Kuingiza Sukari Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuingiza Sukari Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Game Theory, Feb 14, 2012.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakubwa

  Nimepata line ya kuingiza sukari Tanzania baada ya kukutana na wafanyabiashara hiyo Dubai (sukari haitokei Dubai bali hawa jamaa wana base hapa)


  Naweza kupewa tani nitakazo lakini jamaa bado sijakubaliana nao kitu

  sasa naskia biashara ya sukari ina syndicate tanzania yaani Mohd entreprises, bakhressa peke yao

  Je wanunuzi wakubwa wa sukari ni serikali au watu binafsi?

  Je Tanzania soko lipo?

  Je chajuu changu ni negotiate na nani?

  Inalipa?
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sukari toka Dubai????

  Siyo toka Zambia ama Malawi hata????
  Nina mashaka kidogo!
  Ila ngoja wadau waje!

  Majibu mazuri utapata!
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hukunielewa kaka

  jamaa nilikutana nao hapa Dubai ni wafanya baishara wanapeleka Sukari kwa meli nchi mbali mbali duniani

  Dubai ni kama ofisi tuu kaka
   
 4. Old-Timer

  Old-Timer Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengine wanaleta toka Brazil
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hivi ulishawahi kufanya biashara yoyote? Mbona unauliza cha juu upatane na nani? Kuna hao Supplier --- Wewe ---- Buyers (private enterprise, wholesalers ...). Hapo unategemea unegotiate na nani? Anyway hayo tuyaache, mimi nitakujibu kwenye RED tu hiyo conspiracy watakuja kukujibu wenye data

  Je wanunuzi wakubwa wa sukari ni serikali au watu binafsi?
  Wanunuzi wakubwa si Serikali, bali ni viwanda (private enterprise); hawa hununua in bulky, na watu binafsi; hawa hununua rejareja. Sasa soko zuri kwako ni wauzaji wa jumla na watu wenye viwanda.

  Je Tanzania soko lipo?
  Soko lipo, na demand ni kubwa kuliko Spply ndio maana bei inapanda kila kukicha (ingawa kupanda kwa bei kumechangiwa pia na kupanda kwa gharama za uzalishaji)

  Inalipa?

  Kama soko lipo ina maana inalipa
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Poa!

  Nilikuwa cjakusoma vema Kamanda!
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kamanda nimekupata lakini nilitaka tuu kujua maana sijawahi kuifanya hii biashara na sijui mambo ya kodi na mengineyo kama niliyokuuliza yanakwendaje.


  Kuhusu kamisheni ukweli ni kuwa sijajua watu wanalipwa vipi yaani shilingi ngapio kwa Tani.

  lakini mie naona bora ni negotiate na hawa waingizaji ambao najua watakuwa na maximum bei wanayotaka kuuza lakini pia wanunuzi hao wa bulk najua wakiona bei ni ya chini watataka kujifanya wanawajua hawa jamaa ili waniondoe mimi middle man

  ninafkiria kuwasainisha waingizaji mkataba wa kuwa mtu wao Tanzania lakini kwa akili za wafanya biashara wataona mimi nafaidia lakini lazima nilinde maslahi yangu si unajua hali ngumu sana kwetu sie ma mido men?

  Je wanunuzi wa bulk ndio hao akina baaresa na zakaria tuu au?
   
 8. u

  ureni JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye inalipa inadepend,usisahau huyu jamaa anasafirisha hiyo sukari from sijui brazili au dubai na inahitaji gharama,hatujui ananunua huko kwa bei gani,hatujui kodi atalipa kiasi gani,hata kama demand ikiwa kubwa lakini lazima ataendana na bei ya soko.kwa hiyo anahitaji mchakato mkubwa wa mahesabu na uchunguzi wa kina.
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nakubali Mkuu, hapo ulivyoliweka, limekaa vizuri zaidi. Cha msingi ni kufanya utafiti kama ulivyosema na kushughulikia vibali husika kwan si kila mtu anaweza akaagiza hii kitu
   
 10. b

  ben van mike JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 471
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 33
  mkuu hi biashara inalipa sana ,lakini inaonekana swali lako lina base kwenye pricing tuuu , tafuta clearing agency au mtu wa tra akupe estimate ya kodi , wadau humu watakupa bei za jumla za sukari kwa sasa , kwa hiyo we uapiga hesabu yako kila tani unaweza pata faida gani lakini kwa ufupi mzigo ukitua tanzania unauzika ...ukiweza kupata link kenya na uganda ndio balaa , urudi utupe feedback .
   
 11. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Jua kuwa unaitaji leseni ya sugar import toka bodi ya sukari hapa ndo kuna muziki munene
   
 12. MANI

  MANI Platinum Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Na mara nyingi vibali hutolewa mwaka mmoja kabla.Yaani wale consumer wakubwa ie wenye viwanda wanapeleka quota zao kwa hiyo inakuwa planned kabisa the following year so and so will import this much !
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye RED Import Duty ya sukari (BROWN SUGAR) ni 100% or 200$ per mt (which ever is higher).Usishangae kwa nini sukari ni ghali nchini, hapo hujazungumzia port charges wala VAT
   
Loading...