Kuhusu sherehe za Muungano, mbona Magufuli ndio katoa hotuba peke yake na Shein hakufanya hivyo?

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,748
15,669
Husika na kichwa cha Habari hapo juu... nimefuatilia vyema sherehe za muungano na nimeona Mheshimiwa JPM peke yake ndio katoa neno katika sherehe hizi na Dr. Shein hakupewa nafasi kama Rais pekee wa serikali ya Zanzibar "

Wajuzi wa mambo haya ningependwa kujuza Hii imekaaje binafsi ningependa pia Dr. Shein angepewa nafasi ya kutoa neno katika sherehe hizi.
 
Shein akija Bara, ni kama mkuu wa mkoa au Mbunge kutoka Zanzibar. Kwahiyo hawezi anaongea kitu kwenye Mkoa au jimbo la mtu mwingine.
 
Husika na kichwa cha Habari hapo juu... nimefuatilia vyema sherehe za muungano na nimeona Mheshimiwa JPM peke yake ndio katoa neno katika sherehe hizi na Dr. Shein hakupewa nafasi kama Rais pekee wa serikali ya Zanzibar "

Wajuzi wa mambo haya ningependwa kujuza Hii imekaaje binafsi ningependa pia Dr. Shein angepewa nafasi ya kutoa neno katika sherehe hizi.
kwani zamani ilikuwa inakuwaje? maana unaongea kama ndo tunasherekea kwa mara ya kwanza..
 
Aisee kama hajaongea itakuwa ITIFAKI HAIJAZINGATIWA mkuu...

Labda wana sababu zao maalumu ambazo mimi na wewe hatuzijui
 
Nadhani hakukuwa na umuhimu wa yeye kuongea

Ila Magufuli nimempenda leo katoa hotuba fupi na yenye maneno mazuri yaliyoendana na cku yenyewe
 
Huu uzi unanikumbusha jemedari John Okelo, the father of Zanzibar Islands. Walijitahidi sana hasisike ila muda ndio ukaongea na kumtambulisha.
 
Husika na kichwa cha Habari hapo juu... nimefuatilia vyema sherehe za muungano na nimeona Mheshimiwa JPM peke yake ndio katoa neno katika sherehe hizi na Dr. Shein hakupewa nafasi kama Rais pekee wa serikali ya Zanzibar "

Wajuzi wa mambo haya ningependwa kujuza Hii imekaaje binafsi ningependa pia Dr. Shein angepewa nafasi ya kutoa neno katika sherehe hizi.

Sherehe ya Muungano inafanyika kwa kupokezana Bara na Zanzibar, next year itakuwa zamu ya Zanzibar na Shain ndio ata run show
 
Suala la muungano siyo la kuhoji ovyo ovyo km mnavyokejeli. Siri za muungano mm na ww hatuzijui; yanini kukaa kuhoji muungano? Mara Dr shein mara Zanzibar coloni la Tanganyika siku zenu zinafahamika
 
Awamu hii mtazoea tu kuwa kuna Mkuu na wakuu walio chini yake.

Nimependa ilikuwa maonyesho zaidi kuliko hotuba ndefu, kabla yake mtu ulikuwa hadi unakimbia kuangalia matukio kama haya.

Naamini kwa mara ya kwanza ratings za walioangalia makwao lazima zilikuwa juu tangu tupate Uhuru.

Hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom