Kuhusu viwanja vya mpira: Polepole kasema Uongo

M CM

JF-Expert Member
Nov 25, 2012
2,495
1,477
Amesema kuwa CCM ilitumia rasilimali zake kununua ardhi then wakajenga viwanja vya mpira.

Na amesema kati viwanja 23 CCM inamiliki 22. Kwa taarifa za uhakika nilizozipata ni kwamba viwanja vyote vinavomilikiwa na CCM zimejengwa kwa nguvu za wananchi wote wa Tanzania tena wasio na chama.

Na viwanja vingi vilijengwa kutokana mzunguko wa sherehe za Uhuru kila mwaka. Kwa maana hiyo viwanja hivyo si Mali ya watanzania wote? Nawasilisha
 
kwanini Chadema hawaei kuchallenge hii ishu mahakamani?
Nazungumzia hili kwa kuwa viongozi wetu wanajinasibu kuwa ni waadilifu.Kama ccm wanataka wamiliki Mali halali basi warudishe Mali ya watanzani wote. Nasema hili kama raia wa kawaida ambaye mzazi wangu ambaye hakuwahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini alichangia ujenzi wa viwanja.
 
Chadema imewashinda hata kujenga ofisi yao tu,
Kazi kujifanya wanajua kila kitu kuhusu Mali za wengine!!

Shame on you
Sijawahi kuwa mwanachama wa chadema wala ccm na nitabaki kuwa raia wa kawaida. Ila upo toa dukuduku ni lazima uwe chadema?
 
Mahakama ilishatolea uamuzi suala hili.
kesi ilifunguliwa CCM wakashinda? nafikiri ni kesi ambazo zinatakiwa kati ya halmashauri za miji vs CCM. mfano uwanja wa Sokoine iwe halmashauri ya jiji la Mbeya vs CCM. ilikuvyo au ilikuwaje?
 
baada ya mfumo wa chama kimoja kufa ilitakiw baadhi ya mali za ccm zirudi serikalin maana upatikanaji wake uligharimu jasho la watanzania wote.....
 
Kuna halmashauri moja jina kapuni ilipambana na ccm baada ya kuona ccm wanataka kuchukua uwanja wa shule ya msingi. Halmashauri ilishinda na uwanja ukabaki Mali ya shule
 
Polepole toa uthibitisho wa TANU au CCM kununua Kiwanja Na kampuni zilizojenga .Viwanja vyote vimejengwa Na watanzania bila kujali chama watu wamekatwa mishahara, wameuza mifugo kuchangia viwanja
 
ni moja ya makosa yaliyofanyika 1992 wakati vyama vingi vinaanza na nyerere mwenyewe anayejua ukweli alikuwa hai.kulikuwa na haja ya kuwasikiliza wananchi wengi waliopenda CCM iendelee hadi siku tutakapoamua wananchi wenyewe hapo ndio maswali kama haya yangehojiwa vizuri.
Kuna jamaa mmoja anasema wao walikuwa wanatoka shule wanakwenda kushiriki ujenzi wa CCM Kirumba.

Hivi vyanzo vya mapato vya CCM enzi hizo vilikuwa ni nini?
 
Polepole toa uthibitisho wa TANU au CCM kununua Kiwanja Na kampuni zilizojenga .Viwanja vyote vimejengwa Na watanzania bila kujali chama watu wamekatwa mishahara, wameuza mifugo kuchangia viwanja
Huo ndo uhalisia halafu polepole anadai viwanja vimetokana na uwekezaji wa chama
 
baada ya mfumo wa chama kimoja kufa ilitakiw baadhi ya mali za ccm zirudi serikalin maana upatikanaji wake uligharimu jasho la watanzania wote.....

wakati vinajengwa vilijulikana kama ni viwanja vya ccm! sasa kama ulikuwa unajenga wakati huna chama ulikuwa unawachangia ccm! ni kama leo chadema wanavyotangaza harambee watu tukachangia hata bila kuwa mwanachama.

pia kama unataka kumiliki mali za ccm, jibu ni simple tu, jiunge na ccm uwe mmoja wa wamiliki kwani hakuna aliyekufukuza au kukukataza kujiunga na ccm.

mwanamke aliyeachika mwenyewe hana haki ya kugawana mali alizochuma na mmewe! maana kama akizitaka kuzitumia mumewe humwambia aje aishi nae wazitumie! na hata akienda mahakamani hushindwa kwa hoja hiyo.. hakuna aliyekufukuza! kama unataka nyumba njoo tuishi pamoja tuitumie wote.
 
baada ya mfumo wa chama kimoja kufa ilitakiw baadhi ya mali za ccm zirudi serikalin maana upatikanaji wake uligharimu jasho la watanzania wote.....

na ukumbuke kuwa! baada ya kuruhusu vyama vingi hakuna aliyesema kuwa baadhi ya wanachama wa ccm waondoke kuunda vyama vingine! no no no.. waliondoka kwa kujitakiwa wao . so hawana haki ya kudai vya ccm! kama wanataka wende huko huko ccm watumie pamoja
 
Hivi huyu "slow slow" bado mnamtilia maanani! Huyu alishalishwa kitu na keshasahau yote aliyokuwa akiyasimamia.
 
Back
Top Bottom