata kiswahili tulikuwa hatuelewani vizuri, kujielezea ni sheeda, nikamwomba number ya mtu ambae anataka kumtumia simu, nikamwomba atume hiyo hela kwangu ili nimtolee, siku hiyo mtandao ulikuwa mbovu mpaka sa 11 za jion ndo hela iliingia, nikamtolea nikampa, akashukuru nikaenda home.

Kumbe ambe mgonjwa wake alikuwa hoi hakojoi ni maumivu makari, akalipa 250000 ili mgonjwa afanyiwe operation elfu 50 atazilipa baadae maana iyo 50 alibaki nayo kwa matumizi ya chakula, mwee usiku ananipigia, kuwa hela amelipa mpaka sasa hawajamuhudumia na kumbuka mgonjwa hapo alikuwa na siku 3 anapewa panado. Aliponipigia niende kumsaidia niongee na ma dr, akanambia mtoto wake ana njaa. Sasa ikabidi kwanza nipike hili niende kumsaidia, nafika bugando tu akafariki !! Hela alishalipa huduma hakuna, tukaanza kulia, kwenda kuomba arudishiwe hela imsaidie kusafirisha mwili wakasema hiyo hela ataishugulikia baadae, kwanza aende azike atarudi. Loh Bugando mmelaaniwa! Yule mama hakufa kwa mapenzi ya Mungu. Ma dr wa Bugando kama mko humu hii ni laana, mnapenda hela kuliko uhai wa mtu??? '' MWISHO wa kunukuu.

Mkuu luckyline, kwanza nikupongeze sana jinsi ulivyomkirimu huyo mama ili kuokoa maisha ya mama yake. That story is very touching kwakweli!!! Mungu akupe maisha marefu kwa moyo huo. Hakika ulitenda wema mkubwa sana to that poor indigenous woman. Na hayo ndo maisha ya watanzania walio wengi. Hayo ndo yanawapata watanzania wengi, in particular waliopo vijijini.

Wakuu, hayo ni baadhi tu ya matukio ya kusikitisha ambayo yanaendelea huku kitaa. Watu wanazidi kupoteza uhai kwa sababu tu ya uzembe wa kijinga kabsa wa baadhi ya watumishi kwenye hospitali zetu.

Kuna kitu kinaitwa 'PROFESSIONAL NEGLIGENCE', yani uzembe wa kitaaluma (kama tafsiri yangu ipo sahihi). Mtoa huduma anashtakiwa mahakamani na kuwa liable accordingly endapo amefanya uzembe uliosababisha madhara kwa mpokea huduma. Mfano mzuri ni ile inshu ya Daktari kupasua kichwa badala ya mguu. Nchi za wenzetu hawafanyi uzembe wa kijinga jinga kama hapa kwetu. Wanawajibishana haraka sana mtu anapofanya fyongo!

Watanzania wenzagu, hebu sasa tuache kuchukulia poa hizi issues za uzembe wa watumishi wa hospitals. Ifikie mahala tuanze kuwapeleka mahakamani, na case ipewe public attention. Hii itasaidia sana kuwa-lesson wengine wa aina hiyo.

Tuacheni hizi kasumba za kiduwanzi eti ooh 'bahati mbaya', eti oooh 'mipango ya Mungu', eti ooh 'aargh Mtu mwenyewe ameshakufa. Hata nikifuatilia hawezi rudi' n.k. Ebu nenda nchi za wenzetu ufanye huo uzembe wako usababishe damages kwa mtu afu eti uanze kuleta uswahili wako wa 'bahati mbaya, sijuwi mipango ya Mungu' uone utavyotolewa kijasho chembamba! Linapokuja suala la Afya, tusichukulie poa. AFYA ndo mtaji mkuu katika maisha ya binadamu.

Fikiria tu hiyo mikasa yote ya vifo hapo juu, hakuna hata mtumishi mmoja hapo aliekuwa held accountable kwa hizo negligence. Tubadilike watanzania. Watu wengi sana wanapoteza maisha huko mahospitalini kwa sababu tu ya either UZEMBE au RUSHWA.

Ama kweli AFRICA is the went blanket of frustrations! We become warriors of survival by just waiving the web of 'hope' !

