Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,908
- 30,253
JULIUS NYERERE, JULIUS CAESAR, SAHIB NA VITABU VIJAVYO VYA SHEIKH PONDA
Kuna rafiki yangu kaniambia kuwa wakati alipokuwa anafanyakazi katika shirika moja kubwa la kimataifa linaloshughulika na Afrika ndipo alipomjua Mwalimu Nyerere vizuri sana.
Anasema hakuna kilichokuwa kinampita kilichoandikwa na Mwalimu au kuhusu yeye.
Huyu sahib yangu si Mtanzania lakini ana mapenzi makubwa na Tanzania na anasema vitu viwili ndivyo vilivyomfanya aipende Tanzania.
Kitu cha kwanza ni Julius Nyerere na cha pili ni mchezo wa William Shakespeare, "Julius Caesar," mchezo kitabu chake alichotafsiri Mwalimu kwa Kiswahili mwaka wa 1963.
Haya ndiyo yalikuwa mazungumzo yetu siku ya kwanza tulipokutana na akanialika chakula cha jioni nyumbani kwake.
Nimeshangaa kwa yeye kumpenda Shakespeare kwa sababu nilipojulishwa kwake haraka baada ya kuachana nikamtafuta Google.
Naam sahib yangu ni msomi mkubwa na kasoma elimu nzito na kaandika mambo makubwa kuhusu Afrika.
"Mohamed nimesoma kitabu chako na nilikipata Marekani kanipa Mtanzania mmoja tukifanya kazi shirika moja.''
Aliponiambia tu kuwa kasoma kitabu changu kimoyomoyo nikasema, "Bismillah..." kwani nilijua nini kitafuata.
Sahib akasema, ''Huyu jamaa aliniambia kuwa maswali yangu yote ninayomuuuliza kuhusu Tanzania nitapata majibu yake katika kitabu chako.''
Nilichokitegemea kuja hakikuja kama vile nlivyotegemea.
Kikaja kitu kingine kabisa hata hivyo si mbali na yale niliyotegemea.
Sahib ananisomea kipande cha Shakespeare, "There is a tide in the affairs of men which taken at the flood leads on to fortune omitted all the voyage of their life is bound in shallows and miseries?''
Brutus huyo anatafakari alifanye sasa au asubuhi na ana hofu akisubiri huenda nafasi ikampita.
Nikajiambia kumbe ile Bismillah yangu haikwenda patupu.
Maneno haya aliyosema Brutus mazito.
Wanasiasa huyatumia wanapojuta kwa kutochukua hatua stahiki na pili hutumia kwa kuchukua hatua wakafanikiwa au wasifanikiwe.
Nikamwambia umenikumbusha mzee wangu marehemu Aboud Jumbe alipata siku moja kunisomea kipande hicho alipokuwa ananieleza maisha yake na vipi alikuja kuondoshwa madarakani mwaka wa 1984.
"Ukifahamiana na Mzee Aboud Jumbe?"
''Ni baba yangu kwani yeye alinichukua mimi kama mwanae.''
''Aboud Jumbe alikuwa mtu wa aina gani nimesoma kitabu cha Dr. Harith Ghassany...''
Wamarekani wanamsemo, ''There is no free lunch in America.''
Maana yake ni kuwa mtu akikualika chakula cha mchana basi jua ana lake jambo analotaka kwako.
Mimi sitaki kuwa mwizi wa fadhila siwezi kusema kuwa kwa kualikwa chakula cha usiku sahib alikuwa anataka kitu kwangu la hasha.
Mazungumzo yale yote yalikuja kwa kuwa naamini hakupata kukutana na mtu wa aina yangu kwani alinieleza kuwa katika mambo ambayo alikuwa yanamshangaza sana na kumsikitisha ni kuwa katika ofisi za ubalozi wa Tanzania huko nje hakupata kukutana na Muislam hata mmoja ila yule aliyempa kitabu changu UN, New York na yeye lau ni Mtanzania lakini anatoka Zanzibar na huko kila utakayemgusa ndiye.
Basi nikamjibu kuwa wapo lakini ni wachache mno.
Chakula kinakuwa na ladha zaidi kwa muziki mororo na mzungumzo matamu.
Ana vitu si mchezo lakini ndege kaitia katika dhoruba ya upepo mkali.
Nikahisi kama vile wale kamba ladha yake inanibadilikia.
Mimi nimepata kuwa ndani ya ndege iliyopigwa na dhoruba.
Mtu yeyote aliyepitia hali hii atanielewa.
Hili linafaa sana kumuombea adui wako limfike.
Rubani katoa tangazo abiria wote wafunge mikanda pamoja na wahudumu.
