Kama una mshkaji wako ambaye ni askari au mwanajeshi jaribu kumtumia kwa ahadi utampatia hata elfu 50 pesa ikiingia. Ni bora upate angalau sehemu ya pesa yako kuliko kuipoteza kabisa. Ikiwezekana jamaa wakimchimba mkwara vizuri anaweza kulipa na ya usumbufu mkuu.
Siku ingine usipende kuwakopesha marafiki walioko mbali pesa yako. Hata kama yupo jirani jitahidi sana kuangalia life style yake, vyanzo vyake vya kifesha, reputation yake kwa jamii, kiasi anachokukopa n.k siku zote zikiliza hisia zako, ukiona una mashaka mwambie huna hiyo pesa nawe ulikuwa na mpango wa kumkopa.
Jambo jingine la kuangalia, ni kwamba usipende kumkopesha mtu kiasi kilekile anachokukopa .....kama ukikopwa laki mbili unamwambia mkopaji sina hiyo labda nikukopeshe elfu hamsini niliyo nayo na nyingine utaongezea mahala pengine.
Maisja yamekuwa magumu sana kipindi hiki cha JK hivyo ni vyema kuwa makini na utokaji wa pesa uliyo nayo.