Kuhusu Web Series ya 'We Men'

Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
623
1,000
'We Men' ni series mpya ya Kitanzania inayoonyeshwa kwenye Instagram page ya Maxrioba. Maudhui yake ni ya mapenzi (kama kawa). Kwa story nzima mnaweza kwenda kuiangalia huko Instagram.

Technically hii series wanajitahidi. Hapa ninaongelea rangi ya picha, mwanga, namna shots na scene zilivyopangiliwa etc ni standard nzuri

Shida yangu ni sauti. Ninaelewa kwamba sauti wanarekodi pembeni kwenye sound booth na wanakuja kuiongezea baadae lakini haina uhasilia hata kidogo. Husikii sauti ya mazingira unasikia tu sauti ya anayeongea. Kama vile redioni au kwenye podcast. Mimi ninashauri watengenezaji wa hii series wawekeze kwenye mike nzuri zitakazo daka sauti pale pale wakiwa wanashoot ili uhalisia usipotee. Kama hawawezi basi wafanye foley aka warekodi hata majani yaliyokauka yakikanyagwa au upepo ukivuma, waongezee baadae kwenye post production. Hii kidogo italeta uhalisia.

Kingine ni lugha. Kwanini mnalazimisha kuchanganya kiingereza na kiswahili sehemu hata isiyo na ulazima? Mbaya zaidi mnalazimisha kuongea kama African Americans 😂. Mnachekesha kweli, alafu kwasababu mnalazimishia kiingereza na huyo anayewaandikia script hakijui vizuri, dialogue inakua haina uhalisia. Inakuwa mechanical, stiff and cardboard like.

Sana sana mnacopy na kupaste dialogue kutoka Western movies na series. Hata waigizaji wanonekana hawajui kuigiza kwasababu ya dialogue ya Kiingereza mbaya. Mfano ni anayeigiza kama Temba, he isn't natural at all. Yupo kama robot going through the motions. Karibia waigizaji wote pale hawapo natural kwasababu dialogue haipo natural. Ushauri wangu msichanganye lugha. Kama ni kiswahili fanyeni kiswahili tu.

Kama ni kiingereza ni kiingereza tu tena mtafute screenwriter mzuri atakaewaandikia dialogue nzuri na siyo kucopy na kupaste kutoka Power. Kama mtachanganya basi kiingereza kiendane na mazingira ya Kitanzania. We are not Black Americans.

Cha mwisho ni story na pacing. Ingawa episodes ni fupi lakini kuna scene nyingi ambazo wahusika wanapoteza muda kufanya vitu ambavyo havina msingi havisogezi story mbele. Hii kitu inatakiwa iwe fast paced yaani mtu ukiangalia huchomoki mpaka episode inaisha.

Sio mtu unaanza kutafuta kitu kingine cha kufanya huku unasubiri kitu kitokee ili plot isogee. Fix your script! Yangu ni hayo tu mmejitahidi sana, mkijirekebishe mnapokosea. All the best keep on growing!
 
leroytz

JF-Expert Member
May 22, 2016
682
500
Umeongea kweli ila hapo kwenye lugha nadhani wanataka wateke pia soko la nje ya Tanzania, ila wanapokosea ni kuiga flows na kuzilazimishia kwenye uhalisia. Ila wanajitahidi kwa kibongobongo
 
Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
623
1,000
Umeongea kweli ila hapo kwenye lugha nadhani wanataka wateke pia soko la nje ya Tanzania, ila wanapokosea ni kuiga flows na kuzilazimishia kwenye uhalisia. Ila wanajitahidi kwa kibongobongo
Hata wangeongea kiswahili tupu wanaweka subtitles mambo yanaenda.
Hiyo kuiga flow ndo inafanya mpaka mtu unaona aibu hata ku recommend kwa marafiki wa nje.
 
leroytz

JF-Expert Member
May 22, 2016
682
500
Hata wangeongea kiswahili tupu wanaweka subtitles mambo yanaenda.
Hiyo kuiga flow ndo inafanya mpaka mtu unaona aibu hata ku recommend kwa marafiki wa nje.
Umeongea point, maana kuna series nyingi tu za kihispania zimehit worldwide...hyo inaonyesha kuwa ni dhahiri lugha sio kikwazo.
 
Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
623
1,000
Umeongea point, maana kuna series nyingi tu za kihispania zimehit worldwide...hyo inaonyesha kuwa ni dhahiri lugha sio kikwazo.
Umeona eeh. Yaani mtu wa nje akiiangalia atajiuliza hivi wa tz ni afro american wannabes?
Haya maajabu yapo Tanzania tu hakuna nchi wanatengeneza movie na kulazimisha wawe na accents ambazo sio zao.
 
leroytz

JF-Expert Member
May 22, 2016
682
500
Umeona eeh. Yaani mtu wa nje akiiangalia atajiuliza hivi wa tz ni afro american wannabes?
Haya maajabu yapo Tanzania tu hakuna nchi wanatengeneza movie na kulazimisha wawe na accents ambazo sio zao.
Sure Mkuu inabidi tubadlike kwa kweli
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,287
2,000
Kwa kasoro ulizotaja huwezi sema ni nzuri
Sema Tu ina kasoro nyingi

Halafu aeries kwenye insta page
Inaingizaje hela? Anyone?
 
Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
623
1,000
Kwa kasoro ulizotaja huwezi sema ni nzuri
Sema Tu ina kasoro nyingi

Halafu aeries kwenye insta page
Inaingizaje hela? Anyone?
Siwezi kusema ni mbaya moja kwa moja ukiiangalia ndo utanielewa.
Kuhusu kuwepo kwenye Instagram page sielewi wana nia gani sidhani kama ilikuwa the best option.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
22,788
2,000
Kwa kasoro ulizotaja huwezi sema ni nzuri
Sema Tu ina kasoro nyingi

Halafu aeries kwenye insta page
Inaingizaje hela? Anyone?
Wakati mwingine ukitaka kum-convince investor/network unawaonyesha kwa vitendo jinsi ambavyo kazi yako itauza. And the best way to do that is to do a test run, see how people will receive your product then move it to a paying network. I assume that's what they are doing.
 
Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
623
1,000
Wakati mwingine ukitaka kum-convince investor/network unawaonyesha kwa vitendo jinsi ambavyo kazi yako itauza. And the best way to do that is to do a test run, see how people will receive your product then move it to a paying network. I assume that's what they are doing.
Hopefully that's what they're doing.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
22,788
2,000
Wordsworth I can tell your criticism is meant to build these guys up....kudos to that.👊👊 maana watu wengine wamegoma kabisa kumove on from "the jinni looking both sides before crossing the road" era.

Here are my 2 cents......

#1 . You are right about the ADR thingy. Kibongo bongo bado sana kwenye swala la ADR. Watu hawajui kuhusu foley wala ambiance. Wanadhani ukisharekodi sauti za maongezi ikawa clear basi kazi imeisha. Binafsi sijui Max anafeli vipi wakati amekuwa aki-deal na sound recording kwa muda mrefu na ana studio na producer at his disposal. They can do muuuuuuuch better in that department.

#2 . Lugha.
Kwenye hili napingana na wewe kwasababu kuu tatu... 1) Imekuwa kawaida kwa Watanzania wa middle - high class kwenye mazingira yetu kuzungumza kiingereza kwenye mazungumzo yao ya kawaida kwa asilimia ya kuridhisha. 2) Kwa asilimia kubwa wengi wetu tumekuwa wahanga wa kuchanganya lugha mtaani na hata kwenye mazingira ya kazi. 3) Accents nazo zime-improve kutokana na mchanganyiko/mazingira na TV. Ile mambo ya kumtambua mtu haraka kwa accent yake anapoongea Kiingereza yamepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma. Temba/Max ni mmoja ya watu wasio na ile accent ya kibongo bongo....so kwa wewe ku-judge character zao kwa kuongea kiingereza kisichosound kama kinazungumzwa na mswahili sio fair.

