''Kuingia Kwa Uislamu Mwambao wa Afrika Mashariki'' Majumuisho ya Sheikh Alyani Ukumbi wa Idrisa Abdul Wakil 23 September 2023

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,268
Waandaaji wa kongamano Kituo cha Tarekhe ya Uislam na Wanavyuoni wa Afrika Mashariki na Maahad Juneyd Islamy Zanzibar waliwaalika wanahistoria kujadili ni lini Uliingia Uislam Pwani ya Afrika Mashariki.

Wataalamu wa historia na wanafunzi wa historia hii kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaika kutafuta ushahidi wenye ithibati kutaka kutegua kitendawili hiki.

Kongamano hili liliwakutanisha wasomi kutoka Yemen, Kenya, Tanzania Bara na Zanzibar kwenyewe pamoja na masheikh akiwemo Sheikh Alyan Hemed Jabir Al Farisy.

Katika mambo yaliyopamba mjadala ni kuwa baadhi ya Maprofesa waliotoa mada walizungumza jukwaa moja na wanafunzi waliowasomesha wenyewe vyuoni kwao.

Baadhi ya wanafunzi hawa wamefanya utafiti na kuandika vitabu kadhaa vya historia na ilipendeza sana kusikia wanafunzi wakitofautiana kwa kiasi fulani na misimamo ya maprofesa wao kuhusu ushahidi na utafiti mbalimbali uliofanywa kupitia vitabu vilivyoandikwa na uchimbaji (excavation) uliofanywa nje ya mipaka ya Zanzibar na Zanzibar kwenyewe.

Siku zote mijadala ya kisomi ina raha zake katika uchambuzi.

Katika mjadala ilijitokeza sana suala la Dola ya Zanzibar (Zenj Empire) katika historia ya Pwani ya Afrika ya Mashariki.

Katika wakati wa maswali na majibu na michango Sheikh Alyan aliutuliza mjadala mzima kwa namna alivyohitimisha suala la kuingia Uislam Afrika ya Mashariki na Uislam ambao uliokuwapo wakati huo.

Msikilize:

 
Back
Top Bottom