- Kaveli -
 
Kaveli umenena kweli!
Je unaweza kutoa maoni juu ya utatuzi wa changamoto hii!
 
Daaah.. Daktari Mimi sijui niseme lipi,

MUNGU Tusamehe na Utuhurumie


ndo hivyo mkuu. Watu wanakufa kwa uzembe wa wazi wazi kabsa. Na raia tushazoea, tunasema eti 'bahati mbaya' . Watu wanajisemea jamani ni 'mipango ya Mungu', kisha maisha yanasonga hivyo kibongobongo.
 
Inasikitisha sana.Shemeji yangu mpaka leo hapati mimba kwa kuwa mfuko wa uzazi ulishonewa na utumbo na Daktari mlevi.Kwa tukio hili amepata matatizo mengine mengi pamoja na hilo la kutozaa.Kesho kutwa anakwenda kufanyiwa opereashen tena,infact ya tatu kujaribu kurekebisha tatizo hilo hilo,tena kwa malipo!Hapana,something has to be done about these very reckless Doctors.Ni kama wako juu ya sheria hivi.
kabisa mkuu. na maisha ya watu wengi sana yanapotea kutokana tu na uzembe huo. afu raia tunachukulia poa tu. Inasikitisha
 
Ningependa sana rais wetu Magufuli na waziri wa afya wapite wasome hii thread, kuna tatizo kubwa mnoo upande wa huduma za afya.
 
Inasikitisha sana.Shemeji yangu mpaka leo hapati mimba kwa kuwa mfuko wa uzazi ulishonewa na utumbo na Daktari mlevi.Kwa tukio hili amepata matatizo mengine mengi pamoja na hilo la kutozaa.Kesho kutwa anakwenda kufanyiwa opereashen tena,infact ya tatu kujaribu kurekebisha tatizo hilo hilo,tena kwa malipo!Hapana,something has to be done about these very reckless Doctors.Ni kama wako juu ya sheria hivi.


Sasa imagine hiyo inshu yako mkuu. Daktari kwa uzembe wa wazi kabsa, anafanya operesheni vibaya na kumsababishia mgonjwa madhara makubwa for life time. Alafu hilo daktari lipo tu linaendelea kulewa na kuwapasua wengine. Hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake, neither by the employer nor by the victim! Halafu tunaishia kusema ooh 'bahati mbaya' na 'mipango ya Mungu' !

Mkuu, mpelekeni mahakamani huyo Daktari. Tena mna evidence ya wazi wazi kabsa. Mpelekeni mahakamani amlipe fidia huyo mama.

Africa tunafanyiana madudu mengi sana. Ndo maana ni ngumu kupata maendeleo. Mfano huyo shemeji yako, kwa kiasi fulani hapo ni kama kasababishiwa ulemavu wa kudumu humo tumboni. Hatakuwa sawa tena kama mwanzo. That means ataendelea kupata complications na kushindwa kufanya kazi zake za kujenga Taifa. All those just by the negligent Doctor!!!

Poleni sana
 
Ubarikiwe mleta mada hii.
Wakati umefika kwa wenzetu wa fani hii kumulikwa. Baadhi yao wameua watu wengi kwa uzembe na kuathiri maisha ya wengi.
Kweli, lazima kuwe na mfumo unaoeleweka unaongalia Medical malpractice na Professional Negligence hapa Tanzania.
 
Hii mada ni ngumu sana!
Madaktari na wauguzi wanaweza kutumika kama mifano tu ya watendaji wetu!
Tatizo kama hili lipo shuleni, how comes mtoto akae miaka 7 kisha atoke hajui kusoma wala kuandika! How comes case iliyokamatwa na vithibiti ikachelewa hukumu miaka 10 kwa kukosa ushahidi! How comes viwanja viwe na hati 2! How comes serikali ikaibiwa pesa na hakuna wa kushtakiwa!
Kwa lugha ya pamoja, watanzania hatuwajibiki ipasavyo mahala petu pa kazi!
Sasa ni mbaya sana ikiwa eneo lako la kazi linahusiana na maisha ya watu!
Wapo watendaji wa afya wanaodai kuwa kipato chao hakikidhi haja na wanapaswa kutumia mbinu za ziada kuinua kipato, hii ina maanisha kwa rushwa, kuwa na hospitali 2 au zaidi etc!
Kwa wale wanaofanya kazi sehemu zaidi ya 1 ufanisi unapungua kutokana na ukweli kwamba wanachoka, lkn kwa wale wa rushwa sio suala la uchovu tu Bali hata utu hutoweka, kitu ambacho ni msingi Mkuu ktk taaluma! Pia kazi zitafanywa kwa kificho kitu kinachowaweka wewe na mtoa huduma wako ktk uhatari kwa kuwa kazi inatakiwa iwe ya haraka na isishirikishe wengine! Hapa tunazungumzia negligence!
Linapokuja suala la incompetence, hapa tatizo ndio kwanza linaanza na bado kwa kadri miaka inavyokwenda tutazidi kuwa na hali mbaya zaidi!
Zamani Madaktari walikuwa ni watu Fulani vichwa na kile chuo chao cha Muhimbili kilikuwa kinasimamia taaluma hiyo, baada ya kufungua vyuo vikuu vya afya zaidi ya vitano, mambo ya kuchakachua madokta ikazidi, watu vilaza na wachumia tumbo wakajipachika huko na hadi sasa umeshakuwa ngumu kuzuia!
Ni wakati sasa kuwe na mifumo maalum ya ufuatiliaji wa taaluma ktk taasisi za kufundishia na pia ktk vituo vya kutolea huduma!
Bunge lipitie sheria zinazowakaba wanataaluma ili wanapofanya kosa wao na waajiri wao wawajibike!
Lakini kwa upande mwingine, serikali ihakikishe vitendea kazi vinapatikana ktk hospital zetu, ili kujenga morarly kwa wachache wanaojituma wasije kukatishwa tamaa!
 
tuwe pole watanzania wenzangu kwa majanga yanayosababishwa na watoa huduma za afya. mimi kabla cjaunga mkono wachangiaji waliopita naomba niandike hivi.
Sisi tunataka watoa huduma watoe huduma bora za Afya wakati wao hatuwajali katika maslahi yao, mazingira ya kazi sio rafiki, idadi kubwa ya wagonjwa pamoja na malipo duni. Niliwahi sikia kua 60% ya wataaalamu waliomaliza shahada ya udaktari wanafanya kazi nyengine na sio udaktari au wamekimbilia nchi nyengine kwa ajili ya kufuata maslahi mazuri. Tunahitaji maboresho katika sekta ya Elimu na Afya ili tuweze kupata huduma nzuri na sio kuendelea kuwashambulia wataalamu.
NAWASILISHA
 
Mh.Kigwangala hili ndo jipu la kutumbua,achana na akina J.J Mwaka.Poleni sana wahanga wa uzembe wa madaktari! Wakati sasa umefika jamii tuhakikishe madaktari na wauguzi wazembe wanachukuliwa hatua za kisheria.
 