Ulikuwa usiku mkubwa Emirates inakata mawingu kati ya Dubai na Tehran.
Mbawa za ndege unasisikia zinalalamika mfano wa mlango wenye bawaba mbovu zilizoshika kutu.
Nikamrejesha sahib kwa ''Julius Caesar,'' ili kumtoa kwenye ile dhoruba nikamwambia kuwa baada ya kutafsiriwa kitabu kile na Mwalimu Nyerere, Shule ya Pugu waliucheza mchezo mzima mbele yake.
Nikamfahamisha kuwa mchezo ule ulirushwa mubashara radioni na mimi niliusikiliza wote bila kusinzia.
Ilikuwa mwaka wa 1964 na nilikuwa na umri wa miaka 12.
Nikimpenda Mwalimu na ule mchezo naweza kusema ndiyo ulinifanya nimpende William Shakespeare.
Sahib akanipokea na vipi ''The Merchant of Venice?''
Taib.
Chombo kimeshatoka kwenye mawimbi makubwa yanayochafua tumbo kinaelea buheri wa hamsa ishirini.
Nikacheka nikampa kipande kimoja kutoka, ''The Merchant of Venice:''
''Signor Antonio, many a time and oft
In the Rialto you have rated me
About my moneys and my usances.
Still have I borne it with a patient shrug,
For sufferance is the badge of all our tribe.''
Huyu Yahudi Shylock, mla riba.
''Mohamed umemsoma sana Shakespeare.''
Kisha akanipokea kutoka pale akanitupia jiwe akaendelea pale nilikoishia:
''You call me misbeliever, cutthroat dog,
And spet upon my Jewish gaberdine—''
Nilitabasamu nikampa mkono kama ishara ya kumwambia, ''Hakika wewe ni bingwa.''
Allah kawajaalia baadhi ya waja wake nema kubwa ya elimu.
Namtazama sahib wangu nimepwelewa.
Huyu mtu kasoma vyema na uwezo wake wa kuhifadhi ni hatari.
Lakini huyu mtu hakusoma Fasihi.
''Sasa ukitaka kuingia ndani ya ubongo wa Nyerere soma vitabu hivi alivyotafsiri utamuelewa vyema,'' anaieleza huku akikung'uta mkono wangu.
''Why Julius Caesar,'' ''Why Merchant of Venice,'' and for that matter why not ''Wafanyabiashara wa Venice'' it has to be, ''Mabepari wa Venice.''
''Hawa akina Sykes wakifanya biashara hawa, au sivyo?''
Sahib ananiuliza.
Haya ndiyo niliyokuwa nikiyasubiri toka asubuhi mwanzo alipokitaja kitabu changu.
''Rafiki zake wote wa karibu walikuwa wafanyabiashara,'' najibu.
''Hawa ndiyo walikuwa wafadhili wakubwa wa TANU.
Mzee Rupia, Dossa Aziz, Abdul na Ally Sykes wote walikuwa wafanyabishara.''
''Nyerere alikuwa kiongozi jasiri sana.''
Sahib wangu alimaliza na kuongeza, ''Mabepari wa Dar es Salaam.''
Hapa sote tukaangua kicheko.
Kalamu ina nguvu kushinda kitabu.
Siku Sheikh Ponda aliponiletea kitabu chake, ''Juhudi na Changamoto,'' nilimwambia, ''Ndugu yangu sasa umeingia katika dunia nyingine mpya kwako maisha yako hayatakuwa kama yale uliyozoea unatia mguu katika nchi hujapatapo kufika wala kuifikiria akilini kwako.''
Nimaeyasema haya wakati sikuwa najua kuwa Sheikh Ponda tayari kaandika vitabu 16.
Vitabu 16.
Vitabu 16 na vingine unakiogopa kitabu kwa kusikia jina lake tu ukaanza kujitisha mwenyewe.
Nani shujaa na jasiri kiasi akitajiwa Dr. John Sivalon asishtuke hata kidogo akitajiwa kuwa kuna kitabu kimeandikwa na Sheikh ponda kuhusu Dr. Sivalon.
Au akitajiwa kitabu cha ''Masheikh Gerezani,'' ''Waislam na Mkono wa Dola,'' ''Pitio la Zanzibar.''
Sheikh Ponda katufanyia kazi kubwa sana.
Kalamu ya Sheikh Ponda imetufungulia ukweli.
Sahib yangu na wengine mfano wake ambao hawakuwa wanaijua Tanzania vitabu hivi vitawasaidia kuijua nchi yetu na siasa zake.
Kweli Tanzania ni kisiwa cha amani?
Amani inaweza kuwapo vipi penye ubaguzi?