CCM MKAMBARANI
JF-Expert Member
- Mar 15, 2017
- 1,379
- 950
Kwa jinsi nimechukia sina haja ya kutoa salamu, moja kwa moja katika mada.
Ni kuhusu mkutano wa leo mjini Dodoma kati ya wana CCM wakongwe wakijaribu kutuvisha vijana koti la ujamaa kwa nguvu. Ni kuwa suala hili haliwezekani tena, huyu mzee anaeshupalia ujamaa inapaswa atuambie kwa namna gani serikali inaweza kutupeleka mbali kupitia ujamaa wa akina Mzee Nyerere na wenzie.
Babu Butiku anajenga Hoja ya kutupotosha na kutufanya vijana kuwa hatujui hasara za ujamaa. Labda mzee atuambe kuwa anataka ujamaa wa kizazi kipya lakini si ule wa mzee Nyerere. Kwa hakika uchumi hauendeshwi na serikali badala yake huendeshwa na watu binafsi huku serikali ikiwa na macho makali kwa ajili ya kuweka sawa mizani flaniflani ya kiuchumi.
Katika nadharia za kijamii yaani sayansi ya jamii ni kuwa Taifa hili haliwezi tena kuwa na ujamaa, hii inatokana na mambo mengi mosi, mfumo wa elimu haujaandaa watu haswa wanafunzi kuja kuwa wajamaa, pili, dunia ya leo imejaa vitu ambavyo kwa hakika kila mtu angetamani apate.
Hebu nikuulize Mzee Butiku, Mtoto wako Peter yuko wapi na anafanya nini? Je ni Mjamaa wa maneno au porojo? Je umewahi kupunguza zile billion 19 zako ambazo umehifadhi benki kwa kusaidia watz wenzio? Mbona unakuwa mnafiki mzee, kwanini lakini?.
Mwisho; Mzee Butiku usidanganye vijana,unachotakiwa kufanya ni kusema tufanye kazi na kuhamasisha serikali iweke mazingira safi, usiturudishe katika wimbi la umasikini, mzee Butiku unadanganya. Huu ni msimamo wangu na si Uvccm.
Ahsanteni.