Hii mada ni ngumu sana!
Madaktari na wauguzi wanaweza kutumika kama mifano tu ya watendaji wetu!
Tatizo kama hili lipo shuleni, how comes mtoto akae miaka 7 kisha atoke hajui kusoma wala kuandika! How comes case iliyokamatwa na vithibiti ikachelewa hukumu miaka 10 kwa kukosa ushahidi! How comes viwanja viwe na hati 2! How comes serikali ikaibiwa pesa na hakuna wa kushtakiwa!
Kwa lugha ya pamoja, watanzania hatuwajibiki ipasavyo mahala petu pa kazi!
Sasa ni mbaya sana ikiwa eneo lako la kazi linahusiana na maisha ya watu!
Wapo watendaji wa afya wanaodai kuwa kipato chao hakikidhi haja na wanapaswa kutumia mbinu za ziada kuinua kipato, hii ina maanisha kwa rushwa, kuwa na hospitali 2 au zaidi etc!
Kwa wale wanaofanya kazi sehemu zaidi ya 1 ufanisi unapungua kutokana na ukweli kwamba wanachoka, lkn kwa wale wa rushwa sio suala la uchovu tu Bali hata utu hutoweka, kitu ambacho ni msingi Mkuu ktk taaluma! Pia kazi zitafanywa kwa kificho kitu kinachowaweka wewe na mtoa huduma wako ktk uhatari kwa kuwa kazi inatakiwa iwe ya haraka na isishirikishe wengine! Hapa tunazungumzia negligence!
Linapokuja suala la incompetence, hapa tatizo ndio kwanza linaanza na bado kwa kadri miaka inavyokwenda tutazidi kuwa na hali mbaya zaidi!
Zamani Madaktari walikuwa ni watu Fulani vichwa na kile chuo chao cha Muhimbili kilikuwa kinasimamia taaluma hiyo, baada ya kufungua vyuo vikuu vya afya zaidi ya vitano, mambo ya kuchakachua madokta ikazidi, watu vilaza na wachumia tumbo wakajipachika huko na hadi sasa umeshakuwa ngumu kuzuia!
Ni wakati sasa kuwe na mifumo maalum ya ufuatiliaji wa taaluma ktk taasisi za kufundishia na pia ktk vituo vya kutolea huduma!
Bunge lipitie sheria zinazowakaba wanataaluma ili wanapofanya kosa wao na waajiri wao wawajibike!
Lakini kwa upande mwingine, serikali ihakikishe vitendea kazi vinapatikana ktk hospital zetu, ili kujenga morarly kwa wachache wanaojituma wasije kukatishwa tamaa!


Mkuu, hakika umenena vyema sana. Umeeleza mawazo chanya kabisa kuhusu hii sekta ya Afya. Umetoa pendekezo zuri sana kwamba ni wakati sasa kuwe na mifumo maalum ya ufuatiliaji wa taaluma ktk taasisi za kufundishia na pia ktk vituo vya kutolea huduma!
Bunge lipitie sheria zinazowakaba wanataaluma ili wanapofanya kosa wao na waajiri wao wawajibike!
Lakini kwa upande mwingine, serikali ihakikishe vitendea kazi vinapatikana ktk hospital zetu, ili kujenga morarly kwa wachache wanaojituma wasije kukatishwa tamaa .

Maoni yako yameenda sambamba kabisa na hoja ya mdau crocodile hapo juu aliechangia kwamba sasa uwepo mfumo unaoeleweka unaongalia Medical malpractice na Professional Negligence hapa Tanzania.

Pia nadhani, na sisi wananchi tuanze kubadilisha mentality zetu juu ya wauguzi wanaofanya uzembe katika kuhudumia wagonjwa. Watanzania tuache huu 'upole' wetu wa kuchukulia poa kila jambo ata kama jambo linaathiri maisha ya mtu. Daktari/Muuguzi amefanya uzembe wa wazi wazi kabsa ambao hauna reasonable justification na madhara yametokea, basi watu wavoice-out na mhusika afikishwe kwenye vyombo vya kumuwajibisha accordingly.

Nchi zilizoendelea, daktari akifanya fyongo ya kudamage afya ya mgonjwa... anawajibishwa ipasavyo, analipa fidia kwa victim, na Cheti chake cha Taaluma kinakuwa disqualified. Ananyang'anywa Cheti, na anapigwa ban kutoa huduma za kitabibu! Yani hakuna kuchukulia poa, na wananchi wapo very aggressive when it comes to Health issues.
 
Inasikitisha sana.Shemeji yangu mpaka leo hapati mimba kwa kuwa mfuko wa uzazi ulishonewa na utumbo na Daktari mlevi.Kwa tukio hili amepata matatizo mengine mengi pamoja na hilo la kutozaa.Kesho kutwa anakwenda kufanyiwa opereashen tena,infact ya tatu kujaribu kurekebisha tatizo hilo hilo,tena kwa malipo!Hapana,something has to be done about these very reckless Doctors.Ni kama wako juu ya sheria hivi.
Duh
Too much jamani

Wanamtia mtu ulemavu bila sababu

Very sad.

Je walimshtaki dr husika? Unajua uzembe kama huu ujiachiwa matatizo yatakuwa hayaishi
 
Back
Top Bottom