#3 . Dialogue kukosa uhalisia.
Hii haitokani na muandishi kujua ama kutokujua lugha vizuri. It's lack of creativity more than anything else. Kwanini nasema hivyo??? Kwasababu dialogue anazoandika mwandishi zinaweza kugeuzwa geuzwa na msanii chini ya uangalizi wa Director mpaka i-sound natural to that particular person. Yani kitu kinaweza kusound vizuri kwenye kichwa cha mwandishi all the way to the paper ila mtu akiongea out loud ndo unaona it sounds a bit weird.

#4 . Sounding stiff & Robot-like.
You are absolutely right. Wanatakiwa wa-slow down a little, take some time and actually feel what they are saying badala ya kukariri tu na kusema mistari yao.

All in all wakiendelea kujifunza na kubadilika kutokana na makosa they'll make a huge difference in the industry.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,287
2,000
Max level zake ashirikiane Tu na multi choice.
Wamuunge kwenye Portal amtafute waandishi hata nje ya Tanzania..

Max anaweza Sana kutafuta sponsors..why ashindwe hili?
 
Bora umenisaidia kuelezea vizuri kwenye sound.
Inaonekana unaielewa film na television industry vizuri.
Hapo kwenye lugha nimekuelewa ila bado nakazia wanashindwa kuexecute vizuri. Mbona Vanesa Mdee na yeye hana accent ya kitz lakini akiongea yupo natural hayupo fake? Mimi mwenyewe hapa sina kabisa accent ya kitz na wala sijawahi kuwa nayo na ninakuelewa unapo sema kuna watu wanaongea kama Wamarekani. Lakini huyo Max/Temba mbona anaongea kama mbongo ambaye ana lazimisha kuwa na Afro American accent? Na siyo yeye tu ni karibia waigizaji wote pale wanalazimishia na inakuwa cringy.
Ndio maana mi nikaona nibora wangeacha kabisa cause it sounds so fake.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
22,788
2,000
Max level zake ashirikiane Tu na multi choice.
Wamuunge kwenye Portal amtafute waandishi hata nje ya Tanzania..

Max anaweza Sana kutafuta sponsors..why ashindwe hili?
Who said ameshindwa???

It might just be a strategic move on his part.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
22,788
2,000
Bora umenisaidia kuelezea vizuri kwenye sound.
Inaonekana unaielewa film na television industry vizuri.
Hapo kwenye lugha nimekuelewa ila bado nakazia wanashindwa kuexecute vizuri. Mbona Vanesa Mdee na yeye hana accent ya kitz lakini akiongea yupo natural hayupo fake? Mimi mwenyewe hapa sina kabisa accent ya kitz na wala sijawahi kuwa nayo na ninakuelewa unapo sema kuna watu wanaongea kama Wamarekani. Lakini huyo Max/Temba mbona anaongea kama mbongo ambaye ana lazimisha kuwa na Afro American accent? Na siyo yeye tu ni karibia waigizaji wote pale wanalazimishia na inakuwa cringy.
Ndio maana mi nikaona nibora wangeacha kabisa cause it sounds so fake.
Yeahh..to some extent 😉😉

When you put it like that...I agree!

There is still a lot to be done in that department. Haswa upande wa Director maana yeye ndo anaweza ku-influence how an actor delivers his/her lines. Ubaya ni kwamba Director ndo anaweza kuwa na hiyo weakness and he is rubbing it off on his/her actors akidhani ndo sahihi.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,287
2,000
Bora umenisaidia kuelezea vizuri kwenye sound.
Inaonekana unaielewa film na television industry vizuri.
Hapo kwenye lugha nimekuelewa ila bado nakazia wanashindwa kuexecute vizuri. Mbona Vanesa Mdee na yeye hana accent ya kitz lakini akiongea yupo natural hayupo fake? Mimi mwenyewe hapa sina kabisa accent ya kitz na wala sijawahi kuwa nayo na ninakuelewa unapo sema kuna watu wanaongea kama Wamarekani. Lakini huyo Max/Temba mbona anaongea kama mbongo ambaye ana lazimisha kuwa na Afro American accent? Na siyo yeye tu ni karibia waigizaji wote pale wanalazimishia na inakuwa cringy.
Ndio maana mi nikaona nibora wangeacha kabisa cause it sounds so fake.
Inaonekana wewe ni mdau WA hii industry
Ukiwa na kazi zako tuletee tuone
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom