Kuishi Dar ndio dharau kiasi hiki

Kuishi Dar ndio dharau kiasi hiki

Weka tu picha yake utasaidiwa mbona unalialia kama hujui kucheza na technolojia haujafikaga Dar nini? Siku hizi hatuzungukagi kumtafuta mtu tunatumia milingoti ya simu kuisoma destination yake tunampata, hata asipopokea simu unatuma msg ikideliver unaanzia hapo mkuu. Muwe mnakuja Dar kujifunza maujanja

kuja dar kujifunza msg delivered au? Mbona hata internet inatosha kuelewa hayo mambo au we umejifunzia vijiweni nin?
 
Ulishawahi kudhulumiwa ?Hiyo ndio dhuluma sasa.Kupambana na dhuluma kuna njia ya diplomacy au violence,chagua moja utakayo ona inakufaa au samehe tu.

Nimepata funzo mkuu,kama ni dhuluma itakuwa ya kwanza ambayo ni kubwa.
 
Cha msingi hapo n kujaribu ku2mia njia ya mazungumzo zaidi ili akuelewe and who knows labda atalainika na kukurudishia pesa yako
 
Watu waliokuja mjini juzi hao, hawajaona Dar enzi za Halmashauri ya Jiji inazoa taka.

Enzi hizo unaenda Posta half of the kids you meet you know from School, libraries (Tanganyika, British Council, American mpaka Russian Centre next to Diamond - sio Diamond Platinum, Diamond Jubilee - kuchukua vitabu vya Propaganda za Kirusi etc), mpira etc.

Dar enzi hizo mtu akikwambia anapenda muziki maana yake anaenda kuchukua music lessons Jumba la Wakorea, watu wanafanya performing arts Russian Cultural Centre mnaenda kukutana na kina Natasha huko. Mashindano ya breakdancing Chuche, Lauli na Omary. Kabla ya mambo ya pool side na ghorofa ya saba na "Yo Rap Bonanza" na marehemu Abdulakim Mgomelo.

Dar parties za kwa Che Mfaume Rd, hapo sijakurudisha enzi za Dar ina Zimamoto inayofanya kazi pale Mwembetogwa.

Dar unamzaba kofi mtoto wa rais (wakati kila mtu jambajamba) halafu unampiga beat akisema kwa mwalimu utamuuilia mbali kabisa, kisha kakuringishia sura ya baba yake kwenye shilingi (lord forgive me, even though I am a non-believer). Such childish impunity!

Leo walugaluga wamekuja wamekuta Dar wenyewe tumewapisha wahemee wanajifanya wanaijua Dar, wakati watu tunaipata na familia zimo katika historia kabla ya kujengwa "nyumba ya saa".

Walugaluga wakisema wanaijua Dar na wajukuu wa Jumbe Tambaza watasemaje?

Nilivyofika NYC zama hizo an old gentleman once told me, akaniambia wale old school New Yorkers ambao wapo hapa long time wanaelewa vitu hawana matatizo.

Ogopa sana walugaluga waliohamia juzi hawajapoteza hata accents wanavyoringia u-New Yorker.

Ndio kitu kile kile kinaendelea hapa.

Watu wa Dar wenyewe wenye viunga kuanzia Upanga, Obay, Kijitonyama, Sinza, Tabata, Mbezi Beach mpaka Mkuranga, Mbezi na kwenda Chanika na Kisarawe huko tunajua debonair ya Dar na decorum inayotakiwa kwa mtoto wa mjini.

Mtoto wa mjini hawezi kuchafua jina kwa deni, hususan la kitoto kama hilo la 200,000. Ukimwambia Mussa Malori "nimetoa sadaka 200,000" atakwambia "hujatoa bado".

Hiyo ni tip tu anapewa doorman anayefungua mlango au bartender a-keep champagne baridi kwa centrigrade inayotakiwa.

Huyo mlugaluga tu, anaharibia debonairs wa Dar.

Ulugaluga as well as being urbanite are both states of mind more than attributes of origin.

Yeah_enzi za Tambaza hizo mkuu
 
Vuta bangi kiongozi utamwona kama sisimizi ukishindwa muone lwakatare

Hamna haja ya bangi mkuu.,...jamaa anaonekana ni mweupe ndio maana anathubutu kulingia dar... .wish nongekua mimi angefurahi,...pasaka njema mkuu
 
mie naona wajanja na watoto wa mjini wapo Arusha na Mwanza, Hapa Dar ni ubabaifu tu........!

Watu wa huko maporini mnatuonea donge na wivu watoto tuliozaliwa na kukulia Dar! mbona mnadhihirisha ushamba wenu waziwazi hivi? sasa waarusha na mwanza hicho kiswahili chenu tu kinachosha kusikilizwa, yani cha kidosho balaa! kidogo lakini watoto wa Arusha tunaweza kuwaelewa lakini wa Mwanza hata kidogo hawasomeki, yani wamezidi ushamba.
 
Tafuta elf 30 tukamfilishe kwa watoto wa mujini atie adabu,
 
Watu wa huko maporini mnatuonea donge na wivu watoto tuliozaliwa na kukulia Dar! mbona mnadhihirisha ushamba wenu waziwazi hivi? sasa waarusha na mwanza hicho kiswahili chenu tu kinachosha kusikilizwa, yani cha kidosho balaa! kidogo lakini watoto wa Arusha tunaweza kuwaelewa lakini wa Mwanza hata kidogo hawasomeki, yani wamezidi ushamba.
Mie nimezaliwa na kukulia Dar lakini sijaona ujanja wowote wa vijana wa Dar zaidi ya umarioo tu na ushamba ushamba, wachache sana ni wa janja na wengi katika hao wachache hawajazaliwa wala kukulia hapa wametoka Arusha, Mbeya na Mwanza wengi wao ni wachakarikaji sana umemipataa eeh hamy-d ?
 
Tafuta mjeda mwenye mbavu kuanzia mbili au hata nyota moja nenda naye hadi kwao nakuhakikishia atatoa na kama laki 2 hivi ya usumbufu trust me
 
Tafuta mjeda mwenye mbavu kuanzia mbili au hata nyota moja nenda naye hadi kwao nakuhakikishia atatoa na kama laki 2 hivi ya usumbufu trust me


we ngoja tu mwezi wa5 nipo dar kama noma na iwe noma na undugu ufe
 
Ni ndugu yangu kwani ukoo ni mmoja na nimeelezea apo awali aliwahi kuishi kwetu miaka ya nyuma kabla ya yeye kwenda dar 1992,

I predicted this shyt, in Tupacalypse!
-2Pac
 
Back
Top Bottom