JOSE MOURINHO said goodbye to Inter Milan yesterday after a three-hour dinner with president Massimo Moratti.
Kwa wapenzi wa Soka la ulaya watakubaliana na mimi asilimia mia moja kwamba Jose ni kocha mwenye kipaji cha pekee, ni kocha ambaye ana kila mbinu za ushindi ndani ya miaka 10 iliyopita ajizolea misifa kibao, Ureno, Uingeleza, Italy na sasa anaelekea Uhispania kuprove worthy yake.
Baada ya kupata mafanikio na kikosi cha Porto ambacho hakikuwa na mastaa wengi - hakusita kuwaaga na kutafuta challenge mpya - ndipo akatua darajani kuikuta club ya chelsea na kuipa mafanikio makubwa sana.
Nia ya Jose ilikuwa aendelee kufundisha chelsea hadi kufikia mafanikio ya juu zaidi yaani kuipa UEFA cup - mbio hizi zilishindikana baada ya kutoelewana na Mmiliki wa club namna ya uchezaji na mbinu zake.
Jose anashutumiwa kutosheza mpira wa kuvutia ingawa yeye amekuwa akikanusha jambo hili.
Anakwenda Madrid kwa nia ya kuifufua timu hii ili irudi kwenye ulimwengu wa soka - wapenzi wa soka mtakuwa mnakumbuka jinsi Madrid ilivyokuwa enzi za akina Zizu na akina Claude Makalele- Swali Je Jose ataweza kuirudisha hadi hapo ilipokuwa nyakati hizo?
Kuna mastaa wengi tu atakuwakuta hapo, C. Ronaldo, Allonso, Rahul, Kaka na wengineo - nachomsifia Jose ni kwamba anajua to get quality out of players yaani kocha mwingine hawezi kujua jinsi ya kumtumia kaka na C Ronald kuweka combination nzuri - lakini Jose huyu ana kipaji hicho.
Namtakia Mafanikio mema Jose hapo maadrid lakini akumbuke kwamba kila timu inajizatiti vilivyo msimu ujao, Chelsea, Man U, Liver, Arsenal, Inter milan, Inter na Barca hawatakubali kirahisi madrid awe mfalme wa soka kirahisi tu eti Jose kaenda kule.
Sisi wapenzi wa soka tunaomba msimu ufike mapema ili tuanze kuona tena new challenge ya Jose " The Special One" kocha bora wa dunia kama anavyojiita kwa sasa - akitangaza mafanikio mengine huko uhispania.
Read more:
Jose Mourinho says goodbye to Inter Milan | The Sun |Sport|Football